Kwanini mahusiano/ndoa nyingi hazidumu?

ndoa si harusi na harusi si ndoa.. wakiweza kudadavua haya maisha yatakuwa mepesi sana
 
Kila nikiwazaga kuoa naona bdo kichwa changu akijatulia kukaa na mtu 1 ndani" Ndoa si kitu cha mchezo
 
Wengi huwa hatujiulizi maswali hayo.
 
Kimsingi ndoa ni jambo jema na lenye kuleta faraja kubwa sana maishani kwa wana ndoa. Mambo sio mabaya kama hivyo yanavyotiwa chumvi, kuna ndoa nyingi zimedumu kwa upendo, furaha na amani. Asiliamia kubwa ya wana ndoa wana maisha bora zaidi kuliko waliyokuwa nayo kabla kuoa au kuolewa. Ndoa zimewafanya wamekua kiakili na kutambua majukumu kimaisha katika jamii. Kuoa au kuolewa kunatimiza misingi mikuu ya maisha ya mwanadamu. Ndio kuna changamoto za hapa na pale hazikosekani lakini hiyo ni kawaida ya maisha, bila changamoto hakuna maisha, changamoto zinatufundisha kukomaa na kujenga ukaribu wa wanandoa, hata ukiishi na wazazi, ndugu lazima mikwaruzano ya hapa na pale ijitokezee, huwezi kuacha kuishi kwsabababu kuna matatizo katika ndoa. Ndoa moja ya ndugu au rafiki kuwa mbaya au kuvunjika haina maana kwamba 'Ndoa Hazidumu Siku Hizi' na kupelekea kuchochea mawazo mabaya kuhusu ndoa. Inasikitisha kuona vijana wengi wakiwa na mawazo hasi kuhusu ndoa wakati wala hawajaingia katika ndoa. Ni faraja ilioje unaporudi nyumbani kwako jioni baada ya siku ndefu na ngumu kazini unakuta angalau kuna mwenzako wa kumshirikisha jinsi siku yako ilivyoenda leo. Tuitazame ndoa kwa mapana na marefu na sio kirahisi rahisi tu na kejeli. Wanaokejeli ndoa hebu wajiulize wao wangekuwa wapi leo kama taasisi hii ya ndoa isingekuwepo.
 
Kweli tupu.
 
Hill halinihusu. kuoa haimo katika mipango yangu ya maisha. ukitaka kupoteza furaha ya maisha yako, oa/olewa.
Nakubali kabisa.duuh iko wap furaha yangu na tabasamu langu nilipokuwa single.daaah limepotea
 


Unafaa kuwa waziri wa jamii ya baadaye kwa Tanzania. Unaongea point nzuri sana na kama ungekuwa karibu ningekupa kaji-offer. Ni kweli uyasemayo na ilibidi Magufuli akuundie wizara uwe waziri wake. Big up.
 
Kati ya vtu ninavoviogopa ni ndoa nikiona watu walioolewa na kuoa wanavoteseka. Mwanaume anaoa michepuko daily migogoro. Nadhani before entering kwenye marriage lazima kujiandaa kiakili kimwili na kiroho na kuacha mambo yote na kuwa committed haswa pia kuwa na hofu ya Mungu bila hivo aisee
 
Kinachoniboa ni hii culture ya michango jamannii,si tulage dinner tu hivi watu wachache afu basi
 
hahaaaaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…