Kwanini mahusiano/ndoa nyingi hazidumu?

kutokua na utayari wa uwajibikaji ndani ya ndoa, watu wengi hufikiri zaidi ile siku husika ya harusi bila kufikiri maisha baada ya harusi,

kuingia kwenye ndoa kwa sababu ya kitu fulani either ujauzito au shinikizo kutoka kwa ndugu jamaa hata wazazi,
utandawazi unachangia pia na kutoelewa nn wajibu wako kama mwanandoa
tamaa wengi hawajui kusema na nafsi zao na kutokua na hofu ya Mungu
 
watu hawajui nini maana ya ndoa ndo maana wana mbwela mbwela
 
Hivyo vyote ulivyotaja vimo. Pia vijana wengi wanaanza mapenzi wakiwa wadogo mpaka aje afikie umri wa kuolewa kesha badilisha wapenzi si zaidi ya mmoja. Na ukishakuwa hivyo hutaweza kukaa kwenye ndoa salama bila kukumbuka zilipendwa.
Pia wapo wasioridhika na hali ya kipato cha wapenzi wao. Yaani hawa wapo kimaslahi zaidi. Utapendwa pindi unazo ila ukiishiwa umeachwa....
Karbuni wengine jamani tupo darasani[emoji310]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…