Kwanini majina mengi ya wangoni yapo hivi?

Oscar Wissa

Senior Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
108
Reaction score
170
Majina mengi ya wangoni yanafanana na majina ya wanyama. Kwa mfano;

Mapunda ni jina lenye "punda"
Komba ni jina lenye "komba"
Ngonyani ni jina lenye "nyani"
Mapunda ni jina lenye "punda"

Kuna majina mengine mengi pia...

Naomba kujua kwanini majina mengi ya wangoni yapo hivi?
 
Pana sehemu kiongozi mkubwa alikwenda wakamwambia muheshimiwa tunakupenda sana leo utakula Nanguruwe na kulala Nanguruwe.
 
Kuna Nguruwe alikuwa Rpc miaka ya nyuma hapa Dodoma!
 
Pana sehemu kiongozi mkubwa alikwenda wakamwambia muheshimiwa tunakupenda sana leo utakula Nanguruwe na kulala Nanguruwe.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Mkuu hiyo wangoni hatuhusiki hao ni wadau wa mtwara labda na tunduru nd kweny majina ya muundo huo
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Mkuu hiyo wangoni hatuhusiki hao ni wadau wa mtwara labda na tunduru nd kweny majina ya muundo huo
Ndio wale wale majirani zenu akina njomba nchumali mara chipoku.
 
Ni wangoni hawa wa jamii ya kizulu walioshindwa vita vya kugombania ardhi enzi za ubabe wa bwana shaka, shaka zulu wakaamua kutafuta makazi nje ya zululand.

Historia ya wangoni ilitawaliwa na vita vya mara kwa mara vya kugombania ardhi kule zulu land na all the way from south africa to milima ya songea.

Hawa mabwana ili kujipambanua sifa na uwezo walionao katika vita au maisha mengine ya kawaida koo mbalimbali walijipa au walipewa majina ya wanyama ili kusadifu uwezo au udhaifu wao kama alama ya utambulisho.

Koo zenye nguvu na za kibabe au wawindaji hodari walijipachika au walipachikwa majina ya wanyama kama vile simba, faru, tembo n.k.

Wale waoga, wanyonge, watumwa na wadhaifu ndio hawa akina mbawala, komba, nguruwe, punda n.k.

Wale wanjanja wajanja, walaghai, zulumati na matapeli ndio hao akina sungura, nyoka, nk.

Kuna historia kubwa sana wangoni sio rahisi kuiandika yote hapa hususani ubabe wao kwenye vita, utani na makabila mbalimbali.

Lkn wangoni wa leo sijui wamekumbwa na nini ni waoga kupindukia, sifa kubwa waliyobakiza ni kuichagua ccm na kupenda wanawake kuliko hela[emoji24][emoji24][emoji24]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Nyumbi hii bombi hii, wazee wa mfalanyaki bombi mbili. Watani zangu hawataki kwenda mbali kuhangaika kutafuta majina, Fungo, mapunda, matembo kwisha habari.
 
....Sifa kubwa walizobaki nazo ni kuichagua ccm, kupenda mademu na kulewa pombe🀩🀩🀩
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…