A
Ameacha hizo milioni 300 kwa sababu anazo zingine trilioni tatu kwani biashara ya nyara za serikali sio mchezo alafu unajumlisha na vitalu vya kuwindia acha bwana. Sasa hivi tunashangaa tembo wamejazana wanahamia mijini hata wale waliokimbia nchi wamerudi kutoka Msumbiji.
Tatizo Chadema wengi hamjui kitu mnachafua watu bila sababu kama Mlivyomchafua Kinana baadae makamuomba Msamaha.
Ndio maana Mh . Rais anapiga marufuku mikutano yenu ya walevi ya kuchafua watu na kuzusha.
Hivi unajua kuwa Lazaro Nyalandu ndiye akiwa waziri wa Mali asili ndiye aliyeleta ndege na zile drone za kufanya doria kulinda Wanyama wetu wasimalizwe na Wasomali waliokua wanashirikiana na watu ndani ya Hifadhi ?
Unajua kuwa Kabla ya Lazaro, askari wa wanayama pori hawakua wanatumia silaha za Kivita kama AK 47 bali walitumia Short Gun kama wawindaji matokeo yake Majangili yaliyokua na Silaha za kivita walikua wanaingia Kwenye hifadhi kama ukumbini na kuua wanayama wetu??
Unayajua hayo au umepewa Konyagi na Mbowe unabaki kutokana watu walioliletea taifa letu sifa kubwa lakini wakachafuliwa kwa sababu ya woga wa Makundi ya urais ndani ya CCM.
Nyarandu ndiye aliyebadili mfumo nzima wa mafunzo ya askari wa wanayama pori na kuwa mfumo wa kijeshi na kuletewa silaha mpya kabisa za AK 47 na magari ya Land Cruiser na ndipo askari wetu walipoanza kuwazidi nguvu Majangili.
Ulikua unayajua hayo?
Serikali ya JK ilifanikiwa sana kujenga Majeshi yetu katika zana za kivita ndio maana awamu ya Tank haikupata shida kwenye suala la ulinzi.
Nchi ni majeshi kuwa imara. Usione vinaelea ujue vimeundwa.
Kumbuka wakati ule alivyomnyanyua yule askari mdogo wa wanayama pori aliyekua mahiri katika matumizi ya Silaha na mbinu za kivita ,walevi kwa makengeza yao wakabaki kusema eti amemshika Mwanamke na kumbeba badala ya kueleza tukio zima wakabaki wanasambaza picha bila maelezo.
Kabla ya awamu ya Tano vita dhidi ya Majangili ulikua Kali sana lakini makundi ndani ya CCM na Uhuru wa Bunge ulisababisha ile vita ikashindwa mana tume zilikua zinaundwa kila siku kuiwajibisha serikali kwa matumizi ya nguvu kupita kiasi .
.Unakumbuka Operation Tokomeza ujangili ilianza lini ? Au mnakua vipofu kwa kuvaa miwani??
Unakumbuka nini kilitokea baada ya Majangili kuwa yanauliwa kama kumbikumbi wakati wa kiangazi. ??
Bunge liliunda Kamati na mawaziri walijiuzulu wa wizara zaidi ya tatu walilazimishwa na Bunge wajiuzulu.
Hali hii ya wapinzani kuzusha jambo na kupaka watu matope ndilo lililopelekea Awamu ya Tano kudhibiti Bunge,vyombo vya habari na wanasiasa walevi wanaochafua watu huku wakitumia Bunge na vyombo vya habati kupata umaarufu kwa kuchafua watu.
Kwa siasa hizo za maji taka Bora Magufuli atawale mpaka miaka 40 yaani vipindi nane ili tujenge siasa za kistarabu.