Kwanini makamo wa rais atoke zanzibar? Sioni mantiki yake!

Kwanini makamo wa rais atoke zanzibar? Sioni mantiki yake!

Nyerere alipounganisha Tanganyika na Zanzibar alikosea kwenye assumption yake ya " HIVI TANGANYIKA KWELI INAOGOPA KUMEZWA NA ZANZIBAR?".
Sasa watanganyika wameanza kuogopa kumezwa na Zanzibar, wameanza kuhofia uwakilishi kutoka Zanzibar kwenye serikali ya muungano usiozingatia ukubwa wa maeneo ya uwakilishi na wingi wa watu.

Wazanzibar nao wameendelea kudai share kubwa katika pato la muungano kuzidi hata uwiano wa watu wa nchi hizi mbili.

Kama Inakusudiwa muungano uendelee kuwa katika hali hii iliyopo sasa ya serikali mbili, ninawasiwasi kwamba huu muungano hauna muda mrefu.
Suluhisho la muungano ni Serikali moja, na wala siyo serikali tatu, serikali tatu itakuwa mzigo kwa Tanganyika.
Suluhisho jingine ni muungano kupitia EAC, kwa hiyo tunaweza kuvunja muungano wa sasa, kisha tutakutana huko kwenye EAC, ambako lengo mojawapo ni political federation siku moja.
 
Sijakataa kuwa hilo jambo limo ndani ya Katiba. Nionavyo mimi hao walioandika kipengele hichi Katiba walilifanyia uchunguzi suwala hili? Huu ulikuwa ni uamuzi wa papo kwa papo wa CCM waliokuwa wakifikiri kuwa hii nchi ni yao peke yao. Sioni mantiki ya kuwepo Makamo wa Rais iwapo Rais anatoka Bara. Tuchukulie mfano wa DR Gharib Bilali hivi sasa yuko kumsaidia Kikwete kwa upande gani, Tanganyika au Zanzibar. Zanzibar kuna Rais wake na ndie mwenye mamlaka ya serikali ya Zanzibar na hata siku moja kwa kipindi cha miaka zaidi ya 15 toka uanze utaratibu huu, Makamo wa Rais hajawahi kushughulikia mambo ya Zanzibar.
Nimekuwa nikijiuliza kati ya Makamo wa Rais na Rais wa Zanzibar nani ana mamlaka makubwa na nikijiuliza sana kwanini Makamo wa Rais wa Tanzania anaacha kazi ya umakamo na kuwa Rais wa Zanzibar.

Umeuliza swali kwa wana jf, wanakujibu then unakaidi-sasa wee unatakaje? Hebu lete fikra zako basi tuchangie katika muktadha huo.
 
Mkuu.
Huu mkorogo utapungua kama tutairejesha serikali ya Tanganyika.
kama tunakubali au tumetambua sasa kuwa serikali ya Tanganyika haipo basi la kufanya ni kuirejesha serikali ya Tanganyika.
Tatizo litakuwa limetatuka au vipi?
Hakutakuwa na umuhimu wa Tanganyika kuwakilishwa katika serikali ya Zanzibar wala Zanzibar kuwakilishwa kwenye serikali ya Tanganyika.

Uwakilishi wa Tanganyika na uwakilishi wa Zanzibar utahusu kwenye serikali ya Muungano pekee.

Kwa nini Watanzania tunapenda kufanya mambo kuwa magumu na mkorogo wakati hata mtoto wa darasa la pili anajua utatuzi wa mkorogo wenyewe?

Hivi wajemeni, kwa nini hatuzungumzii kuirejesha serikali ya Tanganyika?
Au sote tumekuwa CCM? Tunataka kutekeleza sera ya kutoka serikali mbili kuelekea moja?
Mtumiabusara ni wakati wa kutumia busara!

Sioni mantiki ya kutaka aliyenacho apoteze alichonacho lakini busara ingesema kuwa asiye nacho basi afanye juhudi naye apate!
Tuache unafiki wakuu! Hapa hapana tatizo kubwa, tatizo ni sisi wenyewe hatutaki kudai Tanganyika na serikali ya Tanganyika ambayo haipo wazi wazi.
This leaves me wonder what a game is this? Badala ya sisi kulilia serikali yetu irudi, tunapiga mayowe wao waue serikali yao!!

Are we still sane?
Who brain-washed us?

Mkuu, kwa nature ya Wazanzibari inavyojionyesha, huu mkorogo utakwisha kwa kutokuwa na Muungano tu, japo still watalamika kuwa wanafanyiwa fitna na watanganyika! Hebu jaribu kufikiri kila mtu kwao si mzanzibari, Mwinyi siye! Karume siye! Lakini ukimtaja Seyyid Said watakwambia huyo ndo kindakindaki, yaani ni vurugu match-So hakuna haja ya Serikali ya Tanganyika wala nini kutokuwa na Muungano-hii biashara ya changu changu, chako chetu haina nafasi tena kwa sasa.
 
suala la makamu wa raisi ni tata ukizinagatia katiba ya Tanzania imekuwa ikizibwa viraka kwa manufaa ya CCM, kiutendaji makamu wa raisi yupo tu kiaina aina kuliongezea mzigo taifa, katiba yetu inabidi iandikwe upya kwa faida ya watanzania wote, vinginevyo tutaendelea kuumizana vichwa.
 
We unauliza kitu kisichokusaidia kitu, uliza kwa nini mawaziri wote wa ulinzi watoke zanzibar?
 
Wazee..kubwa hapa ni jinsi wajamaa walivyojipanga katika kuhakikisha wanaweza kututawala watakavyo sasa kwa kuwa awali hutukuweza kuvuka maji kabla hatujayaona naomba tusiende mbali zaidi tuingie kwenye mchakato wa kuipata mpya kwanza halafu tukiipata tutaona nini mapungufu ya katiba ya awali ili tuweze kusonga tukijua tusije kurejea kwenye tope ambalo awali lilituzamisha.

Hata hivyo tuishikuru katiba ya mwaka 1977 ambayo imetufikisha sasa,tusingeyaona kama tungeendelea kulala na hasa pongezi za dhati kwa vyama vya upinzani vilivyopo hapa nchini bila kumsahau MTIKILA ambaye aliweza hata kufika mahakamani kwa niaba ya watanzania kuipinga katiba ya 1977.
 
Mkuu, kwa nature ya Wazanzibari inavyojionyesha, huu mkorogo utakwisha kwa kutokuwa na Muungano tu, japo still watalamika kuwa wanafanyiwa fitna na watanganyika! Hebu jaribu kufikiri kila mtu kwao si mzanzibari, Mwinyi siye! Karume siye! Lakini ukimtaja Seyyid Said watakwambia huyo ndo kindakindaki, yaani ni vurugu match-So hakuna haja ya Serikali ya Tanganyika wala nini kutokuwa na Muungano-hii biashara ya changu changu, chako chetu haina nafasi tena kwa sasa.
Mkuu,
kutokuwa na muungano, kutatubakishia serikali ipi?

Hapa si suali la ulalamishi wa Zanzibar..kuwa na serikali ya Tanganyika itakuwa ni kujitayarisha kwa sisi kuendesha yale mambo yasio ya Muungano ,nje ya serikali ya Muungano.
Pia itapunguza msuguano, wao hawataingia katika Bunge la Tanganyika au baraza la wawakilishi la Tangannyika.
Bunge la Muungano na serikali ya Muungano itapungua ukubwa wake pia.

Surely, kuwepo kwa serikali ya Tanganyika kutapunguza mkorogo na kuweka mipaka ya kiutawala baina ya serikali ya Tanganyika, serikali ya Zanzibar na serikali ya Muungano(Tanzania).
 
Back
Top Bottom