Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Kuna namba yangu ya simu nilikuwa siitumii for almost 3 years kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu. Baadae nikagundua ile namba amepewa mteja mwingine. Just imagine nimeitumia namba ile for almost 10 years, halafu kampuni husika inaamua kuigawa kwa mteja mwingine. Jamaa na ndugu zangu wakawa wanaipiga namba ile inaitika kwa mtu mwingine. Hii ikawa kero kubwa.
Kama hiyo haitoshi, juzi kati hapa nimesajili namba nyingine ya Mtandao mmoja hivi wa simu, kila siku napokea simu atleast 3 za watu wanaonipigia ambao hatufahamiani kabisa, watu hao wanaulizia jina la mtu ambaye nimebaini itakuwa ni mtu aliyekuwa akiitumia namba hii miaka ya nyuma.
Swali langu sasa: Ni kwa nini Makampuni ya simu yanalazimika kuhuisha namba za simu za wateja wa zamani na kuwapa wateja wapya? Je, teknolojia imeshindwa kutumika kuanzisha namba mpya na kuachana na namba zilizotumika zamani? HII IMEKUWA NI KERO KUBWA SANA kwa Observations zangu.
Stop this please.!