Kwanini Makampuni ya Simu yanalazimika kuhuisha namba za wateja wa zamani na kuwapa wateja wapya?

Kutok Unadhani ubunifu pekee wa kukabiliana na changamoto ya kulipia hicho unachoita masafa mapya ni kuwapa wateja wapya namba za wateja wa zamani? Wamekosa kuja na ufumbuzi mpya zaidi ya huo?

Je, umezitazama changamoto za wateja wapya kutumia namba zilizotumika na wateja wa zamani na kujiridhisha kuwa changamoto hizo kwa wateja ni kitu cha kawaida tu ukilinganisha na hasara wanayoikwepa?
 
Nilishawai kuokota line ya simu nikatuma buku kwenye Mpesa ili kuona salio nikaona kweli kuna salio kiasi ila sikuwa na uwezo wa kuitoa sababu ya nywila Nikaacha kuitumia for 3 months, Ile nakuja kuiweka kwenye simu nikaenda kwenye M-Pesa ikanambia set new Mpesa nikaset nywila mpya yale maokoto bado yalikuwepo sikuzitoa zile ela but nilikuwa nazinunulia salio mle mle nikitaka kumpigia watu tofauti kama maX. Nikaiacha tena kama Miezi mitano Ikafungiwa kimoja na yale maokoto 😄😄. They also making money na hizo line imagine walifungia line na maokoto yake
 
Kwanini pia wafungine line zenye maokoto ndani?
 
Siwezi kuwasema kwenye hili mkuu
 
@

Heart Wood.Angalia hii ya india:​


What happens if SIM is not used for 6 months?


In India, most of the mobile carriers deactivates the SIM card if it's inactive for a certain period of time. The period of inactivity varies from carrier to carrier, but it's generally around 6 to 9 months. After this period, if the sim card isn't recharged or used, the carrier may kill the SIM card permanently.

Nini kitatokea ikiwa SIM haitumiki kwa miezi 6?


Nchini India, watoa huduma wengi wa simu huzima SIM kadi ikiwa haitumiki kwa muda fulani. Kipindi cha kutofanya kazi hutofautiana kutoka kwa mtoa huduma hadi mtoa huduma, lakini kwa ujumla ni karibu miezi 6 hadi 9. Baada ya kipindi hiki, ikiwa sim kadi haijachajiwa au kutumika, mtoa huduma anaweza kuua SIM kadi kabisa.
 
Sasa hapa Bongo ni tofauti. Simcard isipotumika kwa muda kadhaa, wanamgawia mteja mpya. Jambo ambalo ni kero kubwa kwa watumiaji.

Mie hapa kila siku napigiwa simu na watu nisiowafahamu wastani mara tatu kwa siku kwa kutumia simcard ya mteja wa zamani. Usumbufu mkubwa kabisa hadi nataka kuiacha hii simcard.
 
Nilibiwa simu sikwenda kuripoti popote, baada ya muda nilikwenda kuhuisha namba zangu za airtel na halotel. Nafika huko kwenye ofisi zao naambiwa namba yako kapewa mtu mwingine na iko hewani. Unabaki kushangaa tu namba kapewa mtu mwingine
 
Hiki kitendo kibaya sana mimi VODACOM walitoa namba yangu kwa mtu ikiwana naTshs 35,000. Nikawahama mazima sintokuja kutumia VODACOm maisha yangu yoote.
Vodacom imekua ya kishenzi mno.
 
Nimewahi kununua line ya Voda,kumbe ilikuwa inatumika sehemu,nikaanza kupata usumbufu wa kupigiwa na watu nisiowafahamu.Mara njoo Kigamboni,utapigiwa tena njoo Chang'ombe kuna msiba..Nkaanza kujiuliza mimi siishi Dar tena nipo mbali kabisa na Dar,hawa ni akina nani.Nikiwajibu mmekosea no wanasema sawa.Siku nyingine tena unapigiwa.Aaah nilipata usumbufu karibia mwaka mzima na kuna jamaa alikuwa na sauti nzito balaa tena akawa analazimisha nimwambie kama hiyo no ni yangu mimi naishi wapi.Nikaamua kuacha kuitumia.Kumbe hiyo no kuna mtu yupo Dodoma ndio alikuwa anaitumia. Airtel nao sina hamu nao kabisa
 
Ujinga huu ungelikuwepo hata kwa T.r.a wangelitoa registration # za magari ya zamani yaliyopata ajali, kuibwa ama kutotengenezeka kwa wateja wao wapya.

Namba ya simu mtu anaisajili kwa alama za vidole Nida lakini hawajali, wao wanabeba na kuigawa kwa mtu mwingine.

Kama wameshindwa teknolojia ya kuchanganya namba, basi upumbafu huo wautumie na kwenye vocha ili tuone hadhi ya huo ujinga inavyoweza kufanya kazi ya tija!

Ni dharau kubwa sana kubeba mali ya mtu iliyonunuliwa kihalali na kuigawa kwa mtu mwingine bila ridhaa ya mhusika.

Sijawahi kusikia popote unyang'au aina hiyo ukifanya kazi.
Hauwezi kusikia mtu akilazimishwa matumizi kwa mali aliyokwisha kuinunua, jambo hilo ni la fedheha kubwa makampuni ya simu yajirekebishe.
 
Ni mapumbavu sana!
 
Shida ni serikali ya ccm TU!
 
Hata mimi tigo wamegawa namba yangu kwa mtu mwingine baada ya kutoitumia kwani nilikuwa nimesafir nje ya nchi for about 3 year.
Nikawafuata wakaniambia hawawezi kunirudishia
 
Hizi line wanazilipia Kodi, sasa imagine unalipia namba zaidi ya milioni ambazo zipo dormant
 
Hizi line wanazilipia Kodi, sasa imagine unalipia namba zaidi ya milioni ambazo zipo dormant
Ni kanuni, miongozo, Sheria dhaifu hakuna mantiki yeyote! Mbona akaunti za benki kila mmoja ana yake sijawahi kusikia ukishindwa kuiendesha wanaigawa. Tigo waligawa namba yangu kwa mtu, walinikera hadi Leo siwapendi. Wavivu wa kufikiri kuchanganya namba mbona vocha hazijirudii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…