Kwanini makocha wazawa wanafeli?

Kwanini makocha wazawa wanafeli?

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
MAKOCHA WAZAWA WANAVYOKUBALI KUACHWA NA MUDA KUELEKEA SOKA LA KISASA NA LA KISHINDNI

Tanzania ni moja ya Nchi iliyobarikiwa kuwa na vijana wengi wenye Taranta ya kusakata kabumbu kwa umaridadi mkubwa sana, kwa miaka mingi sasa Nyota wengi wamepita wakina Kitwana Manara, Abeid Mziba, Mohammed Hussein "Mmachinga", Leodgar Tenga, Bakari Marima "Jembe ulaya", Adolf Richard, Jamal Malinzi, Selemani Matola, Mussa Hassan "mgosi" na wengine wengiii.

Kwa upande wa ulaya kuna kawaida ya wachezaji wanapomaliza kalia zao za Soka huwa wanaendelea kuutumikia mpira kwenye nafasi Tofautitofauti ikiwemo ukocha na uongozi kwenye nafasi mbalimbali kwenye Soka. Kwa hapa nyumbani pia swala hili lipo Japo sio kwa kiasi kikubwa kam wenzetu kule Duniani. Kuna baadhi ya wachezaji wanaamua kukaa Nje ya Soka Mara baada ya kumaliza maisha yao ya uchezaji. Lakini baadhi yao pia wanaendelea kuhudumu kwenye tasnia ya Soka kama wachambuzi, Makocha, viongozi wa mpira.

Katika soka letu Tuna makocha waliowahi kucheza mpira lakini pia tunao wale ambao hawajawahi kucheza kabisa ama walicheza kwenye madaraja ya chini.

Karamu yangu inanishawishi hii Leo kuandika kuhusu Jinsi ambavyo walimu wetu wa Soka (makocha) wanakubali kuachwa na muda huku wakipigwa bao na makocha wa mataifa ya hapahapa Africa ya mashariki na kati katika kuzisaka Ajira Nje ya nchi zao kama Burudi, Uganda, Kongo nakadhalika.

Makocha wetu hawana uthubutu kwa kiasi kikubwaa, ni idadi ndogo sana ya makocha Raia wa Tanzania ambao walishawahi kwenda nje ya nchi kufundisha Soka. Tatizo ni uthubutu, kazi ya ukocha ni kazi ambayo Nafasi ikiwepo kwenye timu Fulani lazima upekeke CV zako kuomba kazi. Na hapa ndipo makocha wa Uganda, Burundi, Kenya, na mataifa mengine wanapotupiga bao. Naamini Tuna makocha wengi wenye CV nzuri za kufundisha Soka nje ya nchi, lakini hawana utayari kiasi kikubwa.

Pia mchezo wa Soka ni sayansi inayobadilika jinsi muda unavyokwenda, mbinu za miaka ya tisini ni tofauti na za sasa. Makocha wetu hawana kawaida ya kuhudhuria kozi mbalimbali zinazofanyika hapa kwetu na Nje ya nchi huko ili kuongeza maarifa zaidi kimbinu. Ukitaka kulijua hili Fwatilia CV za makocha kama Mwinyi Zahera, Ettiene Ndayiragije utang'amua ni kozi ngapi wamehudhuria kwenye maisha yao ya ualimu wa Mpira na wanakwambia wataendelea kusoma zaidi.

Inaumiza sana kuona makocha wengii wa hapahapa Afrika mashariki wamejazana kwenye ligi yetu wakati huohuo wakwetu wanang'ang'ania kubakia hapa kwetu miaka mingii, badala ya kwenda kutafuta changamoto mpya Nje ya nchi.

Ettiene Ndayiragije, Hitimana thiery, Haruna Hererimana, Noely Mwandila, Jackson Mayanja, Masoud Juma, Hao ni baadhi ya makocha kwa Siku za karibuni waliokuja kufundisha Hapa Tanzania wakitokea ukanda huuhuu wa Afrika mashariki na kati.
Kumbukumbu zangu zinanionyesha idadi ndogo ya makocha wetu waliojaribu kutoka Nje ya nchi,, Boniface Mkwasa "master", Dennis Kitambi na Sandey Kayuni.

Ni muda wakuamka sasa walimu wetu wa soka, Muda unatuacha mbalii, kwani hatuoni Faida wanazopata makocha wakigeni wakija hapa kwetu?? Timu ya Taifa ya Burundi imepata kipa kijana mwenye uwezo mkubwa sana Jonathan Nahimana kupitia kwa Ettiene Ndayiragije aliekuja Tanzania kufundisha na kumpa nafasi kubwa ya kucheza hali iliyopelekea kijana Huyo kuimalika na kuitwa Timu ya Taifa ya Burundi ilokwenda AFCON.

Hivyo hata sisi tunaweza tukanufaika na walimu wazawa kutoka nje ya nchi kwasababu wanaweza wakatengeneza njia kwa wachezaji wetu kucheza Soka la kulipwa na kupata wachezaji wakomavu zaidi kwenye timu yetu ya Taifa, kama ambavyo akina Ndayiragije wanafanya kuwapa nafasi wachezaji wa Mataifa yao (Emmanuel Mvuyekure, Jonathan Nahimana, Yusuph Ndikumana)

Selemani Matora,Malale Hamsini, Juma Mwambusi, Amri Said,Kessy Mziray,Adolf Richard,Hemed Morroco,Iddy Cheche, Juma Mgunda,Fred Felix minziro "Baba isaya" Amkeni Amkeni Amkeni,wakati unatuacha , tusikubali kupigwa bao kiurahisi na majirani zetu Hawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jambo moja hua tunafeli sana. Tumekua watumwa wa vyeti katika kila kitu na imeingia hadi kwenye soka. Tunadhani mtu yoyote mwenye leseni A au B ya ukocha basi atakua kocha mzuri. Ni kweli wenzetu wa Ulaya na America ya Kusini wana set standards za vyeti vya kufundisha mpira lakini pia wanaangalia kipaji na uwezo binafsi wa mwalimu. Ni kama hapa kwetu kwenye shule za kawaida za binafsi mwalimu anatakiwa kweli kua na vyeti vya taaluma yake lakini wanamfanyia assessment kama ni mwalimu kweli anaweza ku deliver

Huku kwetu mtu anaweza kua na hayo makaratasi ya kupitia course za ukocha, akajua aina ya mifumo ya soka lakini asijue namna ya kufundisha au kuusoma na kuuangalia mchezo. Mfuatilie kwa mfano Charles Boniface Mkwasa. Ni kweli enzi zake alicheza mpira kwa kiwango cha juu na pia anavyo vyeti vya kufundisha nadhani ni leseni B kama sikosei, lakini kwa maoni yangu Mkwasa hana kipaji cha kua hasa mwalimu wa soka mwenye kufundisha mbinu (tactics) za soka hasa la kisasa tena kwa timu kubwa kama Yanga au National Team ikiwa ni pamoja na kuweza kuusoma na kuuchambua mchezo wakati unaendelea au hata baada!!! Ni sawa tu na kina Juma Mgunda na makocha wengi wazawa. Watu wanaweza kupinga hoja hii lakini naomba wafuatilie kwa umakini tangia sasa watagundua ninachosema

Baadhi ya wachambuzi wa soka kama kina Dr Liki Abdallah, Jef Lea na wengineo kama wangewekeza nguvu na akili zao kwenye ukocha hakika wangekua makocha wazuri,kwa sababu wanaujua hasa mpira, kuufatilia, kuusoma mchezo, kung'amua formation za mpinzani zinavyobadilika, kujua nani anasaidia timu nani ka flop na nani asaidie kwa wakati gani, kujua historia ya mchezaji ndani na pengine hata nje ya uwanja. Na kua kocha mzuri sio lazima uwe umecheza soka kwa kiwango cha juu!

Kwahiyo mkuu ni kweli vyeti ni muhimu lakini soka ni mchezo wa field. Lazima mwalimu awe na jicho la ziada la ukocha kama wanalokua nao waalimu wote wazuri wanaosifika kwenye soka Ulimwenguni au hata hao kina Masoud Djumaa uliowataja. Kua architect au engineer mzuri wa kubuni na kutengeneza majengo ni zaidi ya vyeti kaka, ni kipaji pia.

Kwa kumalizia, umemtaja Jamal Malinzi kama aliwahi kucheza soka, waweza kutuambia japo timu moja aliyowahi kuchezea? Mimi sikumbuki mkuu
 
Back
Top Bottom