Kwanini Marais wa Tanzania huandika vitabu wakishastaafu na marais wa Marekani huandika wakiwa madarakani?

Kadosh

Senior Member
Joined
May 6, 2021
Posts
168
Reaction score
251
Kwanini Marais wa Tanzania [emoji1241] huandika vitabu mara tu baada ya kustaafu, tofauti na Maraisi wa Marekani ambao huandika Vitabu kabla ya kuukwaa Uraisi. Hii picha inakufundisha nini?
 
Refer The Audacity of Hope cha Obama, rhe art [emoji439] of the deal Cha Trump na vingine vingi
 
Kwani wastaafu wao wanasemaje!??? Wewe mwenyewe huwezi kuunda hata sentensi moja sanifu, unakosoa kucheleweshwa kitabu cha marais, as if utavoinunua!??? Jambo la msingi Bi Mkubwa aongezewe ulinzi maana alichojifunza kwa JPM anachojisifia sijui ni nini!??? Mbona haendi kukagua mradi wa umeme kule Rufiji!???
 
Kwa sababu wanaandika kile wasichoweza kukifanya waiwa madarakani. mfano Enzi zile CUF ilimsumbua sana mkapa mabamu ya machozi nje nje,halafu Mkapa angeanzaje kuandika kutamani mchakato wa katiba mpya na kuwapenda wapinzani
 
Na hizo Tawasifu zao zikitoka tu Basi hawachukui round.Mkapa baada ya kuandika Tawasifu yake hakumaliza mwaka na hii ya juzi juzi ni kuaga.Mwingine ingawa sio kiongozi ni mengi.Baada ya ile Tawasifu tu aikuchukua round.
 
Moja ya mambo wanayoandikaga ni pamoja na majutio/makosa yao kipindi cha uongozi, kiguse baadhi ya siri zilizokua na kiu ya mwaswali kwa wananchi(wasomaji), Kitu mbacho hawawezi andika wakiwa madarakani,

Ukionesha kujutia au kujua makosa yako na ukayaweka wazi basi uwe tayari kujirekebisha kitu ambacho kwao ni ngumu hasa ukiwa madarakani.

Na uzuri wa vitabu kama hivi kiwe na ups and downs.
Ukijiremba mwanzo mwisho as if bado unagombea Uraisi, hicho kitabu ukifa nacho kimekufa...

Kwa ufupi vingi naona vimejaa unaa tuu.
 
Wengi naona mmeruka ruka tu hapa , wazo Lanngu ni kwamba tuwe na knowledge purity , kigezo cha mtu kuandika kitabu na kikawa published ni level ya uelewa wa daraja lingine , naona katiba irekebishwe ili mtu awe raisi lazima awe amepublish vitabu viwili itasaidia kuwa na marais critical thinkers ,

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo ulikuwa unauliza kitu ambacho una solution yake? Acha unaa wewe
 
Wewe ndiye unarukaruka.
Hii hoja umeijenga baada ya kuona comments za wadau.

Kiini cha hii mada yako ilikuwa ni kudharau maraisi wetu ukiwalinganisha na wa Marekani.
 
Ukitaka Kufika mbali simama na kagua njia alizotumia aliye mbali, wamarekani bila kuwaonesha umewafanyia nini hawakupi uraisi , especially system lazima iangalie umetumiaje grey matter yako

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Kwani lazima tufanane kwa kila kitu USA ? Basi fananisha na Kenya au Zimbabwe kwani huko ni mbali sana
 
Kwanini Marais wa Tanzania [emoji1241] huandika vitabu mara tu baada ya kustaafu, tofauti na Maraisi wa Marekani ambao huandika Vitabu kabla ya kuukwaa Uraisi. Hii picha inakufundisha nini?
Marekani kuandika kitabu ni sehemu ya kampeni za urais, kama vile unaziweka sera zako kwenye kitabu ili watu wazisome wakujue kabla ya kukuchagua.

Barack Obama aliandika "The Audacity of Hope" kabla ya kugombea urais, watu wamjue vizuri akipata urais atafanya nini.

Tanzania rais anachaguliwa na chama si watu. Hakuna primaries (wanachama kupiga kura wanamtaka mwanachama gani awe mgombea wa chama chao)chama kinakata watu kwa sheria za kuungwaungwa. Mara mtu aliyezidi miaka fulani asiwe mgombea (ili kumkata Lowassa) mara sasa ninzamu ya mwanamke kuwa Spika (ili kumkata Sitta).

Magufuli aliulizwa atafanya nini akiwa rais akakataa kusema kitu, akasema ndiyo kwanza kachukua fomu hajazisoma bado. Yani mtu hatangazi sera zake, kila kitu kishaandaliwa kimo katika ilani ya chama yeye anaenda kuwa muhuri wa chama tu, hivyo hahitaji kuandika maisha yake kwenye kugombea urais.

Na hata hivyo vitabu wanavyoandika baada ya urais ni kama utani tu. Ukikisoma kitabu cha rais Mkapa ni kama katutania tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…