Kwanini Marekani inapandisha ushuru wa bidhaa kutoka Uchina

Kwanini Marekani inapandisha ushuru wa bidhaa kutoka Uchina

Kyodowe

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2013
Posts
1,236
Reaction score
1,368
Je ni sahihi Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa za Uchina? Na kama ni hivyo, kwa nini ilenge zaidi bidhaa za chuma?

Kwa takwimu zinavyoonesha, siyo siri tena kwamba nchi ya Uchina ndiye mzalishaji mkubwa wa bidhaa za chuma duniani kwa sasa. Uchina inazalisha zaidi ya nusu ya chuma kinachonunuliwa duniani kote kwa sasa. Na kati ya kampuni kumi kubwa duniani zinazozalisha chuma, kampuni tano ni za kutoka China. Si hiyo tu, kati ya kampuni 38 kubwa duniani, kampuni 21 ni za China.

Hali ikoje kwa Marekani?
Ni dhahiri kwamba soko la chuma Marekani kwa takribani mwongo mmoja limekuwa likihudumiwa kwa asilimia kubwa na bidhaa kutoka Uchina ikifuatiwa na Japani kwa mbali. Hali hii imeifanya maeneo yaliyokuwa maarufu kwa uzalishaji wa chuma Marekani kama vile Detroit kugeuka kuwa magofu. Zaidi ni kwamba ukilinganisha na Uchina, hakuna hata kampuni moja ya Marekani kwenye kumi bora ya wazalishaji wakubwa wa chuma duniani. Na kama hiyo haitoshi, ni kampuni mbili tu za kimarekani zilizopo kwenye orodha ya makampuni 38 makubwa ya kuzalisha chuma duniani, ukilinganisha na Uchina yenye makampuni 21 kwenye orodha hiyo.

Swali la kujiuliza ni:
1. Je, ni kweli Marekani hakulifahamu hili mapema?
2. Kwa nini Marekani achukue hatua sasa wakati mambo yamekwishaharibika?
4. Nini kimeikumba sekta ya chuma Marekani hadi kuporomoka kiasi hicho?
3. Je, kuongeza ushuru kwenye bidhaa za Uchina ndiyo suluhisho?
4. Je, ni kwa kiwango gani ukuaji wa uchumi wa China unategemea soko la chuma?
5. Nini kitatokea endapo China itashindwa katika vita hii ya kiuchumi?

Nawasilisha

List of steel producers - Wikipedia
 
Back
Top Bottom