Kwanini masikini wana chuki na matajiri?

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Kisaikolojia ikoje?
Unakuta mtu amepambana kivyake Sasa amejipata.
Kipindi anapambana kutafuta mtaji, connection na ramani, watu wanakuona tu.
Sasa ukianza kuinuka kupata japo kidogo uhakika wa watoto kwenda shule vita inainuka.
Utaitwa jambazi.
Utaitwa muuza madawa ya kulevya.
Utaitwa shoga.
Utaitwa freemason
Na uzushi mwingi ili mradi ionekane ridhiki yako haina uhalali wowote.

Alikuwapo mwanasiasa aliita wananchi wanyonge na alijisifu kuwafirisi wafanyabiashara kama Manji na kutumbua ili awafurahishe Watanganyika mbumbumbu na hakika walifurahi Kwa unafiki wao.

Utaanzisha kabiashara kadogo diwani na masikini wengine wavivu wakuletee watu wa TRA, sijui jiji, TMDA, fire n.k yani tu ushindwe biashara ufunge.
Na watakaa kijiweni wafurahi.

Tubadilike Watanganyika mbumbumbu na wanyonge
 
Hata ukijipata utashangaa marafiki zako uliosoma nao au wa kitaa wanaanza kujitenga na wewe

Wanakuwa wanajiona kabisa kwamba kwa sasa wao sio level zako wanajihisi inferior halafu wanakuwa wana chuki na wivu kiaina
 
Siku zote maskini anaamini tajiri ni ameiba haki/mali zake yan matajiri ni wezi! na tajiri naye anamhofia maskini kuwa atamroga ili awe maskini. Vita kati ya wenyenavyo na wasionavyo ni kali sana.
 
Hata ukijipata utashangaa marafiki zako uliosoma nao au wa kitaa wanaanza kujitenga na wewe

Wanakuwa wanajiona kabisa kwamba kwa sasa wao sio level zako wanajihisi inferior halafu wanakuwa wana chuki na wivu kiaina
Kuna wanasiasa walikuwa wakienda majimboni kwao huko vijijini, wanavaa mavazi ya gharama za chini. Mmojawapo alipoulizwa alisema wanataka wafanane na wananchi wa hali hiyo-ya chini! Wakivaa mavazi ya gharama kubwa, wataonekana tofauti.

Ukiwa katikati ya rafiki au ndugu wenye hali ya chini yaani maskini wa mali au hali; jitahidi kutokujionesha. Ama sivyo lazima wakuchukie! Vita kati ya tajiri na maskini ni kali sana huwezi amini!
 
Unajua ishu inakuja wapi? Utakuta mtu aliyejipata yuko simple na bado yuko peace na humble kwa wanae

Ni vile tu vitu vyake vya maendeleo alivyopiga hatua huwa havifichiki itajulikana na wataona tu kuwa amefanya hiki amenunua kile

Hapo ndipo tatizo la wivu na majungu linapoanzia
 
Wivu na chuki laZima vitaibuka
 
Back
Top Bottom