Kwanini matajiri hukupatia pesa kwenye bahasha ya khaki?

Kwanini matajiri hukupatia pesa kwenye bahasha ya khaki?

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Hili swali kuna mtu kaja kuniuliza nikashindwa kumjibu, what is it behind matajiri wanapokupatia pesa cash, kukuwekea kwenye bahasha ya khaki, anauliza kwanini wasikupatie tu mkononi.

Inaonesha alifanya kazi fulani akatakiwa kupewa cash, akapewa kwenye bahasha ya khaki, na yeye ni kama mtu asiyejiamini, alifikiri kuna namna za masharti ya kishirikina.

Kama kuna mtu alishakutana na hilo hebu atupatie uzoefu, na kama kuna tajiri hapa atufafanulie kama kuna ubaya wowote.
 
Hili swali kuna mtu kaja kuniuliza nikashindwa kumjibu, what is it behind matajiri wanapokupatia pesa cash, kukuwekea kwenye bahasha ya khaki, anauliza kwanini wasikupatie tu mkononi. Inaonyesha alifanya kazi fulani akatakiwa kupewa cash, akapewa kwenye bahasha ya khaki, na yeye ni kama mtu asiyejiamini, alifikiri kuna namna za masharti ya kishirikina. kama kuna mtu alishakutana na hilo hebu atupatie uzoefu, na kama kuna tajiri hapa atufafanulie kama kuna ubaya wowote.
Pesa hutolewa kwa njia nyingi
Kuingiziwa kwenye account ya bank
Kutumiwa kwenye simu
Kuwekewa kwenye hiyo bahasha ya khaki.. Hapa ndio pamekutatiza nadhani
Bahasha za khaki unazozungumzia ni zile ndogo sio zile kubwa za A4..hizo zinatumika kwa viwango vidogo tu vya pesa zisizozidi laki 5 na kuna nyeupe zake pia
Hapa hakuna ushirikina wowote bali ni urahisi wa kupatikana kwakwe na unafuu wa bei na matumizi yake ni hizi pesa ndogo ndogo kama nilivyoainisha hapo juu
Kingine ni heshima na usiri, si lazima hadhira ione umepewa bei gani lakini hata ikijua si heshima kumpa tu pesa ya zawadi bila kibebeo japo kwa baadhi ya matukio hufanya hivyo
 
Jamaa ana imani za kishirikina sana kuaminini mpaka vitu vidogo vidogo namna hiyo! Huyo anaamini kuwa bahasha ina ushirikina ambayo ni imani potofu iliyopindukia, atakuwa yupo karibu sana na ibilisi huyo! Ningekuwa mimi tajiri yake nikimgundua mtu mwenye imani za kishirikina na namna hii ni kumtimua tu maana hachelewi pia kukuendea kwa waganga!

1. Kwanza kuwekewa hela kwenye bahasha ni kwa ajili ya usalama wako wewe mwenyewe! Unaweza pewa hela cash hapo watu hawana dogo wakakuchapa visu wakaondoka na hiyo hela ambayo ni jasho lako! Kwa hiyo inakuwa ni usalama wako!

2. Mshahara ni siri kati yako na mwajiri! Siyo lazima kila mtu ajue kwamba unalipwa shilingi ngapi kutokana na kazi.uliyolipwa!

3. Bahasha za Khaki ndo zipo.available kwa wingi na urahisi kwenye maduka yote! Hata banks huwezi kuta bahasha tofauti na khaki!

Banks zenyewe ukiona mtu anachukua hela nyingi wanamuwekea kwenye bahasha za khaki nazo banks ni wanashirikina!?

Wewe hata ungewekewe hiyo hela kwenye bahasha nyeupe bado ungeuliza tu.

Nikiwa boss wako nakuwekea kwenye bahasha nyekundu au nyeusi kabisa kama zipo, maana washirikina wanaogopa sana hizo rangi! Nakufuata nyuma nyuma najua utazitupa tu kwa ujinga wako naziokota, weekend naenda kuzipiga kiroho safi!

Wito!

Vijana chapeni kazi hakuna ushirikina utakao kuingizia hela hata siku moja! Utajiri ni. matunda ya kufanya kazi kwa bidiii na matumizi mazuri ya hela.

Ushirilina ungekuwa kweli basi hata hao waganga leo hii wangekuwa matajiri wa kwanza na magotofa mjini.

Mwamini Mungu wako chapa kazi ndo msingi wa maendeleo, achana na imani potofu!
 
Pesa hutolewa kwa njia nyingi
Kuingiziwa kwenye account ya bank
Kutumiwa kwenye simu
Kuwekewa kwenye hiyo bahasha ya khaki.. Hapa ndio pamekutatiza nadhani
Bahasha za khaki unazozungumzia ni zile ndogo sio zile kubwa za A4..hizo zinatumika kwa viwango vidogo tu vya pesa zisizozidi laki 5 na kuna nyeupe zake pia
Hapa hakuna ushirikina wowote bali ni urahisi wa kupatikana kwakwe na unafuu wa bei na matumizi yake ni hizi pesa ndogo ndogo kama nilivyoainisha hapo juu
Kingine ni heshima na usiri, si lazima hadhira ione umepewa bei gani lakini hata ikijua si heshima kumpa tu pesa ya zawadi bila kibebeo japo kwa baadhi ya matukio hufanya hivyo
Umemaliza mshana.
Uzi ufungwe tafadhari.
 
Hata angewekewa kwenye nyeupe angeuliza tuu,. inaonekana kijana ana amini sana shirki..
ni kweli, si unajua zaidi ya asilimia 70% ya watanzania ni washirikina? na hata hiyo 30% sio kwamba hawajawahi kugusa ushirikina, aidha hawana hela kuuendeleza au wameamua kuacha kwasababu ya dini n.k. kama sio mchawi basi kachanjwa chale na mchawi/mganga, anda hirizi, anapiga simu kwa babu yake mchawi kijijini, anasafisha nyota, anakunywa madawa ya kienyeji aliyopewa na wachawi/waganga, n.k.
 
Ila akili za Watu wengine ni ndogo sana! Imagine mtu kama huyu kaajiriwa na unategemea awe creative kwenye kazi yake kweli,🤣🤣🤣
 
[B[Ulichokosea hujawahi kumueleimisha yule Marehemu wako kiasi akawa anagawa gawa miburungutu barabarani hovyo2 hovyo!
Pesa hutolewa kwa njia nyingi
Kuingiziwa kwenye account ya bank
Kutumiwa kwenye simu
Kuwekewa kwenye hiyo bahasha ya khaki.. Hapa ndio pamekutatiza nadhani
Bahasha za khaki unazozungumzia ni zile ndogo sio zile kubwa za A4..hizo zinatumika kwa viwango vidogo tu vya pesa zisizozidi laki 5 na kuna nyeupe zake pia
Hapa hakuna ushirikina wowote bali ni urahisi wa kupatikana kwakwe na unafuu wa bei na matumizi yake ni hizi pesa ndogo ndogo kama nilivyoainisha hapo juu
Kingine ni heshima na usiri, si lazima hadhira ione umepewa bei gani lakini hata ikijua si heshima kumpa tu pesa ya zawadi bila kibebeo japo kwa baadhi ya matukio hufanya hivyo

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
1620885086064.png
 
Huyo jamaa yako ni type ya wale wanazuzuka na hela, alitaka alipwe waziwazi hadharani wale manyang'au wapiga ngeta washuhudie ili wampige roba za mbao kiulaini wapite nazo zote kisha aende kwake kalowana ka kinda la njiwa.
 
Hata dukani bahasha za kaki zinapatikana kwa urahisi zaidi. Zinazalishwa zaidi.
 
Back
Top Bottom