Kwanini matajiri wa Yanga wamemsusia Manji hadi anateseka na kuaibika hivi?

unataka tufanye fujo tuzidi kumponza mwenyekiti wetu...wazidi kumkandamiza tunalijua hilo fika kwa uwezo wa bwan atatoka tuu na hakuna lisiokua na mwisho
 


Hata Yanga mnamtegemea tena asilimia zaidi ya 120.
Rejea mlivyogalagala kwenye vumbi baada ya kutishia kuachia uenyekiti
 
Hata Yanga mnamtegemea tena asilimia zaidi ya 120.
Rejea mlivyogalagala kwenye vumbi baada ya kutishia kuachia uenyekiti
by the way mi sio shabiki wa soka hasa la bongo, ila nashangaa sana unapotaka watu wapaze sauti pasipo na sababu, unataka watu wasifuate utaratibu na kutengeneza mazingira ya watu kuona Fulani anaonewa.
 
Kuchanganyikiwa si lazima uvue nguo hata huku ni kuchanganyikiwa
 
Nikiwa kama Mwanachama ' Mwandamizi ' kabisa wa Yanga ( hadi Malaika wa Mbinguni wanajua ) tena mwenye Kadi namba 0..3..9..1 niitwae GENTAMYCINE napenda kutoa masikitiko yangu makubwa kabisa kwa ' Matajiri ' wa Klabu yangu ninayoipenda ya Dar es Salaam Young Africa ( Yanga FC ) kwa kitendo chao cha kushindwa hata tu kwenda kumjulia hali Wodini Tajiri mwenzao, Kiongozi na Mwana Yanga mwenzao Mheshimiwa Yusuph Mehboob Manji hasa katika Kipindi hiki Kigumu anachokipitia.

Na hi inaonyesha dhahiri kuwa pengine hata Watu waliohusika ' kumchongea ' Manji ni hawa hawa Matajiri wenzie ili tu Manji ' afungwe ' na wao waichukuwe Yanga FC yetu na wafanye yao. Hivi inawezekana vipi Mchungaji Gwajima kaweza kumtembelea Manji wodini Muhimbili halafu nyie mnaojifanya ' Matajiri ' wa Yanga FC mshindwe? Kwanini mnakuwa na roho mbaya hivi?

Mimi mwenyewe pamoja na ' Umasikini ' wangu ila jana niliweza tu kumchungulia Mwenyekiti wangu Manji wakati anapewa dawa na Manesi na nikampungia mkono na kumtakia kila la kheri na yeye akanijibu kuwa nisijali kwani leo atatoka Hospitalini na atakuja Klabuni Kwetu Kesho ili kupanga mikakati ya Kuiua Ngaya FC ya Comoro na kujipanga na mechi ya Simba SC tarehe 25, February 2017.

Wana Yanga FC wenzangu nadhani huu sasa ni wakati ' muafaka ' kabisa wa kuwakataa hawa ' Matajiri ' wengine wa Yanga FC na kama Mwenyekiti wetu Manji atatoka ' Kolokoroni ' leo basi tumwambie tu ' awafukuze ' wote na Timu abaki nayo Yeye hadi atakapochoka kwani tuna Imani kubwa na Yusuph Mehboob Manji na tunampenda hasa ( hasa Mimi GENTAMYCINE ) na namwombea kwa Mungu atoke na awe huru.

Hakuna kama Yanga FC, Yanga ni mbele kwa mbele na Manji ' tufukuzie ' hao ' Matajiri ' waliokusaliti ukiwa na matatizo haya kwani sisi kama wana Yanga FC hatuwataki tena.
 
Tunakuhitaji mwenyekiti wetu uwe huru.Mi mwenyewe sifurahii hata kidogo we kua mahabusu.
 

Una hakika wao ndiyo wametoa amri akamatwe?
 
Kwanini usngeenda kumpa mkono wa pole hapo wodini , badala yake umempungia kwa mbali na kumuonyesha alama ya dole gumba , moyoni ukijisemea mambo itakuwa yee danga chee!!!
 
Naona kama mtoa Mada nae kandia kwa mbaliiii anaonekana maneno na vitendo tofauti kabisaaaaa
 
Watanzania tuna shida..... Hatujui nini tunataka na nini kifanyike kwa ajili ya taifa letu. Mtu kapelekwa Mahakamani kujibu tuhuma za kutumia madawa ya kulevya..... Matajiri wa Yanga wafanyeje sasa?!! This is very funny!!!
 
Kufuatia kitendo cha Diwani wa Mbagala-CCM,kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kutumia dawa za kulevya,CCM inatakiwa iachane kabisa na Manji.

Manji amekiaibisha Chama ambacho Mwenyekiti wetu Magufuli amejinasibu kupambana na wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya.

Ni aibu kwa ccm hata kwa wapinzani wa CCM.Tunaonekana ni chama cha wala unga,na hiyo sio sera wala desturi ya CCM.

Manji amekiuka miiko ya uongozi ya CCM,na akiachwa atazidi kukichafua chama na kuifanya vita hii ionekane si lolote na ni ya kupambana na dagaa.

Kama kweli Magufuli yupo makini na vita hii na kweli amedhamiria kusafisha chama chetu,basi fukuzilia mbali Manji na wana CCM wengine wowote watakaoonekana kukichafua chama kwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Mtumiaji na dawa na mnunuzi lao moja,na ili iwe funzo kwa wengine tuanze na Manji ili watu wajue kuwa CCM sio chama salama kwa wadau wa madawa ya kulevya.
 
Utafukuza wafadhili wote wa chama (kupitia drugs, ukwepaji kodi, na biashara za magumashi).


KADA
 

Ubavu mnao??Chama Cha Majangili
 
Ukimpiga teke chura unamuongezea hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…