Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
Wengi washakamatwa kwa kosa la kumtukana rais, na kila anapo kamatwa mtu kwa kosa la kumtukana rais mtu huyo hutangazwa na huishia kupelekwa mahakamani.
Pamoja na hatua zote hizi za kisheria wanazo chukuliwa watu hawa lakini kila uchao ukipita katika mitandao unakutana matusi dhidi Mh rais, au dhidi ya kiongozi yeyote wa serikali.
Unadhani hii inasababishwa na nini?
A. Watu wameichoka sana CCM na serikali kiasi wasiogope lolote? Lakini kama wameichoka kwanini rais Magufuli alishinda?
B. Vitendo vya kumtukana rais ni kosa kama makosa mengine kama vile ya wizi. Kila siku wezi wanafungwa na wengine kuchomwa moto, lakini watu bado wanaendelea kuiba.
C. Vijana wanachochewa na wanasiasa wa upinzani, na wanajua wakikamatwa makada wa vyama hivyo watafanya harambee ya michango, michango ambayo pia kwa namna moja humnufaisha mchangiwa. Ina maana hii ishakuwa fursa aka DILI?
D. Vijana kupenda sifa na kujijenga kisiasa, na ikichangiwa na ile kasumba kuwa ili uwe mpinzani wa kweli dhidi ya serikali ni lazima ufungwe au upate msukosuko kama Mandera au Mwalimu Nyerere. Je, wanamtukana rais na viongozi wenzake kwasababu ya kutafuta "kiki"??
E. Jamii imemomonyoka kimaadili na ndio maana kumekithiri matusi kwenye mitandao, si kwa rais wetu tu, hata hao wanaotukana pia ukifuatilia huwa wanatukanana wenyewe kwa wenyewe.
F. Hotuba za viongozi wa serikali hasa za Mh Rais kujaa vijembe kwa viongozi wa upinzani na wafuasi wao, vijembe ambavyo mara zote na siku zote huibua mijadala kwenye mitandao ya jamii, na katika mijadala hiyo wafuasi wa watu waliopigwa vijembe hutumia kurejesha vijembe hivyo Mh Rais. Kwasababu hiyo, wadhani Mh Rais akiacha vijembe kutapunguza matusi dhidi yake ukilinganisha na hatua hii ya kamatakamata?
Njano5
0622845394