Jamani, mbona tunatia aibu hivi. Ukipitia page ya Aston Villa kuhusu mchezo wao na Man City jana (hasa pale walipoiweka picha ya Samatta), matusi ya vijana wa Bongo yameendelea kurindima. Hii ni tofauti kabisa na maoni ya wengine walioyatoa kwa lugha ya Kiingereza. Karibu maoni yote ya Kiingereza yameipongeza timu na kuipa moyo kuwa wamecheza vizuri sana pamoja na kupoteza mchezo.
Sasa ukija kwa maoni yaliyotolewa na waswahili, ni matusi matupu. Wengine wanatukana ati kwa nini Samatta alipumzishwa dakika ya 80 na kwa maoni yao angeendelea mpaka mwisho. Sioni tatizo kwa kutoa maoni yao lakini matusi yanayotumika sasa yanatia aibu hadi basi. Vijana jueni kuwa hii ndio picha itakayojengeka dhidi ya Watanzania kuwa si wastaarabu na lugha ya Kiswahili itaonekana kama ya kihuni vile.
Niwaulize tu watu wenye tabia kama hiyo; Je ninyi mnaufahamu mpira saaaaana kuliko wachezaji na walimu wao? Mmmelazimishwa kutazama hiyo mechi? Mmelazimishwa kuwa mashabiki? Usipokuwa shabiki wa Aston Villa na Samatta undhani unaipunguzia nini timu na Samatta mwenyewe? Kama yote hayo hakuna, sasa nini kinapelekea kwenda kuchafua taswira ya Taifa kwenya page maarufu kama ya Aston Villa? Walau mngekuwa mnatoa maoni yenu kwa Kiingereza isingekuwa rahisi kujua ni watu wa kutoka nchi gani.