Kwanini matusi ya Wabongo yanashamiri kwenye Twitter ya Aston Villa?

Kwanini matusi ya Wabongo yanashamiri kwenye Twitter ya Aston Villa?

Maelau

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
1,366
Reaction score
1,342
Jamani, mbona tunatia aibu hivi. Ukipitia page ya Aston Villa kuhusu mchezo wao na Man City jana (hasa pale walipoiweka picha ya Samatta), matusi ya vijana wa Bongo yameendelea kurindima. Hii ni tofauti kabisa na maoni ya wengine walioyatoa kwa lugha ya Kiingereza. Karibu maoni yote ya Kiingereza yameipongeza timu na kuipa moyo kuwa wamecheza vizuri sana pamoja na kupoteza mchezo.

Sasa ukija kwa maoni yaliyotolewa na waswahili, ni matusi matupu. Wengine wanatukana ati kwa nini Samatta alipumzishwa dakika ya 80 na kwa maoni yao angeendelea mpaka mwisho. Sioni tatizo kwa kutoa maoni yao lakini matusi yanayotumika sasa yanatia aibu hadi basi. Vijana jueni kuwa hii ndio picha itakayojengeka dhidi ya Watanzania kuwa si wastaarabu na lugha ya Kiswahili itaonekana kama ya kihuni vile.

Niwaulize tu watu wenye tabia kama hiyo; Je ninyi mnaufahamu mpira saaaaana kuliko wachezaji na walimu wao? Mmmelazimishwa kutazama hiyo mechi? Mmelazimishwa kuwa mashabiki? Usipokuwa shabiki wa Aston Villa na Samatta undhani unaipunguzia nini timu na Samatta mwenyewe? Kama yote hayo hakuna, sasa nini kinapelekea kwenda kuchafua taswira ya Taifa kwenya page maarufu kama ya Aston Villa? Walau mngekuwa mnatoa maoni yenu kwa Kiingereza isingekuwa rahisi kujua ni watu wa kutoka nchi gani.
 
Wazungu wanajua evolution ya mtu mweusi bado inaendelea usijali kabisa we are still on progress
 
Mfano mzuri wa Watz angalia washabiki wa Simba na Yanga, watu hawajielewi hata mipaka ya ushabiki hawaijui. Wanataka hadi kikosi wampangie kocha, utasikia huyu kocha hajui mechi ya watani wa jadi anamuachaje fulani? Yaani hata kama perfomance yake ni mbovu, ana injury ama ameshindwa kucope na mfumo wa kocha wao wanataka apangwe tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni malezi, Mtoto umleavyo ndio akuavyo.

Kijana aliyelelewa kwenye malezi yenye misingi ya maadili mema hawezi kutukana hovyo bali atatoa maoni yake kwa kutumia lugha ya staha.
 
Mfano mzuri wa Watz angalia washabiki wa Simba na Yanga, watu hawajielewi hata mipaka ya ushabiki hawaijui. Wanataka hadi kikosi wampangie kocha, utasikia huyu kocha hajui mechi ya watani wa jadi anamuachaje fulani? Yaani hata kama perfomance yake ni mbovu, ana injury ama ameshindwa kucope na mfumo wa kocha wao wanataka apangwe tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Toa sababu nyingine aisee kwa mashabiki wa Simba na Yanga kutojielewa lakini hii ya mashabiki kuongelea vikosi vya mechi ni dunia nzima na sio kwamba ni kutojielewa na muda mwingine wanakuwa sahihi.

Ukienda page ya Man U utaona mashabiki wanatoa maoni kuwa leo angeanza Ighalo badala ya fulani vivyo hivyo kwa mashabiki wa Chelsea, Arsenal n.k wanatoa maoni kuhusu lineup timu isipopata matokeo mazuri.
 
Ni sawa kama umesoma vizuri hapo juu utaona nimezungumzia mazingira ambayo yanaambatana na team selection mfano fitness report ya madaktari, perfomance ya mchezaji husika mazoezini, mfumo ambao kocha ame opt kuutumia katika game husika.

Hivi vitu wabongo wengi hatuna uelewa navyo, mfano unaposema team itacheza 4-4-2/3-5-2/4-3-2-1/4-2-3-1/4-3-3 nk nk bado hatujui ni mchezaji gani yuko effective zaid kwny mfumo upi atleast wenzetu wana uelewa wa nini wanacho pendekeza.

Huku kwetu mchezaji anafanya human error, utaskia huyu jamaa huwa ni shabiki wa Yanga ama amepewa hela achome. Mara ooh sisi ndio tunaoumia wachezaji mechi ikiisha hawana hata uchungu wanakumbatiana, sasa unajiuliza huyu alitaka mechi ikiisha ianze boxing ama?

Sikatai washabiki wana nafasi yao na wana nguvu sn kiasi cha kusikilizwa na team/wamiliki wa team,ila tuwe na mipaka na discipline. Huwezi fanyia kazi maoni tofauti ya watu zaidi ya elfu kumi kujenga team moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Villa watafute moderators wa kufuta upuuzi wa watu na ku-block vichaa
 
Villa watafute moderators wa kufuta upuuzi wa watu na ku-block vichaa
Hapo umenena vema. Napendekeza wangetafuta moderator wa comments za Kiswahili kwa kuwa ndizo huambatana na matusi kwa kiasi kikubwa.
 
Kwa sababu wanatukana kwa kiswahili hamna shida. Tunaosoma ndio hao hao watanzania.
 
Back
Top Bottom