Kwanini mazishi ya Kiserikali ya Shinzo Abe yana utata?

Kwanini mazishi ya Kiserikali ya Shinzo Abe yana utata?

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1664164927740.png

Wiki moja iliyopita, viongozi wakubwa wa kimataifa walikusanyika London kwa ajili ya mazishi ya kiserikali ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza. Sasa wengi wao wanaelekea upande wa pili wa dunia kwa mazishi mengine ya kiserikali ya Waziri Mkuu wa zamani wa Japan aliyeuawa, Shinzo Abe.

Lakini Wajapani, inaonekana, hawajafurahishwa nayo - si haba kwa sababu inakadiriwa kuwa mazishi yake yatagharimu $11.4m (zaidi ya Tsh. bilioni 23).

Katika wiki chache zilizopita upinzani dhidi ya mazishi ya kiserikali umekuwa ukiongezeka. Kura za maoni zinaonesha zaidi ya nusu ya idadi ya watu nchini humo sasa wanapinga serikali kugharamia mazishi.

Mapema wiki hii, mwanamume mmoja alijichoma moto karibu na ofisi ya Waziri Mkuu mjini Tokyo. Na siku ya Jumatatu karibu waandamanaji 10,000 waliandamana katika mitaa ya mji mkuu wakitaka mazishi yasitishwe.

Lakini kwa upande mwingine, tukio hilo linawavuta washirika wa Japan kutoka kote ulimwenguni. Rais wa Marekani Joe Biden hatahudhuria, lakini atawakilishwa na Makamu wake Kamala Harris. Waziri Mkuu wa Singapore Lee Hsien Loong atakuwepo.
1664165307754.png

Vivyo hivyo Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese, pamoja na watangulizi wake watatu. Waziri Mkuu wa India Narendra Modi alikwepo mazishi ya Malkia lakini anasafiri kwa ndege kuelekea Tokyo kutoa heshima zake kwa Abe.

Je, hali hiyo inatafsiri nini kuhusu Abe, kwamba hata viongozi wa dunia wanapokusanyika kwa ajili ya mazishi yake wengi katika nchi yake wanaipinga?

Kwanza, hii sio tukio la kawaida. Huko Japani, mazishi ya kiserikali yametengwa kwa washiriki wa Familia ya Kifalme. Mara moja tu, tangu Vita vya Pili vya Dunia, mwanasiasa amepewa heshima hii, na hiyo ilikuwa mnamo 1967. Kwa hivyo, ukweli kwamba Abe anapewa mazishi ya kiserikali ni jambo kubwa.
1664165317266.png

Kwa sehemu ni kwasababu ya jinsi alivyofariki, alipigwa risasi kwenye mkutano wa uchaguzi mwezi Julai. Na Japan iliomboleza kwa ajili yake. Hakuwahi kuwa maarufu sana, kulingana na kura za maoni, lakini wachache wangekataa kwamba aliiletea nchi utulivu na usalama.

Kwa hiyo uamuzi wa kumfanyia mazishi ya kiserikali pia ni kielelezo cha hadhi yake. Hakuna aliyehudumu kwa muda mrefu katika ofisi ya Maziri Mkuu kama Abe, na bila shaka, hakuna mwanasiasa mwingine wa baada ya vita aliyekuwa na athari kama hiyo kwa nafasi ya Japan duniani.
 
Ni vile na sisi hatukuambiwa yale mazishi ya CHAT.. yaligharimu kiasi gani laiti tungewekwa wazi basi ingekuwa utata
 
Kama kuna watu wanakufa na njaa halafu mtu mmoja aliyekufa anaghalamiwa sh. Billion 23
Kwakweli hizo pesa ni nyingi sana.
 
Back
Top Bottom