Kwanini Mazoezi hayanisaidii?

454

Senior Member
Joined
Apr 23, 2017
Posts
136
Reaction score
193
Habari wakuu wa humu JF,Mimi ni mnene sana Nina 105 kg nimepima Juzi.

Najitahidi sana kufanya Mazoezi lakini sipungui,Kwa kweli nauchukia unene kuliko kitu chochote na mbaya zaidi Nina kisukari nashangaa wagonjwa wenzangu wakipungua na wako na mwili mzuri.

Je Kwanini Mimi Mazoezi hayanisaidii?
 
Either unayafanya ndivyo sivyo kwa maana Huna elimu ya kufanya mazoezi ipasavyo na , hauko consistent . Punguza kula pia ila kuwa makini maana una kisukari.

Kama huwezi mazoezi, nenda kafanye bypass surgery India itakusaidia.
 
Mkuu kuna Dr ntakuunganisha nae nakupa guarantee utapungua kilo zitafika hadi 70 km utafata nasharti yake has a kwny chakula
 
Acha kula vyakula vya mafuta, kula chupuchupu,then punguza kipimo cha kula
 
Kwa kifupi ni kwamba hufanyi mazoezi yoyote wewe!!.....Mazoezi ya kupunguza mwili siyo kitu kirahisi kama kula pilau la xmas!!......Wewe unaenda kucheza cheza then unasema kuwa unafanya mazoezi???[emoji32][emoji32][emoji32]
HAhahhahaha mkuu umenichekesha sana eti anaenda kucheza cheza

Kuna jamaa mmoja nae eti anataka kupunguza mwili anachofanya anazunguka uwanja wa mpira raundi moja zen anachekacheka tayari anaona kamaliza
 
HAhahhahaha mkuu umenichekesha sana eti anaenda kucheza cheza

Kuna jamaa mmoja nae eti anataka kupunguza mwili anachofanya anazunguka uwanja wa mpira raundi moja zen anachekacheka tayari anaona kamaliza
Mkuu hakuna kitu kigumu kama kufanya mazoezi ya kupunguza mwili!!......Asilimia 99 huwa wanakata tamaa then wanaanza kudai kuwa wanafanya mazoezi na hawapungui kumbe walishakata tamaa siku nyingi sana!!
 
Kamwe mazoezi hayatakusaidia kama diet yako ni mbovu na hauhitaji mazoezi kupunguza uzito kama ukiweka diet yako vizuri.

Kwa kkfupi njia rahisi ya kupjnguza uzito ni kuondoa vyakula vyene sukari na wanga kwa ujumla kwenye diet kama ukiondoa wanga kabisa <10 grams a day unaweza kula protein na mafuta bila limit.
Wanga ni soda,bia,vizi,wali,unga,asali etc.
 
Ngoja ntaweka youtube video za maelezo zaidi ila kwa kifupi hii idea ya iliyoenea duniani kuwa mafuta ndo adui wa afya ni uongo ulioenezwa kwa makusidi na mashirika ya vyakula marekani miaka ya nyuma, walifanya hivyo kwa kuwahonga wanasayansi kutoa research za uongo na kuminya research nyingine.
 
Kuna mtu amepungua kutoka kilo 85 mpaka 66.Alianza project rasmi mwezi wa nne mwishoni.
Mazoezi + Nidhamu ya chakula.Ila inahitaji moyo
 
Unafanya mazoezi ya aina gani na kwa kiwango gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…