Kwanini Mbowe anatetea sana maridhiano wakati alisema tumedanganywa?

Kwanini Mbowe anatetea sana maridhiano wakati alisema tumedanganywa?

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
20,189
Reaction score
29,663
Katika hotuba yake ya Jana, Mwenyekiti wa CHADEMA alitumia muda kutetea maridhiano na kuonesha ya kwamba Kuna mafanikio tumepata baada ya kufanya maridhiano.

Kwa mfano anadai tumeweza kujenga jengo la makao makuu baada ya kupokea Ruzuku, pia amedai kuwa tumeruhysiwa kufanya siasa na kufutiwa kesi zaidi ya mia nne.

Shida yangu sio hayo mafanikio ya Maridhiano Bali ni unduminakuwili wa Mwenyekiti baada ya juzi yeye mwenyewe kudai ya kwamba CCM waliwaingiza mjini ila Leo anadai mafanikio yalikuwa makubwa.

Nimeshangaa Sana. Hakuna katiba Mpya, sheria za uchaguzi za hovyo na chama kimepata Asilimia 0.78 kwenye serikali za mitaa kutokana na uharamia wa CCM na serikali yake. Inakuaje Mbowe yeye anaangalia Ruzuku na mikutano? Chama kimepoteza wanachama wake katika Hali ya kutatanisha na wengine wamekufa wakati wa huo uchaguzi, yeye Mbowe mafanikio yake ni Ruzuku tu?

Ni kwanini Mbowe anashangilia Vitu ambavyo vilikuwepo kabla na kuviaacha ambavyo ni vya msingi?
 
Anajua alipewa nini kusaliti wazalendo...
Pesa mkuu, kwenye pesa Mimi mwenyewe nasema sikujui...Tena nakukana Mara 3 kama Petro
Haaaa bora hata unesema ukweli wako kutoka moyoni mm simakani mama mzazi tu aliebakia mbele napita nae mbele ya pesa
 
Lile zee limekaa kifisad Sana🤣🤣🤣🤣

Huyu angekuwa ccm mafisadi kina rostam,gsm,kinana ingekuwa Cha mtoto kwake🤣🤣🤣
 
2. Chadema itatoa Waziri mkuu wa JMT
Chadema bado hawajajitambua. Wana tamaa ya pesa kuliko kazi . Chadema hawafai kuongoza serikali watatapanya kodi zetu hovyo . Bora ccm waendelee kuongoza serikali milele katika vyeo vyote vya kisiasa.
 
Back
Top Bottom