Kwanini mbunge Musukuma anapenda kuwadharau wasomi wetu?

Kwanini mbunge Musukuma anapenda kuwadharau wasomi wetu?

Hapo Hakuna kumtafuta mchawi,
Mchawi wa wasomi Ni wasomi wao wenyewe.

Tatizo linaanzia,
Wasomi wenyewe wanapokiuka miiko ya taaluma zao na kufuata matakwa ya matumbo yao kwa maslahi ya kisiasa.

MWISHO wa sikU,
Tija ya taaluma yao Inakua Ni sawa na sifuri, maana na wao wanaburuzwa mputa mputa Kama sisi tusiosoma.
 
Nimesikiliza kwa makini wakati mbunge Musukuma akichangia leo bungeni, moja alikua akichangia kuhusu bajeti na kuwaita wataalamu wetu wa uchumi kua wataaalamu uchwara, hasa akitetea kuhusu wamachinga na kuondolewa barabarani hasa Kariakoo.

Hali iliopelekea Naibu Spika kumtaka aondoe neno hilo. Hivi kwanini mheshimiwa mbunge Musukuma kila akichangia anakua akiwasigina wasomi na kuwatukuza darasa la saba?

Hii inatokana na kutojiamini kwa kukosa elimu au kuna nini kafanyiwa na wasomi hadi chuki yake kufikia kiwango cha juu?

Au ndio kutaka kuwawini wananchi wengi ambao hawana elimu?
Hiyo ni sumu ya inferiority complexity. Anapambana na fikra kuwa yeye haujiendeleza kielimu so anajaribu kushawishi hadhira yake kuwa yeye na kuishia la 7 ni bora zaidi kuliko hao walioendelea na shule .

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Msomi mzuri tungeanza na ndugai mwenyewe.

Ukiitafakari Tija ya elimu aliyonayo unaona kabisa hapa, TULIPIGWA.

KABLA YA MWENDAZAKE,
Alishupalia Sana bandar ya bagamoyo ijengwe.

Wakati wa MWENDAZAKE,
Akaungana na MWENDAZAKE kuipondea bandari ya bagamoyo kua Ni ya kihuni.

Baada ya mwenzake,
Akageuka kua MWENDAZAKE alipotoshwa, bandar ya bagamoyo Ina Tija kiuchumi.

Msomi mwingine Ni ndugu yetu uyu PASKALI,
Uyu nikimtafakari ndo nachoka kabisa, naishia TU kumhurumia.
 
Kusoma ni kitu kimoja na kuwa na akili ni kingine.
Wakati mwingine Msukuma ana hoja zenye akili kuliko wasomi anaowabeza.
 
Msukuma ni mganga wa kienyeji , alishawahi kuwa mwenyekiti wa waganga Tz Sasa anawajua vizuri Sana ,wabunge ,mawaziri ,wanavyotegemea ndumba kusavaivu kwenye siasa , alishawahi kuwauliza bungeni nani kaingia humu bila kupitia kwa Mganga wote wakakaa kimya , siri ndio hiyo .wasomi hawafanyi kitu wenyewe bika kutegemea waganga . Ila usomi mwingine kama wa Kabudi sijui una faida gani?
 
Msukuma yupo sahihi 100%

Wasomi wa Tz asilimia kubwa wanafiki

1. Corona, waliikana, na hawaeleweki wanasimamia wapi hadi sasa.

2. Uchumi, walipongeza unakuwa kwa kasi, kinyume chake, no one challenging

3. Elimu wanasema bure, wapi Elimu bure..... nobody challenging

4. Afya... hakieleweki......

5. Madini na makinikia, umbea mtupu

6. Katiba YETU ya hovyo sana no lawyer to complain except Lisu na wanaharakati

7. Tume ya uchaguzi ya hovyo... kimyaaa
A) uchafu wa uchaguzi serikali mitaa
B) uchafu wa uchaguzi serikali kuu

8. Kilimo ...... utopolo

9. Viwanda na biashara, kaijage aliwahi sema cherehani 4 kiwanda wakapiga makofi bungeni , hivi definition ya kiwanda inakuja low to 4 sewing machines?

10. Kitambulisho cha machinga, tukadanganywa mtu anaweza chukua mkopo benki.... wakapiga makofi , hakina au
A) bila jina
B) bila maelezo unapoishi
C) bila signature

Nknk

Huo usomi unaanzia wapi?

Bungeni Jobu anajiamlia tu wewe toka yule Ingia, hawa hapana.....na hakuna wakumchallange bora liende

Msukuma mbunge yupo sahihi 100%
 
Joseph Kusheku a.k.a Msukuma ni mbunge na mfanyabiashara mkubwa.
Utajiri wake ni wa kupata tu kwenye dhahabu.

Haihitajiki elimu au kutokuwa na elimu kuokota dhahabu, yeyote angeweza kupata bahati hiyo.
 
Nchi hii tuna list ya wasomi mizigo kabisa,
Na bahati mbaya zaidi tulokua nayo wao ndio wameshikilia mpini wetu

Nawataja[emoji116]
1. Yule sabufa pale kiti Cha mbele kabisa.
2. Yule kalamaganda alietuletea urojo wa comoro
3. Yule Mama wa afya na msaidizi wake
4. Yule ya daktari kigamboni wa vifurushi nafuu
5. Yule katibu mkuu, kiongozi wa viti maalum
6. Yule Bwashee wa kilimo
7. Yule Dada Suu aliekuaga maliasili
8. Yule mchora mawe wa singida
9. Yule Mzungu kichaa wa ada ya uzalendo
10. Yule mzee wa UTANAMBIA NINI nina Degree Nne
11. Yule kesi wa kule KUSINI
12. Yule mfufua watu
13. Yule mzee wa injinia Soma iyo
14. Yule mzee wa vunjo paloli
15. Yule mama wa Nguvu za kiume bungeni
16. Wale madaktari Wote wa Muhimbili waliochonga dubwasha la kujifukiza
17. ...........
 
Kabisa!. Fikiria msomi kama Lisu anaamisha watu kwamba yeye akichaguliwa kuwa rais ndio tatizo la ajira litaisha wakati bibi yako kapambana bila hata Lisu kuwa mwenyekiti wake wa kitongoji na amewasomesha!
Fikiria "msomi wa Ph.D" kama mwendazake eti ndio kiongozi mkuu wa nchi!!
Msomi ambaye hujui dunia inaendaje wawezaje kujiita msomi!? Msomi asiyejua hata siku ina masaa 24 kweli anajiita msomi!!??
 
Kwa sababu anaamini ana pesa, ila ni mjinga tu kama wajinga wengine
Bora mjinga ambae hajaenda shule,
Kuliko mjinga ambae ameenda shule.

Unabaki unatafakari,
Hivi uyu jamaa alienda kusomea ujinga uko vyuoni, SI Bora TU angebaki mtaani na sisi tukauza Wote chips.
 
Wasomi wenyewe wanajidharau. We fikiria Prof anaita chuo kikuuu Jalalani. Mwenye Elimu ya hapo si kama nzi amechua takataka na sio Elimu

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
 
Utajiri wake ni wa kupata tu kwenye dhahabu.

Haihitajiki elimu au kutokuwa na elimu kuokota dhahabu, yeyote angeweza kupata bahati hiyo.
Kwani kila siku anaokota dhahabu?

Mtazamo finyu sana huu! Alichimba dhahabu pengine akapata mara moja au mbili lkn akaweza kuendeleza huo mtaji alioupata kupitia dhahabu huo pia ni uwezo si jambo la kubeza.

Au tuseme Kama kuokota dhahabu ni rahisi hivyo kwann hao wenye vyeti wanaojiita wasomi hawaendi kuokota?
 
Back
Top Bottom