Kwanini Mbuni, Tausi na Kasuku hatufugi Kwa wingi hapa Tanzania?

Kwanini Mbuni, Tausi na Kasuku hatufugi Kwa wingi hapa Tanzania?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Mimi ni mdau wa kilimo na Ufugaji na ninapenda kutoka moyoni kabisa.

Katika Hali inayonipa maswali mengi ni hili swala ufugaji wa Ndege kama Tausi Mbuni na Kasuku.

Huwa napenda kujifunza bila ukomo hasa kupitia mitandao ya kijamii. Ukiingia mjini YouTube uka search Ufugaji wa Tausi Tanzania
Utakacho kutana nacho utaogopa na kutetemeka. Aisee binafisi Mimi Huwa naletewa Njiwa Tausi!

Tena wafugaji wa njiwa Hawa ni wengi sana Kwa maana hiyo Tanzania wafugaji wa Tausi hawapo kabisa hata mmoja?

Kichekesho ni kwamba uki search hivyohivyo Kwa lugha ya kiingereza utakutana na wakenya wengi sana wanafunga hao Tausi mbuni na Kasuku na wapo openly sana.


View: https://youtu.be/c2e7M-9wL6w?si=LM6kz3T0LWFYI8DW

Najiuliza Ina maana Tanzania ni kosa kisheria kufuga Hawa ndege? Kama ndiyo vipi kuhusu kanga mbona wao wanafugwa Hadi wale maporini?

Basi kama Kuna taratibu za kufuata Ili kufuga ndege Hawa naomba wajuvi wa hili watupe mwongozo wa kufuata.

Binafisi sidhani kama ni dhambi watu wakiji fugia tu kiholela Ili mradi tu anauwezo wa KUFANYA hivyo. MFANO kama kasuku hata upatikanaji wake sio rahisi na hata Tausi Hali kadharika vilevile.

Kwa maana hiyo hata kama wakiruhusu Bado wafugaji watakuwa wachache vile vile. Ni Nini hofu ya serikali kwamba watu wakifuga Tausi Hadi wawe na vibali na mlolongo kibao wa vitu vya kufuata Ili Hali Tausi Hana madhara yoyote Kwa binadamu.

Wala siyo kusema labda Tausi anapatikana Tz pekee yake hapana.

Nilitamani sana watu tuuziwe hata wannyama rafiki kama swala,digidigi,pofu na wote wa jamii hiyo.

Issue iwe ni kulipia kibali Cha kununua tu ukipenda ukachinje niwewe. Maana Kwa kifupi sisi tunazuiana lakini wazungu ambao tunategemea waje watalii kwetu ndo wanawabeba na kwenda kufuga kwao hii Nini Sasa tunafanyiana?

Mnadhani baada ya miaka michache ijayo mzungu atatoka Canada kuja kumuona nyati anayemfugaja kwakwe ama jirani yake?

Niliwahi ona jamaa alikuwa anafuga tumbiri(Gendere) wakaguzi mara kazaa walikuwa wanakuja kuangalia mahala pale. Wakati huko maporini ngedere wanategwa na kuuliwa Kwa Sumu daily mfano mzuri tu kijijini kwetu.

Gendere wanao kufa ni wengi mno Kwa kuwindwa na mbwa wakali na kuuliwa Kwa Sumu na mitego kwani huharibu sana mazao ya wakulima!

Sasa hizo route mnazo fanya kwenda kuangalia Gendere mmoja au watatu waliofugwa zingekuwa zinafanyika kwenda kijijini kuwapa darasa watu Ili wasiwaue zingezaa matunda sana.

Kwanini wakenya tukubali watuzidi Kwa kiasi kikubwa namna hii?

Ni hitimishe Kwa kusema Nia tunayo sana ya kufuga hasa wanyama na ndege rafiki Kwa bindamu hasa waliotajwa hapo juu akiwemo na mbuni na wengine wengi kama sungura pori nk


View: https://youtu.be/oD9HihuWTpU?si=4oT0_9ZZVcDy2DU4

Hata Ghana wanafuga Kwa wingi sana.


View: https://youtu.be/Sj3UGIYmGGY?feature=shared
 
Nadhani hatufugi kwa sababu ya gharama kubwa za kuanzisha na kuendesha mradi pamoja na soko dogo la bidhaa zao nikiwa na maana ya competition kutoka kwa wafugaji wenye mitaji mikubwa na wazoefu
 
Nadhani hatufugi kwa sababu ya gharama kubwa za kuanzisha na kuendesha mradi pamoja na soko dogo la bidhaa zao nikiwa na maana ya competition kutoka kwa wafugaji wenye mitaji mikubwa na wazoefu
Siyo kweli hata kidogo mbona njiwa wanauzwa milioni moja? mbona kuku wa mapambo wanauzwa hadi laki7?
Kuku jamii ya kuchi kuuziwa laki3-4 ni kawaida.Je! kwa mifani hiyo Tausi hatuwezi nunua kwa m5 pair? maana wakenya wanauza 150k kwa pesa yao ni sawa na m3 kasoro ya kibongo sasa tunashindwa vipi mkuu?
 
Nadhani ni hazina ya taifa au kuna jina lingine wamepewa mana ninachofaham wana historia ya kutokea India na kuletwa hapa na nyerere kama zawadi enzi za uhuru
Sheria za kipumbavu hizi hapo kenya wanauza kwa 150k kwa pesa yao japo kuna aina kadhaa zingine hadi m1 kwa pair kwa hela ya kenya.

Sioni kama kuna haja ya kuzuia kuwafuga kama mtu anahitaji
 
Nadhani ni vile sisi tunafuga zaidi kwa ajili ya matumizi.ya chakula.

Lakini mtu unaweza kufuga mnyama yoyote Tanzania ni swala la kufuata utaratibu tu kama mnyama/ndege husika ni mnyama/ndege pori.

Kwa ndege jamii ya kanga, ni vile tu serikali imeamua kufumbia macho ila kimsingi unatakiwa kuwa na vibali kumfuga sababu ni ndege pori hivyo ni nyara ya serikali.

Ila hapa Tz unaweza kufuga hadi simba ni wewe tu na uwezo wako na kuwa na vibali husika kiongozi.

Nikifa MkeWangu Asiolewe
 
Back
Top Bottom