Kwanini Mbuni, Tausi na Kasuku hatufugi Kwa wingi hapa Tanzania?

Inasikitisha sana
Kinacho sikitisha zaidi ni serikali hii hii kuwapa wazungu wanyama pori na kuondoka nao huku sisi tukiwekewa vigezo na masharti magumu yasiyo na maana yoyote ile. Ukweli tunaongozwa na watu wasio na upeo kabisa
 
Kanga pori wanafugika. Teke moja la mbuni linaua mtu.
Hivi mkuu unawaza madhara tu huwazi kingine? kasuku ana madhara gani?tausi ,swala,nyumbu na digidigi wana madhara gani kwa bindamu?

Mbona hujiulizi wenzetu hapo kenya wanawafugaje? kule india wanafyga hadi tembo na kumbebesha mizigo wewe ushindwe kufuga mbuni serious?
 
Kuna sababu watu walifuga Ng'ombe na kuacha Nyumbu na swala. Swala akikupiga pembe ni kama umepigwa mkuki. Pia si madhara yao tu, na welfare yao imezingatiwa. Swala ukimfungia bandani atapiga ukuta hadi afe. Digididi ukiwafungia hawazaliani nk nk. Mengine kama kasuku unakuta kuzuia magendo ya wanyama. Mambo ni mengi.
 
Kuna mchangiaji kasema hadi uwe na heka 500.Hii ina maana kwamba kwa mtu wa kawaida sana kama sisi wenye heka 5 wala tusifikirie kabisa.

Nadhani bado tunahitaji hii sheria na masharti yapunguzwe yaani kiwe kibali tu hasa kwa ndege rafiki na wanyama rafiki wasio na madhara kwa binadamu. kama nilivyosema kuna jamaa aliwahi fuga gendere lakini wakaguzi walikuwa hawachelewi kuja kuwaona wale gendere sasa mambo hayo yote ni ya nini?

Unataka kufuga kasuku masharti kibao yasiyo na tija yoyote.
 
Mkuu mbona huko kwa wenzetu wanafuga vizuri tu? Swala kutokuzaliana ni issue nyingine hata bata bukini anaweza wasizaliane vilevile
 

Sina uhakika na hili la sharti la eka 500 ila labda nipitie upya kanuni za maliasili na vibali vyake Mkuu.

Ila kuna kipengele cha kulipia ada kwa kila nyara tena
 
Sababu zako wala hazina mashiko,kwani hata ng'ombe akikupiga na pembe ndio huwezi kuumia?Na kuhusu digidigi kwa mfano nimewanunua wawili tu na sitaki wazaliane ndio utanizuia kufuga kisa hawazai kwani mimi nahitaji wajae banda lote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…