Kwanini mbwa wanatupiwa mawe?

Kwanini mbwa wanatupiwa mawe?

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
6,373
Reaction score
16,073
Sijui ni desturi ya huko Tanganyika ama ni nini? Mtu akimuona mbwa lazima amtupie jiwe!

Nafikiri hii pia ni mojawapo ya zile "tamaduni za kitanganyika" ambazo zinapigiwa makelele mpaka wameamua kuunda programu maalumu ya kwenye redio ili KUHUBIRI na KUTANGAZA UTAMADUNI WA KITANGANYIKA.

Na nimesikia hapo mwakani kutakuwa na somo la UTAMADUNI WA KITANGANYIKA huko mashuleni. Hili nalo liingizwe.

Mbwa wengi wamegeuka kuwa mbwa-koko kwa sababu ya kupigwa hovyo, kurushiwa mawe, kufokewa na kunyanyaswa.

Mtu akiona mbwa tu ni kama anapata mtikisiko wa neva, unashangaa anaokota jiwe anambonda nalo! Kwa hakika huu nao ni UTAMADUNI WA KITANGANYIKA. Inashangaza.

Sijawahi kuona watu huko Tanganyika wakiwaheshimu wanyama hususani mbwa! Kama wapo basi ni wachache sana.

Unashtukia tu mtu ameokota kajiwe kake anamrushia mnyama! Akimkosa anaongeza la pili, ni kama JUHUDI fulani hivi!

Kuna haja ya mitaala shuleni kuanza kufundisha watoto tabia ya kuheshimu wanyama! Haya mambo ya UTAMADUNI WA KITANGANYIKA wa KUWABAMIZA WANYAMA hebu tuachane nayo!

Naamini hili nalo wahusika wa Jamiiforums watalichukua na kulisambaza mitandaoni ili kueneza hii elimu ya dharura! Wanyama wanaumizwa sana na hakuna wa kuwasemea!

Huwa naonaga Jamiiforums wanasambaza taarifa zao huko facebook kwa kuwanukuu "WADAU" mambo waliyoyapost humu. Na hili nalo mlichukue na MKALITIZAME.

Asante.
 
Nafikiri hii pia ni mojawapo ya zile "mila za kitanganyika" ambazo zinapigiwa makelele mpaka wameamua kuunda programu maalumu ya kwenye redio ili KUHUBIRI na KUTANGAZA MILA ZA KITANGANYIKA.

Mbwa wengi wamegeuka kuwa mbwa koko kwa sababu ya kupigwa hovyo, kurushiwa mawe, kufokewa na kunyanyaswa.

Mtu akiona mbwa tu ni kama anapata mtikisiko wa neva, unashangaa anaokota jiwe anambonda nalo! Kwa hakika huu nao ni UTAMADUNI WA KITANGANYIKA. Inashangaza.
Na kama wakinatiana ndiyo balaa watakimbizwa hata kilomita 5 na mawe juu
 
Umeongea Ukweli mtupu moja kati ya Tabia inayonikera na Kuniumiza sana ni Kuonea Wanyama na Waathiriwa wakubwa wamekuwa ni Mbwa na Paka. Inabidi Programm ya dharura ianzishwe ili Kuvitetea hivi Viumbe.
Kwa kwelii.

Watoto wamekuzwa kwenye UTAMADUNI WA KITANGANYIKA ambao umewaaminisha kwamba wanyama wanatakiwa kupigwa na kufukuzwa.
 
Hao watakuwa sio mbwa bali "mbwa"
koko wanaokamata kuku za watu mtaani
kwa hiyo wajumbe wanalipa kisasi.
Wanakamata kuku kwa sababu hawapewi chakula.

Unataka wakale wapi labda?

Wewe mwenyewe usipokula siku moja tu domo linaachama na kuhorojoka mpaka unataka kukata roho. Sembuse mnyama ambaye hana SHAMBA!

Jamani! 🥴
 
Mbwa anaanzaje kuranda mtaani, akingata mtu nani anawajbika? Mbwa asiye na wenyewe anapaswa kuuwawa na afisa wanyama na kwenda kuchimbiwa. Hatuhitaji mifugo bila mpangilio. Hata wanyama pori wanalindwa wasiingie kwenye makazi ya binadamu. Punguza ujinga
 
Back
Top Bottom