Kwanini Michael Carrick hakupewa nafasi Timu ya Taifa ya England?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Hivi ni kweli Michael Carrick katika ubora wake ule katika nafasi ya Holding Midfielder kwanini hakupata nafasi ya kuchezea timu ya taifa ya England?

Carrick anajua kukaba, anajua kuziba nafasi, anajua kuanzisha mashambulizi, anajua kupiga pasi fupifupi na pasi ndefu zenye macho na pia anajua kufanya interception.

Lakini pamoja na ubora wake wote huo Makocha kadhaa wa timu ya taifa ya England walimpa nafasi finyu sana, na ikapelekea timu hiyo kutopata mafanikio katika michuano ya kimataifa kama vilr ya Kombe la Dunia na Kombr la Mataifa ya Ulaya.

Kwanini Carrick hakupewa nafasi? Naamini England ingefika mbali sana kama Carrick angepewa nafasi ya kutosha kwenye timu ya taifa ya England
 
Kupewa nafasi ki vipi??

kama kuitwa National team alikuwa anaitwa lkn ilikuwa ngumu sana kusema Steven Gerad akae bench au Super Frankie Lampard halafu aamze huyo...

Waingereza wenyew wanajua ndiyo maana hawaongei...Carrick ndiyo mzuri lkn huwezi mueka Gerrard nje halafu acheze huyo labda kwa game flan flan tu...

Muache Gerard aitwe Gerard na Super Frankie Lampard
 
UK hata media zinawaharibu sana wachezaji wao..mfn sasa hivi wanasema Lingard ni Messi wao mtarajiwa...hahahaha

Wachezaji.wa UK wengi media zinawagharim sana na wanaridhika wakifikisha miaka 24 hamna kitu

Wale mpira wao ni wa kudesa class mpira wa kufundishwa class
 
Acha uongo we jamaa...mi nipo UK na ni mshabiki na mfuatiliaji wa mpira lkn sikuwahi kusoma wala kusikia hizo habari zako za "Messi mtarajiwa"
 
Dany Mussa Noel Drink water ktk form yake yote ameitwa mara 1 tu ktk National team
Drinkwater aliitwa wakati team inajitayarisha na mechi za kirafiki na ujerumani na Brazil akachomoa sababu tu alikuwa ametoka kwenye majeraha na alikuwa anajifua kwa kupata namba kwenye kikosi cha Chelsea. ....wengi wakammaind kwa hicho kitendo, so unategemea ataitwa tena?
 
Hata angeenda. Mpira unachezwa uwanjani na siyo mdomoni kama walivyo england na vyombo vyao vya habari. Wangeishia kupigwa tu.
 
Huwa inatokea katika maisha ya soka, Steve Bruce akiwa nahodha wa Man Utd katika kiwango cha hali ya juu sana aliishia kuitwa mara 1 tu kwenye timu ya taifa.

Inawezekana makocha waliona Carrick kuna vitu anamiss. All in all amepata heshima kubwa sana klabuni Man Utd.
Steve Bruce Garry pallister , Peter scheimel hao jamaa Ni noma
 
Hapa Frank Lampard pale Steven Gerald angecheza wapi
Hapo alitakuwa aitwe kwani carrick anatoa options tofauti eg kupiga long pass , tatizo kubwa england hawanaga kocha , tena afadhali sougathe kuliko roy
 
Humu naona wengi mnaongea lakini seems like hamjui vizuri mpira, Carrick ni holding midfielder, anacheza namba 6 mara nyingi, Lampard na Gerrard wanamnyimaje namba wakati wao ni namba 8?

Carrick amekua akiitwa national team akiwa kwenye early 20's but hakuwa akicheza kwa Sababu ya Paul Scholes ambaye alikua akicHeza ka holding midfielder, je Carrick on his best ana uwezo wa kumuweka benchi Scholes?
 
UK hata media zinawaharibu sana wachezaji wao..mfn sasa hivi wanasema Lingard ni Messi wao mtarajiwa...hahahaha

Wachezaji.wa UK wengi media zinawagharim sana na wanaridhika wakifikisha miaka 24 hamna kitu

Wale mpira wao ni wa kudesa class mpira wa kufundishwa class
Tatizo kubwa la england ni makocha wao ni hovyo , mfano euro iliyopita england ilikuwa na timu nzuri saana lakini kocha hamna kitu kabisa, tena southgate anajitahidi kuliko roy
 
Una rashford, delle , vardy , kane , chamberlain halafu unashindwa kufunga hata hata kwa counter attacks , timu kama ile angeeipata kocha italy au didier deschamps england wangefika mbali euro , england kocha hovyo ( hodgson)
 
Humu naona wengi mnaongea lakini seems like hamjui vizuri mpira, Carrick ni holding midfielder, anacheza namba 6 mara nyingi, Lampard na Gerrard wanamnyimaje namba wakati wao ni namba 8?

Carrick amekua akiitwa national team akiwa kwenye early 20's but hakuwa akicheza kwa Sababu ya Paul Scholes ambaye alikua akicHeza ka holding midfielder, je Carrick on his best ana uwezo wa kumuweka benchi Scholes?
Kwanza kabisa Scholes sio kiungo mkabaji kama unavyojaribu kutuaminisha.

Pili Scholes alistaafu timu ya taifa punde tu baada ya mashindano ya Euro 2004, je Carrick alishaanza kucheza kwa kipindi hiko? jibu ni HAPANA.
 
Carrick ni holding midfielder aliekua anacheza as deep lying midfielder.

Carrick katoka tottenham as holding midfielder, kaenda Man utd 2006 coz ferguson alikua anatafuta replacement ya Keane, Carrick akawa ana pair na Scholes yeye anacheza as holding midfielder Scholes anacheza mbele yake,
Carrick kacheza finali zote mbili za Champions league as holding midfielder ina maan hujawahi kuli notice hilo mkuu?
 
Carrick ni holding middle na attacking middle ni kama vile ander herreira
 
Back
Top Bottom