Yaani ukisikia pesa inayotengwa na serikali kwa ajili ya mifumo mbali mbali nchi hii unawezwa kutokwa machozi.
Pesa nyingi utengwa kwa ajili ya ma IT wa mchongo ili kupiga TU pesa ya wananchi.
Mfano ninazaidi ya miezi 6 nafatilia kusajili jina la biashara huduma ambayo utolewa na BRELA. Lakini bahati mbaya sijawahi kufanikiwa kwa mfumo wa BRELA jambo Hilo.
Nilipojaribu kufatilia kwenye office za BRELA, kwa dharau kabisa yule mhudumu ananiambia "huduma ya kusajili jina la biashara gharama ni 20,000 ukifanya mwenyewe ila kwa kuwa mtandao unasumbua leta 50,000 nikusajilie"
Hivyo hapo ukipiga hesabu itanibidi nilipie 70000 ili kupata huduma ambayo gharama zake kama mfumo ungekuwa mwepesi kwetu sisi wananchi ningelipia 20,000 TU. Sikuweza kulipa hiyo pesa nipo napambana na mfumo ambao nimemaliza kujaza taarifa zote ila kutumia taarifa imegoma.
Sasa najiuliza kama nchi hii viongozi Hadi mawaziri wanakiri ajira hakuna, jambo kama hili la mfumo wa kusajili biashara mpya ambalo lilitakiwa liwe jepesi ili kusaidia biashara mpya ziweze kusajiliwa na kurasimishwa ili kukuza biashara nchini. Lakini kwa staili hii ya mifumo kama hii watanganyika tutasubiri sana.
Mdau na wewe ni mfumo upi wa serikali unaokupa changamoto ambazo hazina maana yoyote?