Kwanini Migahawa ya Wakristo Tanzania haina chakula kizuri?

Dah tukuwache tu mkuu bora. hatuwezi kujua mazingira yako unakotoka na ulivo yapo vipi
Uchagani.umeshawahi kunywa supu mikoa ya kaskazini ?onja supu atakayotengeneza mchaga alafu onja ya wapemba .utapata ninachomaanisha
 
Uchagani.umeshawahi kunywa supu mikoa ya kaskazini ?onja supu atakayotengeneza mchaga alafu onja ya wapemba .utapata ninachomaanisha

Ndo nikakwambia upo mbali. Ushakunywa supu ya waarabu au wahindi?
 
Wakristo lazima ukute chumvi imezidi
Mafuta yanaelea
Maharagwe yanakukodolea
Hawajui tumia nazi
 
Kwan dini ndio inapika?
 
Kuna vitu katika miaka ya hivi karibuni vimeanza kupuuzwa ktk madrassa zetu na hii inaweza ikawa ni sababu ya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii au kujua kwingi
Katika miaka ya zamani tukienda madrassa sio kusoma dini tu ilikuwa na shughuli nyingine kwa mfano kama kuna shamba la mwalimu basi walimaji walikuwa wanafunzi
Wanafunzi ndio tulikienda sokoni, wanafunzi ndio tulikifagia na kufua nguo za Sheikh na Mkewe bila kusahau mapishi na hizi shughuli tukizifanya kwa team work kwa hivyo tunapiga ndege 3 kwa jiwe moja yaani tunamsaidia Mwalimu+ tunasoma dini + tunajifunza life skills. Yamkini hiyo inaweza ikawa sababu ya dada zetu wengi kuwa mahiri ktk kupika

Kupika ni maarifa na kwa wengine ni talanta kuna jamaa tupo naye hapa Muscat jamaa ni Muhaya lakini anapika Biryani na pilau balaa hao wapakistani na wahindi wenyewe wanasubiri. Mtu yeyote duniani aweza jifunza kupika na akawa mahiri ktk fani hiyo bila kujali asili yake au dini yake

"Utamu wa pipi mate yako" si kila chakula ambacho ni kitamu kwako lazima kiwe hivyo kwangu kuna vitu sijui tumerithishwa au viko kihisia zaidi kwa mfano mtu anayetoka mikoa ya kusini atavyosifia ming'oko ni tofauti na mtu wa kaskazini au baadhi ya watu watavyosifia utamu wa bia, nyanya chungu, kahawa chungu au hata kikombe cha juice ya pilipili na supu ya chura kwa wabangladesh au kwa wali + mchuzi wa Wamalaysia wanaotia sukari to strike the balance is very difficult

Tunakula ili tufurahi au ili tuishi ??
Dunia hivi sasa inasumbuliwa na Lifestyle diseases na mojawapo ya kisababishi kikubwa ni vyakula na bahati mbaya zaidi vyakula vyenye ladha nzuri vimeonekana ndio visababishi vikubwa vya maradhi haya hivyo wakati tunajadiliana na utamu wa mavyakula ni muhimu kuwakumbuka kina Kansa, Kisukari, BP, bila Kusahau Figo. Na mwisho niseme
" Take your breakfast like a King, your lunch like a Prince and your dinner like a beggar"





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata chipsi za Wapemba au watu WaTanga zipo poa sana. Nenda pale njia panda ya Segerea kwenye mataa, kuna Mtanga mmoja pale kashika soko balaa.
Nje ya mabibo hosteli,kuna hoteli moja inaitwa kwa wapemba,ebana pale pilau lao huwa ni balaa!Sijui kama wapo siku hizi au vipi maana ilikuwa 2014 mara ya mwisho kula pale!
 
Pilau ya pale si ya kitoto, mbuzi mlainiiii
 
Hawajui baba angu...wanadhani kupika ni pilau na biriani tu baabaa angu...kuna mapishi hawajui kabisa.......wakipika mtori usishangae wakijaza mdalasini nA ilikii etiii
Utamu wa mtori pilipili manga
 
Unaijua adhabu ya kumbadilisha MTU kutoka dini ya allah hadi awe kafir?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…