Fundi_Mjasiriamali
JF-Expert Member
- Aug 13, 2018
- 748
- 1,340
Wakuu habarini za usiku,
Ni muda nimekuwa mtumiaji mzuri wa mkate katika kifungua kinywa cha asubuhi, lakini nime-kutana na changamoto ya kitafunwa hichi kuwa na chembe chembe za michanga ndani yake. Nimejaribu kubadili brand mbali mbali lakini naona hali ni ile ile.
Je, hali hii inasabishwa na mazingira ya uandaji wa mikate hii kabla ya kumfikia mlaji, au ni ngano wakati wa kuvuna na kusaga, au ni viwanda bubu vya mtaani ambavyo havina mazingira rafiki ya uzalishaji, au ni vyombo vinavyotumika huko viwandani au shida ni nini, au ni mamlaka husika kutokufanya ukaguzi kwenye viwanda!?
Kuna haja ya mamlaka ya chakula kufatilia hili, maana imekuwa kero kuanzia shida ya meno mpaka afya kiujumla.
Nawasilisha