Kwa nini mikoa ya kusini mwa Tanzania imeonekana kusahaulika kimaendeleo?
Serikali imekuwa haitoi fursa za kutosha za uwekezaji, licha ya kuwepo kwa rasilimali nyingi. Miundombinu bado ni dhaifu; kwa mfano, barabara za Kilwa–Liwale, Liwale–Nachingwea na Dar es Salaam–Lindi zina hali isiyoridhisha. Pia, baadhi ya majengo na ofisi za serikali Lindi bado ni za zamani.
Mikoa ya kusini inajulikana kwa uzalishaji wa korosho, lakini bado kuna uhaba wa viwanda vikubwa vya kuongeza thamani ya zao hilo. Kwa upande wa historia na utamaduni, Lindi na maeneo kama Kilwa yana urithi mkubwa, lakini bado hayajaendelezwa kikamilifu kuwa vivutio vya utalii.
Je, kuna sababu gani zinazofanya mikoa ya kusini kubaki nyuma kimaendeleo? Serikali imewasahau, au kuna changamoto gani inayozuia uwekezaji na maendeleo katika maeneo haya?