Kwanini mikopo ya Halmashauri inalazimisha vijana kujiunga vikundi

Kwanini mikopo ya Halmashauri inalazimisha vijana kujiunga vikundi

Habari

Kwanini taratibu za mikopo ya Halimashauri ambayo inatokana na 10% ya mapato ya halimashauri husika inalazimisha vijana watakaokopeshwa au kwenda kuomba ni lazima waende kivikundi na kuja na idea za vikundi?

Kwahiyo kwa mfano mimi nina kampuni yangu ya kuuza magari, au nina biashara ya studio ya photoshoot, au nina duka la nguo, au nina mgahawa wa kisasa siwezi kwenda kuboost mtaji wangu kwa kupata mikopo hii nafuu ili nikuze biashara yangu?

Sababu hasa huwa ni nini kinachofanya hawa jamaa wanalazimisha masharti ya kizee na ya kishamba namna hii?!

Kwani hizo hela wanatoa mifukoni mwao au ni za baba zao?!

Hela si ni zetu raia na zinahitajika kufanyia maendeleo yetu.

Hapa nilikuwa natazama kipindi hapo channel 5, DC anahojiwa kuhusu mikopo ya Halimashauri, anatetea hoja ya kuwepo kwa vikundi.

Katika kipindi wamekaribisha vijana wajasiriamali kuelezea maoni yao wengi wameonesha kukerwa na hii hoja ya vikundi na wamewaambia hao maofisa biashara waache kutumia mawazo ya kizee waje kitaa watazame biashara active ambazo zinahitajika mitaji ili kukua. Nyingi si za vikundi....

Vikundi vikundi kwani tunataka kucheza ngoma?

Kila mtu apambane kwa mbinu zake wanaotaka vikundi waende kwenye section ya vikundi, wanaotaka binafsi waende na business plan zao wakabidhi wapewe mpunga wafanye biashara.

Serikali imejazwa watu wenye mawazo ya kijima na ya kibwege sana . Ushamba ushamba tu. Wanajifanya wanazijua risk na hawajawahi kufanya biashara hata ya nyanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu; Upo msemo kwamba anayetoa hela ndio anachagua wimbo. Halmashauri inao utaratibu huo kwani ndio msimamizi mkuu wa utoaji wa fedha hizo. Kama utahitaji fedha hizo basi zingatia vigezo na masharti. Kama unataka kukopa fedha sio lazima ukakope Halmashauri kwani zipo Taasisi nyingine nyingi (microfinance institutions) zinazokopesha fedha.Unaweza kujaribu huko na uone kama hawana vigezo na masharti unayotakiwa uyazingatie. Acha kuing'ang'ania Halmashauri au kuishinikiza Kwa maneno makali eti ibadili mtindo huo. Kumbuka Fedha za Halmashauri ni mali ya Wananchi (ww ukiwa mmoja wao); na wananchi hao(Kupitia Wawakilishi wao i.e. Madiwani) ndo wameridhia Utaratibu huo.
 
Mkiwa kwenye kikundi ni vigumu kutoroka. Na pia mkitoroka ni rahisi kuwakamata. Mana ukishampata mmoja tu atabeba wenzake.
Vikundi ni siasa tu.

Huku Kilimanjaro vijana wanakopa, wakishapewa wanatimkia Dar.

Pesa nyingi hazirudishwi.

Wafanyakazi was Halmashauri wana maisha magumu bora wangekuwa wanakopeshwa hizo prsa, na zingerudi zote kwa 100%.

Kwanza walemavu huwa wanakopa hata mmoja mmoja.
 
Mkuu, Vikundi sio siasa kwani vikundi hivyo pia hupimwa kuona uahalisia na uhalali wake. Aidha vikundi hivyo hudhaminiwa na kabla ya kupewa fedha hupitia mchakato maalum unaozihusisha ngazi mbalimbali za Uongozi na hukaguliwa ili kuthibitisha uwepo wake.
Ni kweli pesa nyingi hazirudishwi lakini hiyo haijawa sababu kubwa kivile inayopelekea kuacha Utaratibu wa Vikundi. Ugumu katika marejesho upo pale ambapo Halmashauri inatakiwa kuwapeleka wahusika Mahakamani - kesi za Madai ni gharama kubwa (Na haiko kwenye Bajeti) na huchukua muda mrefu. Aidha mradi ulioibuliwa wa wanakikundi unaweza kutofanikiwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa wanakikundi husika e.g. Moto, Mafuriko, ukame, magonjwa ya mlipuko n.k. Ni kutokana na hali kama hiyo Halmashauri hutumia busara na kuwa waangalifu zaidi ili kuepuka hasara zaidi.
 
Mkiwa kwenye kikundi ni vigumu kutoroka. Na pia mkitoroka ni rahisi kuwakamata. Mana ukishampata mmoja tu atabeba wenzake.
Kwan watu wanaokwenda kukopa benki huwa wanatorokea wapi?!

Mbona bank watu hukopeshwa kwa option zote yaani aidha uende kama kikundi au mtu binafsi?

Kwan hawawezi kuja na utaratibu salama wa kupata taarifa za mtu na kuweza kuwa na uhakika wa udhamini wake na namna ya kumpata?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vikundi inasaidia watu kuwa commited hata kuwafatilia ni rahisi na mara nyingi wanaopata hiyo mikopo ni wanawake sbb ndio wako sana kwenye mambo ya vikundi na wote wanajuana tabia na washazoea kukopeshana.

Kuna kikundi tu juzi hapa wamepewa 400M
Wale hata kumi hawajafika na walienda kufanya jambo kwapamoja yaani kufungua zahanati.

Sasa mfano mtu ana biashara zake binafsi ambazo hataki kumix mitaji na mtu why kusiwe na mkopo wa aina yake ambao utamfanya aweze kusecure hata milioni kuanzia 10 pekee yake ili aweze fanya issue yake?

Vikundi huwa ni ngumu sana kufunction kwa watu mnaoanza biashara tamaa, majungu na wivu huleta uharibifu na kurudi nyuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ni mbinafsi simple tu afanye kuwakusanya ndugu zake watengeneze kikundi hewa
Sio ubinafsi. Si kila biashara utataka kufanya na watu. Management ya biashara inataka umakini na iwe monitored na aliyeleta idea. Sio kila mtu atake kucontrol hakutakuwa na matokeo mazuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo ni madhara ya Ujamaa....Alaaniwe nyerere kokote aliko
Nyerere kafanya nini mzee wa watu mbona vijana mnapenda kukosa adabu kwa ancestors wa taifa. Yule mzee ndie ameweka misingi mizuri ya taifa. Haya yanayoendelea hata hahusiki kuna watu wanatuchezea mchezo mchafu tu hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inamaana mtu mmoja hawezi kupata?
Sasa mfano mlemavu nitawatoa wapi wenzangu Hadi nipate kikundi?
Hawaoni kuwa ni busara kumkopa yule mlemavu mmoja aliyeonyesha uthubutu?Ajitegemeee kuliko kuwa omba omba!?
Mtu m'moja hawakupi yaani wapo kisiasa sana aisee. Masharti yao ni ya kishamba sana. Hawana ujuzi wa baishara na wengi wamekaa pale ila hawana ufahamu wa kutosha juu ya soko la mitaji linataka nini huku nje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jibu ni kwamba moja ya lengo la hiyo mikopo ni kwa ajili ya political propaganda za CCM. Ili uelewe vizuri subiri kipindi cha uchaguzi ambapo vikundi vya vijana na wanawake hukusanywa na kukopeshwa hela kwa sharti la kuwa na kadi ya chama na kuaminishwa kwamba pesa walizokopeshwa zinatoka CCM. Unapoona CCM wanaendelea kuitawala hii nchi kwa miaka zaidi ya 50 sababu ndo km hizooooo!
Kwanza ukifika unaulizwa kama unakadi ya chama. Wanataka watu wa chama cha kijani wapewe kipaumbele.

Pesa wanazitolea macho zile utadhani ni za urithi. Mfano hao waliopewa pesa wakafungua zahanati, nimeona yule Jerry Slaa alienda kufungua ile zahanati na wamelifanya kama jambo la kisiasa.

Ila kuna biashara ambazo ni za kisasa na zinataka mpunga na ukiwekwa mpunga hapo pesa ina rudi.

Hivi unakwenda Halimashauri unataka kukopa 200 milioni unataka kufungua hoteli watakuelewa?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya uchaguzi huku kijijin kwetu walitoa haya matangazo yao watu tukajioganaizi na tukapatikana 10,wakatufungulisha akaunti na madokumenti yet walichukua bt mpaka uchaguzi unaisha hakuna pesa wala nn
Majina yenu yalitumika kutolea hela na hilo deni wamelizika kama deni mfu lisilolipika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu; Upo msemo kwamba anayetoa hela ndio anachagua wimbo. Halmashauri inao utaratibu huo kwani ndio msimamizi mkuu wa utoaji wa fedha hizo. Kama utahitaji fedha hizo basi zingatia vigezo na masharti. Kama unataka kukopa fedha sio lazima ukakope Halmashauri kwani zipo Taasisi nyingine nyingi (microfinance institutions) zinazokopesha fedha.Unaweza kujaribu huko na uone kama hawana vigezo na masharti unayotakiwa uyazingatie. Acha kuing'ang'ania Halmashauri au kuishinikiza Kwa maneno makali eti ibadili mtindo huo. Kumbuka Fedha za Halmashauri ni mali ya Wananchi (ww ukiwa mmoja wao); na wananchi hao(Kupitia Wawakilishi wao i.e. Madiwani) ndo wameridhia Utaratibu huo.
Ndio tunapaza sauti taratibu zibadilishwe. Hii mikopo inaweza kutumika kuinua biashara za kati na kubwa kama itapelekwa kwa watu creative wasio na mitaji ya kutosha.

Kuna vijana wana photos studio. Wanataka kupata vitendea kazi kama computer za kisasa, kamera, taa, reflectors, meza, viti, software nzuri, etc. Unakuta anatakiwa kuwa na kama 30 million kuleta mapinduzi ili kuweza kuingiza faida na kuajiri watu zaidi na kurudisha pesa.

Why hiyo iwe ngumu sasa?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, Vikundi sio siasa kwani vikundi hivyo pia hupimwa kuona uahalisia na uhalali wake. Aidha vikundi hivyo hudhaminiwa na kabla ya kupewa fedha hupitia mchakato maalum unaozihusisha ngazi mbalimbali za Uongozi na hukaguliwa ili kuthibitisha uwepo wake.
Ni kweli pesa nyingi hazirudishwi lakini hiyo haijawa sababu kubwa kivile inayopelekea kuacha Utaratibu wa Vikundi. Ugumu katika marejesho upo pale ambapo Halmashauri inatakiwa kuwapeleka wahusika Mahakamani - kesi za Madai ni gharama kubwa (Na haiko kwenye Bajeti) na huchukua muda mrefu. Aidha mradi ulioibuliwa wa wanakikundi unaweza kutofanikiwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa wanakikundi husika e.g. Moto, Mafuriko, ukame, magonjwa ya mlipuko n.k. Ni kutokana na hali kama hiyo Halmashauri hutumia busara na kuwa waangalifu zaidi ili kuepuka hasara zaidi.
Mfano mimi nina garage yangu imeshaanza kufanya kazi. Au nina supermarket ndogo inayohitaji mtaji kama wa milioni 30 kuweza kukua na kuanza kupata faida kubwa na kuajiri vijana wenzangu wengi, kwann nijiunge kikundi ili niweze kuaccess mkopo wa halimashauri?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom