Kwanini miradi mingi ya serikali inachelewa huku miradi binafsi ikikamilika kwa haraka na viwango?

Kwanini miradi mingi ya serikali inachelewa huku miradi binafsi ikikamilika kwa haraka na viwango?

Pantosha

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
640
Reaction score
958
Hivi ndugu zangu naomba niulize ni kwa nini miradi mingi ya serikali huwa inachelewa au kufa kabisa na huku tukishuhudia miradi binafsi ikikamilika kwa muda na viwango vizuri. Shida ni nini?

1. Ukiritimba?
2. Usimamizi mbovu?
3. Poor project planning?
4. Ukosefu wa fedha?

Naomba wajuzi wa mambo watuambie.

Nimepita somewhere leo nikaona bango la mradi wa ujenzi wa barabara ya KM 1 ambayo imepangwa kujengwa ndani ya miezi 6. Miezi ilishapita wameishia kumwaga kifusi.

Nikawa najiuliza
1. Inakuaje serikali kuwa na mradi wa KM1?
2. Kwa nini ijengwe kwa muda wote huo?

Nikakumbuka nipo Afrika, nikaendelea na safari zangu.
 
Kwani kati ya nyumbani na kwa mchepuko wapi process ya kutoa hela inakua ndefu?
 
Miradi binafsi watu wametoa pesa zao wana uchungu napo

Miradi ya serikali watu hawana uchungu, ni sehemu ya upigaji
 
Miradi binafsi watu wametoa pesa zao wana uchungu napo

Miradi ya serikali watu hawana uchungu, ni sehemu ya upigaji
Miradi binafsi hawana muda wa kuchezea, pesa inatolewa kwa malengo, ufuatioiaji wa hali ya juu. Lakini pia mkandaras akizingua kupata kazi za mrad private institution ni kazi.
 
Nani mmiliki wa mali inayosimamiwa na serikali?

Ni mwananchi! lakini mwananchi huyo hana uwezo wa kuiwajibisha serikali aliyoiajiri ili ifanye hiyo miradi.

Hence shown :Clueless: !
 
Watanzania wengi ni wezi na wahujumu uchumi, ni vile tu wengine hawajapata nafasi.

Nina uzoefu na miradi ya serikali.

Akiwepo kiongozi mkali na mwenye msimamo thabiti, miradi haswa ngazi ya Halmashauri inaenda vizuri na kwa kiwango.

Hili nimeliona kwenye Halmashauri kadhaa nilizofanya kazi.
 
1.Makadirio ya Bajeti ya Nchi huwa hayafiki 100% baadhi ya miradi huchelewa kutokana na changamoto hiyo.

2.Mitaji ya wakandarasi wazawa wengi huogopa kuweka hela yao yote kwenye mradi kwani ukisema ukimbize mradi kwa hela yako halafu ubaki unaidai serikali unaweza filisika na Mali zako kupigwa mnada kwa kucheleweshwa malipo kutokana na kusuasua kwa Mapato.

3. Mabadiliko ya hali ya hewa kama mvua ingawa hii haina uzito sana maana unapochukua mradi inabidi uwe na mpango kazi wa kufanya kazi zinazoweza kufanyika wakati wa mvua.

4.Mkandarasi kupewa miradi mingi kuliko uwezo wake kutokana na sheria ya manunuzi kutokutoa ukomo wa kumpa kazi nyingi mkandarasi hivyo wataalam msipotumia busara mkandarasi anaweza kukumbatia kazi zote za mkoa wakati anajuwa hana uwezo.
 
Back
Top Bottom