Kwanini Misri inayafaidi zaidi maji ya Ziwa Victoria kuliko sisi wenye nayo?

Updates,
Baada ya utafiti kidogo nimegundua kuwa hili ziwa tunalimiliki kwa location tu na hatuna uhuru nalo.
ndio maana wamisri huwa wanakuja kutuchimbia visima huku ili kutuondolea mawazo ya kutumia maji ya ziwa hili.
inaonekana hata tukiforce inaweza sababisha hata military conflict.
 
Tulitumie tu, military conflict ni nzuri ili pia na sisi tufanye mazoezi tusije kuwa kama jeshi la Kenya japo ni risk
 
Mto Nile siyo mto mkubwa kabisa Africa, hata kwenye kumi bora haupo. Ma maji yake mengi, zaidi ya asilimia 60 yanatoka Ethiopia na siyo ziwa Victoria. Nakubali kuwa tuna ufala wa kushindwa kutumia ardhi na maji tuliyopewa kufanya kilimo cha umwagiliaji.

Wanakopa pesa na kwenda kujenga daraja la kuvuka baharini ili wapate sifa 'wamependeza' badala ya kwenda kujenga miradi ya umwagiliaji. Tabia za watu limbukeni.

kama 60% ya maji ya mto nile yanatoka ethiopia,kwa nini tukiyagusa wamisri wanaongea sana?
unafikiri kwa nini wamisri wanatuchimbia visima sana huku?
 
Umesema wamisri walipinga sana, tafsiri yake ni kwamba hatuna mamlaka na maji hayo hata kama yapo kwetu.

na kama wametulia maana yake pia hatuyatumii ipasavyo bado wanafaidika wao.
Subiri mradi uishe tutapata picha kamili
 
Mbona kikwete alianzisha mradi wa kuyavuta Maji ya ziwa Victoria kufika Dodoma ila mpaka Sasa yamefika Nzega kuelekea shelui and so on. Huo mradi ulipingwa sana na Misri Hadi kutishia kutuma ndege vita kama tutaendelea mbele na mradi huo.

Unless useme tumechelewa sana ila matumizi yameshaanza na mradi ukikamilika maeneo ya Kanda ya kati yatasahau ukame.
mpaka sasa maji yamefika igunga sheria tabora nzega kahama
 
Sababu Hatuna Nguvu Ya Kijeshi.

Tuyatumie Tutakavyo, Kisha Wakileta Vurugu Watulizwe Kijeshi, Hiyo Mikataba Ya Kikoloni Ni Mapambo Tu..

Ethiopia Walikataa Kabisa Kuwasikiliza Mbona Wakatulia..
 
kama 60% ya maji ya mto nile yanatoka ethiopia,kwa nini tukiyagusa wamisri wanaongea sana?
unafikiri kwa nini wamisri wanatuchimbia visima sana huku?
Asilimi karibu 30 si ndogo. Wanahitaji kila tone
 
Tangu nikiwa shule ya msingi nimekuwa nikisikia habari za mto nile. Mto nile ndio mkubwa zaidi barani Africa na chanzo cha maji yake ni ziwa victoria. Misri wanautumia mto huo kwa kilimo cha umwagiliaji chenye tija sana kwa nchi yao.

Tija ya ziwa hili kwa nchi yetu sijawahi kusikia zaidi ya uvuvi na maneno kwamba Mungu katubariki rasilimali hii na ukifuatilia zaidi hata mikoa inayozunguka ziwa hilo huwa inakubwa na uhaba wa maji.

Kwanini hakuna sifa ya kutia fora kwa nchi yetu juu ya ziwa hili zaidi ya kujisifu tu tunalo?

Kwanini nasi tusitumie kwenye kilimo cha umwagiliaji chenye tija sana kama hao wenzetu wa misri? Shida nini huku kwetu?

Hamna akili ndo shida
 
Back
Top Bottom