Kwanini Mkapa??Je CCM Kugawanyika??..Yes I said Makamba Jiuzuru

Kwanini Mkapa??Je CCM Kugawanyika??..Yes I said Makamba Jiuzuru

Bora kuyazungumzia sasa yanayomhusu Mkapa kuliko kutoyazungumzia kabisa, aendelee kutanua tu.

Huwezi kunyamza au kumwacha "apumzike" Mkapa ilhali kila kukicha tunasikia watu wakijiuzulu Chenge alikuwa AG kwenye serikali ya Mkapa baraza la mawaziri la Mkapa JK akiwamo ndilo lililopitisha mkataba yote mibovu.

Na ndio maana JK hawezi kufanya kitu chochote kwenye hili kwani yeye ni part and parcel of everything wenziwe si watamshangaa?
 
1.

1. Mkuu FDR acha jazba, nimeomba ufafanuzi kwanza ndio nitoe hukumu sasa nitende haki ipi hiyo bilka kujua charges?

2. Kwa kutumia hicho kichwa cha habari, kwamba eti CCM itagawanyika kwa sababu ya mkapa? Au kwa sababu ya kutaka achunguzwe? Kwa sababu siioni sababu yoyote ya msingi hapo ya kuifanya CCM iliyokuwepo kabla mkapa hajajiunga nayo (TAA) ya kina Doss Aziz ivunjike, haitavunjika, lakini makpa atachunguzwa na kufikishwa kwenye sheria.

3. Hivi Gembe, hebu kuwa mkweli hivi Makamba toka amekuwa katibu wa CCM, naomba nitajie one thing as a policy au utekelezaji alichowahi kufanya ambacho ni so bad kwamba anahitaji kujiuzulu? Amekaa muda gani kwenye hiyo nafasi kiasi kwamba amevuruga tayari na anahitaji kuondoka?

Ndio maana mkuu FDR niliomba ufafanuzi zaidi, je sasa ninaweza kuupata?

Good analysis Mkulu. Nasubiria majibu sasa toka kwa wale watetezi wa mkapa.
 
Bahati ya CCM ni moja tu.

Tanzania hapajapatikana upinzani wa maana - I am more convinced of this than ever - hakuna upinzani. Gembe, mbona itakuwa baraka sana kama utabiri wako wa CCM kugawanyika utakuwa kweli?

Can't wait for that to happen, and let it be sooner, ----please!
 
Gembe, mbona itakuwa baraka sana kama utabiri wako wa CCM kugawanyika utakuwa kweli?

Kumbe ni utabiri? nilifikiri ni fact...kama ni utabiri tu you can have it!

CCM haiwezi kugawanyika kwa sababu ya uchunguzi wa mkapa, haikugawanyika kwa sababu ya Lowassa wala the mighty Chenge, na ilikuwapo kabla wote hawa mafisadi hawajajiunga nayo, pleaseeee!
 
Kumbe ni utabiri? nilifikiri ni fact...kama ni utabiri tu you can have it!

CCM haiwezi kugawanyika kwa sababu ya uchunguzi wa mkapa, haikugawanyika kwa sababu ya Lowassa wala the mighty Chenge, na ilikuwapo kabla wote hawa mafisadi hawajajiunga nayo, pleaseeee!
Mkuu FMES,unafikiri ni sababu gani iliyofanya KANU ikapoteza Mwelekeo,embu nenda nyumba angalia historia ya KANU kuanzia mwaka 1990 mpaka 2000 utaniona ni kwanini ilifikia ikakosa nguvu nahuku ndiko tunakokwenda.

simple Fact,umekuja kwa Jazba,Mie nimesema CCM itagawanyika,wewe umefikia kusem aCCM itafunjika,hiyo ni Conclusion yako ila siyo maana yangu,Mie nimeelezea kwa umakini mkubwa hoja yangu,kama unakumbuka Jinsi ambapo Mtandao ulivyoigawa CCM mpaka JK alipotangaza kuvunja Kikundi.

Kuhusu Mzee Makamba,
Alichoharibu ni kushindwa kwanza kumaliza Mgogoro wa Zanzibara,yeye kama aKatibu Mkuu wa Chama ameshindwa kuwashawishi wajumbe wakubali maoni waliyoafiki an CUF badaye akawapotosha kwa kutumia gia kwamba CCM zanzibar wamekataa.tabia ya Unafiki.

Suala lingine ni kwa yeye makamba kumtetea Lowassa kipindi cha Kashafa ya RDC,na bila Heshima ya Jk kwa tingatinga Basi huu ndio ulikuwa Mwanzo wa CCM kuanza kugawanyika.Heshima Mbele kwa Malechela.

Tatu,
Mhe. Makamba ameshindwa kumaliza migogoro ambyo inaendelea katika Chama,hususiani kati ya viongozi katika mikoa na wilaya,na migongano mingine inamhusu yeye mwenyewe,mfano huko Tanga ambako yeye hauziki.

Mgogoro wa CCM, mbeyea,Je yeye amesimamia wapi?watu hawajui ni nani kiongozi na nani siyo kiongozi.hili ni tatyizo na limeanzia juu.
 
1.
Mkuu FMES,unafikiri ni sababu gani iliyofanya KANU ikapoteza Mwelekeo,embu nenda nyumba angalia historia ya KANU kuanzia mwaka 1990 mpaka 2000 utaniona ni kwanini ilifikia ikakosa nguvu nahuku ndiko tunakokwenda.[/B
]

KANU ilitolewa madarakani na Moi kwa sababu zake binafsi, alijua kuwa baada ya maovu mengi aliyoyafanya akiwa kwenye power, dawa ya yeye kutokuguswa akitoka ni ku-make a deal na rafiki yake mprnzi Kibaki, huenda hii hujaiona vizuri kwenye siasa za Kenya, alimuachia Mkikuyu kwa makusudi makuu bro, na sasa hivi anaendelea kutanua tu, lakini it has nothing to do with KANU as a chama cha siasa!

2.
Gembe

simple Fact,umekuja kwa Jazba,Mie nimesema CCM itagawanyika,wewe umefikia kusem aCCM itafunjika,hiyo ni Conclusion yako

[SIZE="3"]FMES[/SIZE]

CCM haiwezi kugawanyika kwa sababu ya uchunguzi wa mkapa, haikugawanyika kwa sababu ya Lowassa wala the mighty Chenge, na ilikuwapo kabla wote hawa mafisadi hawajajiunga nayo, pleaseeee!

Mkuu acha uongo na jazba, wewe umesema itagawanyika na mimi nimesema haitagawanyika, ushahidi huo hapo juu, tizama maneno yako na yangu, kuwa mkweli mkuu, hapa JF hatupendi uongo!

3.
Kuhusu Mzee Makamba,
Alichoharibu ni kushindwa kwanza kumaliza Mgogoro wa Zanzibara,yeye kama aKatibu Mkuu wa Chama ameshindwa kuwashawishi wajumbe wakubali maoni waliyoafiki an CUF badaye akawapotosha kwa kutumia gia kwamba CCM zanzibar wamekataa.tabia ya Unafiki.

Mkuu hapa pia huna hoja kabisaa, kwa sababu katibu wa CCM kwenye muafaka ankwenda kuwakilisha tu mawazo ya mwenyekiti na makamu wa visiwani, sio mawazo yake, kama hoja yako ya kushindwa kwa Makamba kutatua hilo tatizo lingekuwa kweli, basi tatizo la muafaka lilitakiwa kuwa limemalizwa na Mangula,

Baadhi ya wana CCM tunazo akili za kutosha kujua kuwa Makamba, yupo tu kwa ridhaa ya mwenyekiti, lakini kwamba ana function yoyote au alaumiwe kwa anything as far as CCM is concerned, labda ni wewe tu ndiye mwananchi wa kwanza kumsikia akimlalamikia Makamba. Wengine wala huwa hatu-bother hata kama yupo CCM.
 
The name "Benjamini William Mkapa" 2006-2008 ni jina lililotajwa sana JF,Magazetini,Vibarazani isipokuwa ktk nyumba za ibada ,ametajwa sana kushinda jina la muumba, kuna nini hapa waungwana, is it UFISADI tu au? JK anataka kutupa somo gani? CCM na Bunge lake wanataka kutueleza nini? Ipo siku tutauona ukweli lakini lililo bora na hakika soon as JK akiiachia nchi huyu bwana Mkapa atapigiwa mfano wa matendo yake yote kwa umma wa TZ na siyo JK. Tusubiri na tuombe uhai maana waswahili wanasema anayecheka mwanzo na yule achekaye mwisho ,mfaidi ni yule wa mwisho.
 
Kama ni kweli cha muhimu ni kuomba immunity iondolewe ili tuanze kazi ya ukweli,

Kiongozi msafi Mwalimu, siku alipotuhumiwa na Kambona pale Jangwani kuwa yeye na Kawawa ni wezi, guess what? Hawakujificha nyuma ya kustaafu na kwamba hawahusiki na siasa tena, kesho yake walijitokeza na kujibu mashambulizi na kumpa wiki moja Kambona atoe ushaidi au wamfikishe kwenye sheria kwa kusema uongo, au aombe radhi, Kambona alishindwa kutoa ushahidi,

Sasa kiongozi msafi na mwenye record nzuri, mwenye kuturekebishia uchumi, aliyejenga bara bara, aliyeacha surplus kwenye bank ya taifa, anashindwa nini kujitokeza kujibu mapigo na mfano upo uliowekwa na Mwalimu na Kawawa, viongozi wasafi?

Off Course alianza kucheka yeye alipokuwa antufisadi, sasa ni zamu yetu wananchi kucheka mwishoni!

And I love every moment of it! JF hatutakubali anything less than ukweli tena wote!
 
Back
Top Bottom