Kwanini Mke wa Ayubu kwenye biblia hakuguswa kabisa na shetani?

Alikuwa sehemu ya jaribu tu usifikiri shetani alimsahau wala nini!
“Mtu ajaribiwapo asiseme, ‘Najaribiwa na Mungu, maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.”
Yakobo 1:13.



“Bwana Mungu wako alikuongoza miaka arobaini jangwani, ili akudhalilishe na kukujaribu, ajue yaliyo moyoni mwako"

Kumbukumbu la Torati 8:2


????
 
Mke wa Ayubu alikuwa sehemu ya jaribu kihisia zaidi. Wakati Ayubu afya yake imedhoofika, watoto wote wamefariki; mke badala ya kutoa support kwa mumewe ndio kwanza anazidi kuhoji uhalali wa kuendelea kuweka imani na matumaini kwa Mungu ambaye alimsababishia mateso yote.

Shetani lengo lake lilikuwa kumkatisha tamaa (Ayubu) kupitia mke wake; huku mke wa Ayubu akiwa katika hali ya hofu, woga, huzuni vyote kwa pamoja
 
Huyu Mungu kama yupo kweli, anashindwa vipi kuwapa mwongozo juu ya mwaswali yanayoulizwa kila siku kuhusu vitabu vyake?
 
Hili swali huwa najiuliza sana. Kwanini shetani hamkugusa kabisa mke wa Ayubu? Ikumbukwe shetani aliua hadi watoto wote wa Ayubu lakini mke hakuguswa kabisa. Shetani huwa ana double standards kwenye kazi zake?

Kwa mantiki ya Biblia yenyewe, shetani hakumuua mke wa Ayubu kwa sababu alikuwa sehemu ya jaribu lake. Ndiyo maana baada ya watoto kufa na mali kuangamia, mke akamwambia:


“Je! Wewe bado washikamana na ukamilifu wako? Mkufuru Mungu ukafe.” — Ayubu 2:9


Hapo unaona wazi kazi yake ilikuwa kumshawishi Ayubu aanguke kiroho, si lazima kumuua kila mtu. Biblia pia inaonyesha shetani hutumia watu wa karibu kujaribu wengine:


Petro akawa kikwazo hadi Yesu akamwambia: “Nenda nyuma yangu, Shetani.” — Mathayo 16:23
Yuda alitumika kumsaliti Yesu — Luka 22:3

Kwa hiyo hoja yako ya “double standards” inaonyesha hujaisoma hata Biblia yako vizuri. Kila jaribu kwenye Biblia lina njia tofauti. Wakati mwingine shetani huharibu kwa mauti, wakati mwingine kwa maneno, ushawishi, au watu wa karibu.
 
1. Yakobo 1:13 — Mungu hamjaribu mtu kwa maovu

Biblia inasema Mungu hamshawishi mtu atende dhambi au uovu.
Hapa “kujaribu” ni kwa maana ya kumvuta mtu aanguke, kumshawishi atende dhambi, au kumwangamiza kiroho.

Mungu hana tabia hiyo.

Ndiyo maana Yakobo anaendelea kusema kuwa mtu huvutwa na tamaa zake mwenyewe.

Kumbukumbu la Torati 8:2 Mungu huwajaribu watu wake

Biblia hapa “kujaribu” ni kwa maana ya kupima imani, kufundisha utiifu, kufunua yaliyo moyoni, na kuwakomaza watu kiroho.

Ni kama dhahabu inapopita motoni ili ionekane safi. Kwa hiyo Mungu hapandishi uovu ndani ya mtu lakini Mungu anaweza kuruhusu mazingira ya mtihani ili imani ya mtu ionekane.

Kuhusu mke wa Ayubu

Katika simulizi la Biblia, si Mungu aliyemshawishi mke wa Ayubu kusema mabaya.
Baada ya Ayubu kupoteza mali, watoto, na afya mke wake alimwambia:
Je! Wewe hata sasa washika sana ukamilifu wako? Mkufuru Mungu ukafe (Ayubu 2:9)

Hapa tunaona mambo mawili
1. Mungu aliruhusu Ayubu apitie mtihani wa imani.
2. Lakini ushawishi wa kumkufuru Mungu haukutoka kwa Mungu.

Kwa lugha nyingine, Jaribio la mazingira liliruhusiwa na Mungu, lakini kishawishi cha kutenda dhambi kilitoka katika maumivu, udhaifu wa kibinadamu, na kazi ya Shetani.

Ndiyo maana Ayubu hakumlaumu Mungu kwa uovu huo.

Mistari hii haipingani kutoka na mtazamank wako kibiblia..
→ Mungu hashawishi watu kutenda dhambi.
→ Mungu hupima na kufundisha imani kupitia majaribu.
~Katika Biblia, Mungu aliruhusu mtihani, lakini hakumtuma mke wa Ayubu amshawishi atende dhambi.

NB: Najua bado utaendelea kupinga! Kila la kheri..🤸🏽‍♀️
 
Hii hata wana theologia wanazunguka zunguka tu ina mkanganyiko mkubwa biblia ni kitabu kimejaa mikanganyiko kama utatumia logic
 

Noma sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…