Kwanini mkoa wa Njombe una vilima vingi?

Kwanini mkoa wa Njombe una vilima vingi?

Nimeishi Mwanza!

Nimefika Chunya mkoani Mbeya.

Nimeshafika Iringa.

Zanzibar napafahamu.

Nimefika na maeneo mengineyo ya Tanzania. Ni mikoa miwili tu ndiyo bado sijafika: Mtwara na Lindi.

Japo nimeona vilima na miinuko maeneo mbalimbali ya Tanzania, sidhani kama kama kuna inayofikia ya Njombe.

Kwa barabara zenye kona nyingi, miinuko na miteremko mikali, huenda Iringa na Njombe inaongoza.

Kwa mkoa wenye vilima na miinuko mingi sana, naipa Njombe nafasi ya kwanza.

Kisayansi, hali hiyo imesabishwa na nini?

Ndo maana tumesema mkoa wa njombe sio wote Kuna halmashauri Zina tambarare mfano hii makambako gap Ina cover makambako tc wangingombe DC mbarali DC, na mufindi kUsini soma HiYo utapata kitu 👇👇👇👇👇👇👇👇👇♨️Jiografiahariri

Nyanda za juu zinajumuisha milima, volkeno na tambarare za juu, pamoja na Milima ya Mbeya, Milima ya Poroto, Safu ya Kipengere, Mlima Rungwe, Tambarare ya juu ya Kitulo, Milima ya Umalila, na Nyanda za Juu za Umatengo. Tambarare ya Juu ya Ufipa inaenea kaskazini magharibi, kati ya Ziwa Tanganyika na Ziwa Rukwa. [2] Matawi mawili ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki yanaungana katika Nyanda za Juu za Kusini. Kwa upande wa kaskazini mashariki, pale Makambako kuna pengo linalotenganisha Nyanda za Juu za Kusini kutoka Milima ya Tao la Mashariki. [3]

Ziwa Ngozi katika Milima ya Poroto.
Mlima Rungwe (mita 2,960 juu ya UB), na mlima Mtorwe (au: Mtove, m 2961) ndiyo vilele vya juu katika nyanda za juu. Vingine ni pamoja na Chaluhangi (m 2933) na Ishinga (m 2688) katika eneo la Kipengere, Ngozi (m 2621) katika Uporoto, na Mbeya (m 2826), Loleza (m 2656) na Pungulomo (m 2273) katika Milima ya Mbeya. [4]

Kutoka mitelemko ya kaskazini na mashariki ya Milima ya Mbeya maji hutiririka kwenye beseni la Ziwa Rukwa. Mto Ruaha Kuu ambao ni tawimto la Rufijiunapokea maji yake kutoka mitelemko za mashariki ya milima ya Mbeya na Kipengere.

Mto Songwe unapokea maji yake kutoka Milima ya Umalila ukiendelea kuwa mpaka kati ya Tanzania na Malawi. Mto Kiwira unakusanya maji kutoka mitelemko ya Milima ya Umalila, Milima ya Poroto na Mlima Rungwe.

Mto Ruhuhu unapokea maji ya sehemu ya kusini ya Safu ya Kipengere na Nyanda za Juu za Umatengo.

Mitelemko ya mashariki ya Umatengo hupeleka maji yao kwenda Mto RuvumaEastern_Arc_Mountains_sheme.jpg
 
Back
Top Bottom