Kwanini Mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi ya HIV Tanzania?

Carla

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2012
Posts
398
Reaction score
331


Kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia takwimu mbali mbali kupitia vyombo mbali mbali kuwa mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi na waathirika wa UKIMWI.

Swali langu ni la kidadisi(curiosity). Napenda kusikia toka kwa wataalamu na watafiti(kama tafiti zipo), kwanini isiwe majiji na mikoa mikubwa kama Dar, Mwanza, Mbeya n.k? Kama awali ilikuwa mkoa wa Kagera ndiyo ulioripotiwa mgonjwa wa kwanza na baadaye kuwa na waathirika wengi, ilikuwaje HIV iliruka mikoa ya hapo kati(Shinyanga, Tabora, Dodoma, Singida...) na kuufanya mkoa wa Njombe kuongoza?

Kama ni tohara kwa wanaume je, ni mikoa mingapi Tanzania hii walichelea kufanya tohara? Kwanini mikoa hiyo haijaathirika kiasi hicho? Japo kwa zamani(ninavyokumbuka) wilaya ya Makete(Njombe) ndiyo iliyokuwa ikiongoza na kwa sasa sina taarifa rasmi, bado ni jambo ambalo sina majibu yake, ilikuwaje mkoa wa Njombe uongoze kwa maambukizi?

Naomba wenye kufahamu majibu ya swali langu la msingi wanisaidie.

Kwanini Njombe?

 
Pia kwenye ulanzi kuna mavitu meupe meupe kama maziwa mgando yanatwama china yachupa au chombo ulimowekewa yale mavitu ukiyanywa VIAGRA cha mtoto jinsi chuma kinavokuwa kimenyooka ukitumia condom kwenye mechi inachanika hata kabla ya shoo kuanza so nikupiga kavu kavu na kupeana umeme tu
 
Mkuu sidhani kua watu wote wa Njombe walioathirika waliupatia ugonjwa huo mkoani mwao (Njombe)

Bila shaka kuna waliokua wakiishi mikoa mingine nje ya Njombe,lakini baada ya kujigundua kua wameathirika ndipo wakafanya maamuzi ya kurudi mkoani kwao ili kua karibu zaidi na familia zao,
So, linapokuja suala la kuhesabiwa waathirika watahesabiwa ni waathirika wa Njombe na hawatohesabiwa kua ugonjwa huo waliupatia mkoa gani!

Huenda ikawa watu wa Njombe wanatabia ya kurudi mkoani kwao baada ya kuathirika ndio maana idadi ikawa ni kubwa mkoani humo,

Nimejibu kwa mtazamo wangu tu na niko radhi kusahihishwa na wataalamu,

One love.
 
Hakuna jibu hadi sasa, hakuna mwenye takwimu sahihi
Mtoa mada hahitaji kujua "takwimu" bali anahitaji kujua "tafiti" kama zipo,kwanini mkoa wa Njombe uwe na idadi kubwa ya waathirika? Msome tena mtoa mada utamuelewa tu,
 
Niliwahi kumuuliza daktari flani wa njombe hili swali nilichoambiwa ni kuwa njombe kuna hospital kubwa kama ikonda hosp, bulongwa hosp, kibena hosp, ikelu hosp lugarawa na ilembula hosp. Zote ni hosptali kubwa sana hivyo watu wengi wanafika kupata matibabu huko kutoka sehemu mbalimbali na wakipimwa vvu takwimu zinasoma njombe kwakuwa watu wengi hawatoi taarifa sahihi wanatoka wapi... Ila sijui kama ndo uhalisia wenyewe
 
lete takwimu za Ukimwi Zanzibar ndio inaongoza kwa maambukizi kidogo kupita sehemu zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…