Takwimu zinaonyesha maambukizi njombe ni 14.8% na ndo mkoa unaoongoza. Sababu za maambukizi ya VVU kuwa juu ni:- Biashara ya viazi mviringo. Biashara hii huwaleta wafanyabiashara na madereva, matingo wa malory, na makuli ambao hulala vijijini wakikusanya na kupakia viazi. Watu hawa kwa kuwa na fedha hufanya sana ngono zembe na wanawake wa vijijini. Mbili, Tohara kwa wanaume haikwepo kwa Kabila la wabena, pangwa nk. Tatu, idadi ya wanawake mabinti ni ndogo kulinganisha na wanaume. Mkoa huu nazani ndio unaoongoza kwa kutoa house girls wengi Tanzania. Hivyo unakuta mwanamke mmoja anagombaniwa na wanaume kumi na zaidi no way out. Nne, Ulevi hasa kwa wanawake hasa njombe vijijini, na ludewa na makete pia. , Tano, house girls hurudi kwao na VVU na kwa uchache wa wanawake basi kila mwanaume kijijini ata mlala kwa uzuri wake.. Sita, uhaba wa kondomu vijijini. Maduka mengi vijijini hayauzi kondomu. Unaweza tafuta kondomu ludende siku nzima usiipate. Saba, biashara ya mbao nk