Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 146
- 351
Hivi hivi karibuni, tumeshuhudia operation kubwa ya kiudhibiti wa ubora na usalama wa vinywaji nchini Rwanda lililozua gumzo kubwa Afrika Mashariki. Lakini kinachoshangaza na kusikitisha zaidi ni jinsi Shirika letu la Viwango Tanzania (TBS) linavyolichukulia jambo hili kana kwamba halituhusu kabisa sisi Watanzania. Ukiangalia kwa umakini kile kinachoendelea, huwezi kuacha kujiuliza: hivi Mkurugenzi wa TBS bado anasubiri nini kuachia ngazi?
Kule Rwanda, mambo hayakuwa rahisi kama tulivyo ya chukulia. Chombo cha uchunguzi cha RIB kimemkamata Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (Rwanda FDA), Emile Bienvenu, akiwa pamoja na maafisa wengine 18 kutoka kwenye taasisi hiyo na Bodi ya Viwango (RSB). Wote hawa wanachunguzwa kwa tuhuma nzito za kutoa leseni na vyeti vya ubora kwa vinywaji visivyokidhi viwango na vile haramu bila kufuata utaratibu wa kamati za kiufundi.
Hapa ndipo swali linapokuja kwetu sisi raia wa kawaida: Ikiwa kiongozi wa taasisi kama hiyo nchi jirani anashikiliwa na polisi kwa sababu ya kuruhusu vinywaji hatari kuingia sokoni, Mkurugenzi wetu wa TBS hapa nyumbani anajisikiaje pale vinywaji hivyo hivyo vinapopatikana kwenye masoko yetu na kutumiwa na Watanzania? Kwa nini kwetu hakuna uwajibikaji wowote wala maelezo ya kueleweka?
Kwetu tunaiwaza Diplomasia, Wenzetu Wanapigania Afya zao
Kitu kinachoshangaza zaidi ni jinsi TBS inavyotazama kushoto wakati tatizo linaweza kuwa kulia. Wenzetu wa Rwanda wamelichukulia suala hili kama janga la afya na usalama wa jamii.
Sisi hapa Tanzania, TBS inaonekana kutaka kulifanya hili kuwa suala la kidiplomasia na mahusiano ya kibiashara tu. Badala ya kusimama kidete kama walinzi wa afya zetu na kupiga marufuku bidhaa zote zenye mashaka, wako bize kuangalia mambo kwa jicho la kisiasa. Je, biashara na diplomasia ni muhimu kuliko afya za wananchi wanaokunywa vinywaji hivi kila siku?
Kichekesho kingine kinachosikitisha ni majibu ya TBS katikati ya taharuki hii yote. Wakati wananchi tukiwa na hofu na maswali mengi juu ya vinywaji vilivyopigwa marufuku na orodha ya makampuni yanayohusika kuingiza au kutengeneza bidhaa hizo,
Hivi kweli huu sio usanii na kukwepa mpira? Yaani watu wanahoji usalama wa vinywaji vinavyoingia tumboni, taasisi inaleta habari za nondo na mabati. Huku ni kutudharau raia na kuonyesha wazi jinsi gani hawana ushirikiano na hisia za wananchi wanaowahudumia.
Kama Mkurugenzi wa TBS na timu yake wameshindwa kulinda soko la ndani na kutuhakikishia usalama wa afya zetu, na badala yake wanakimbilia kutoa matamko yenye mlengo wa kidiplomasia na matangazo yasiyohusiana na mada ili kutupoteza maboya, basi jambo la kiungwana lililobaki ni yeye kuachia ngazi. Tunastahili uongozi unaoweka afya zetu mbele, sio unaosubiri mambo yaharibike zaidi ndio uanze kujitetea.
Wakuu pigeni "Unde" hili suala la kidiplomasia na uingiliano wa Kibiasha tu, hapo Rwanda huko wanakompliketi mambo, sisi ndio wataalamu.
The EastAfrican
BBC
Kule Rwanda, mambo hayakuwa rahisi kama tulivyo ya chukulia. Chombo cha uchunguzi cha RIB kimemkamata Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (Rwanda FDA), Emile Bienvenu, akiwa pamoja na maafisa wengine 18 kutoka kwenye taasisi hiyo na Bodi ya Viwango (RSB). Wote hawa wanachunguzwa kwa tuhuma nzito za kutoa leseni na vyeti vya ubora kwa vinywaji visivyokidhi viwango na vile haramu bila kufuata utaratibu wa kamati za kiufundi.
Hapa ndipo swali linapokuja kwetu sisi raia wa kawaida: Ikiwa kiongozi wa taasisi kama hiyo nchi jirani anashikiliwa na polisi kwa sababu ya kuruhusu vinywaji hatari kuingia sokoni, Mkurugenzi wetu wa TBS hapa nyumbani anajisikiaje pale vinywaji hivyo hivyo vinapopatikana kwenye masoko yetu na kutumiwa na Watanzania? Kwa nini kwetu hakuna uwajibikaji wowote wala maelezo ya kueleweka?
Kwetu tunaiwaza Diplomasia, Wenzetu Wanapigania Afya zao
Kitu kinachoshangaza zaidi ni jinsi TBS inavyotazama kushoto wakati tatizo linaweza kuwa kulia. Wenzetu wa Rwanda wamelichukulia suala hili kama janga la afya na usalama wa jamii.
Sisi hapa Tanzania, TBS inaonekana kutaka kulifanya hili kuwa suala la kidiplomasia na mahusiano ya kibiashara tu. Badala ya kusimama kidete kama walinzi wa afya zetu na kupiga marufuku bidhaa zote zenye mashaka, wako bize kuangalia mambo kwa jicho la kisiasa. Je, biashara na diplomasia ni muhimu kuliko afya za wananchi wanaokunywa vinywaji hivi kila siku?
Kichekesho kingine kinachosikitisha ni majibu ya TBS katikati ya taharuki hii yote. Wakati wananchi tukiwa na hofu na maswali mengi juu ya vinywaji vilivyopigwa marufuku na orodha ya makampuni yanayohusika kuingiza au kutengeneza bidhaa hizo,
TBS wakatoa tangazo rasmi la kuitisha mkutano. Unapofungua ukurasa ukidhani wanatolea ufafanuzi usalama wa vinywaji, unakutana na taarifa inayowaita waagizaji na wauzaji wa bidhaa za chuma kwenye mkutano wa Ubungo!
Hivi kweli huu sio usanii na kukwepa mpira? Yaani watu wanahoji usalama wa vinywaji vinavyoingia tumboni, taasisi inaleta habari za nondo na mabati. Huku ni kutudharau raia na kuonyesha wazi jinsi gani hawana ushirikiano na hisia za wananchi wanaowahudumia.
Kiufupi hapa, uwajibikaji umekuwa sifuri. Nchi jirani viongozi wamewekwa ndani ili kupisha uchunguzi wa kina wa jinsi nyaraka za ubora zilivyotolewa kimakosa. Hapa kwetu, vinywaji vile vile vinazunguka mtaani, lakini hakuna kiongozi hata mmoja aliyesimama na akasema "hapa tulikosea, ninawajibika."Kama Mkurugenzi wa TBS na timu yake wameshindwa kulinda soko la ndani na kutuhakikishia usalama wa afya zetu, na badala yake wanakimbilia kutoa matamko yenye mlengo wa kidiplomasia na matangazo yasiyohusiana na mada ili kutupoteza maboya, basi jambo la kiungwana lililobaki ni yeye kuachia ngazi. Tunastahili uongozi unaoweka afya zetu mbele, sio unaosubiri mambo yaharibike zaidi ndio uanze kujitetea.