Kwanini Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Ulijadili Jina la Mgombea Urais Bila Agenda Rasmi kutoka Kamati Kuu na Halmashauri Kuu za CCM!

Kwanini Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Ulijadili Jina la Mgombea Urais Bila Agenda Rasmi kutoka Kamati Kuu na Halmashauri Kuu za CCM!

Ingekuwa kweli wasingehangaika kumhonga mbowe. Safari hii wamekwama, subiri hiyo Oktoba kama tutakuwa hai.
Tutafanya nini, tume yao, Jeshi lao, Mahakama zao, Bunge lao, Pesa zao. Sasa yeye Lisu ana nini kama si domo tupu. Hapa ni mwendo wa kushatap mkia juu.
 
Mara nyingi jambo au kitu fulani kinapoelekea kwenye anguko au kifo chake, mifumo ya kawaida ya utendaji kazi wa jambo au kitu hicho huwa inakuwa corrupted na kisha ina - colapse kabisa. Na hapo ndipo huo mwisho huthibitika..

Mfano wa karibu na rahisi ni hapa kwa jirani zetu Kenya. KANU chini ya Daniel Arap Moi ilipitia njia hii hii inamopitia CCM leo ilipokuwa inaenda kuanguka na kufa kabisa na kisha kupotea hadi leo...

Daniel Arap Moi na wazee wa KANU by then, kwa hofu ya kui - maintain "status quo" walitumia njia nje kabisa ya taratibu na kanuni za chama kuwalamisha wanachama wamkubali mtoto wa Jomo Kenyatta, Uhuru Kenyatta awe mgombea u - Rais kinyume na matakwa na mapenzi ya wanachama wao. Wazee wa establishment, wazee wakongwe wa chama hawakuelewa kabisa badala yake waliziba masikio yao na ufahamu wao...

Wanachama walilalamika na kupinga kama wafanyavyo CCM leo. Matokeo yake kaburi la KANU liko mpaka leo na marumaru zake ziking' aa tu kwa nje wakati ndani kuna mifupa na uozo wa maiti tu na imekuwa ni historia isiyovutia kabisa kuisoma...!

Ili uelewe nisemacho kila mmoja asome jinsi mfarakano ndani ya KANU mwaka 2002 uliosababisha anguko kuu la chama hicho👇🏻👇🏻👇🏻
===============================================

MFARAKANO ULIOPELEKEA ANGUKO LA KANU MWAKA 2002

"......Mwaka 2002 Moi alipanga kukabidhi uongozi wa taifa mkononi mwa Uhuru Kenyatta aliye mtoto wa mzee Jomo Kenyatta kwa njia ya uchaguzi wa rais. Hii ilileta farakano ndani ya KANU. Kundi la Raila Odinga pamoja na wanaKANU wa miaka mingi waliondoka kwa sababu hawakuridhika na Kenyatta kuwa mgombea wa urais.

Wananchi wa Kenya walipendelea chama cha National Rainbow Coalition pamoja na mgombea wake Mwai Kibaki na KANU ilipata kura chache ikarudi bungeni kama chama cha upinzani...."

Matatizo ya KANU kukaribiana na Kibaki

Baada ya 2002 KANU kikiwa chama cha upinzani kiliendelea kukumbwa na kushuhudia mafarakano mengi. Chama kilichobaki kiliongozwa na Uhuru Kenyatta lakini alipingwa na kundi chini ya Nicolas Biwott kilichojitenga kwa muda. 2006 wakajiunga na serikali ya umoja wa kitaifa cha Kibaki.

Kabla ya uchaguzi wa 2007 KANU iliunga mkono muungano wa Party of National Unity ya Rais Mwai Kibaki ikimpigania Kibaki kama rais lakini kuwa na wagombea wake wa pekee. Kenyatta alitangaza ya kwamba KANU itadai cheo cha makamu wa rais.

Uchaguzi wa mwaka 2007

Katika uchaguzi wa 2007 KANU ilishika viti 11 bungeni. Wapinzani wa Kenyatta ndani ya chama walidhoofika baada ya Biwott kutofaulu kutetea nafasi yake bungeni.
Kule ni Kenya mzee
Zenji 2015 walifuta uchaguzi kwan mlifanya nn?
 
Tutafanya nini, tume yao, Jeshi lao, Mahakama zao, Bunge lao, Pesa zao. Sasa yeye Lisu ana nini kama si domo tupu. Hapa ni mwendo wa kushatap mkia juu.
Uchaguzi unafutwa kama zenji tunaanza upya hakuna mtachofanya
 
Tutafanya nini, tume yao, Jeshi lao, Mahakama zao, Bunge lao, Pesa zao. Sasa yeye Lisu ana nini kama si domo tupu. Hapa ni mwendo wa kushatap mkia juu.
Leta mrejesho hapa baada ya uchaguzi kama utakuwa hai.

Jeshi ni lao, mahakama... Nini kiliwasukuma kumhonga mbowe na maridhiano feki kama wanajua hivyo vyote ni vyombo vyao?
 
Leta mrejesho hapa baada ya uchaguzi kama utakuwa hai.

Jeshi ni lao, mahakama... Nini kiliwasukuma kumhonga mbowe na maridhiano feki kama wanajua hivyo vyote ni vyombo vyao?
Just kupunguza kashkash lakini hata wainge muhonga angefanya nini. Wewe unazani kunamtanzania wa kureact hata mmoja, wewe kunywa tu juice yako ulale usilete mchezo mbele ya chuma.
 
Uchaguzi unafutwa kama zenji tunaanza upya hakuna mtachofanya
Upo sahihi kabisa watu wanajidanganya danganya tu. Eti wanamtegemea Trump. Trump mfanya biashara aakipewa mgodi mmoja anaweza hata tuchinjwe tuwekwe kwenye mabucha
 
Katika mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, kuna maswali mengi yanayozungumziwa kuhusu jinsi Samia Suluhu Hassan alivyoteuliwa kuwa mgombea urais kupitia chama hicho. Moja ya masuala muhimu ni kuhusu wapi agenda za kumteua Samia zilipatikana, hasa ikizingatiwa kwamba Kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ya CCM havikuwahi kujadili rasmi suala hilo.

Kwanza, ni muhimu kuelewa mchakato wa uteuzi wa wagombea ndani ya vyama vya siasa nchini Tanzania, hasa CCM. Kwa kawaida, mchakato huu unajumuisha hatua mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kujadiliwa na vikao vya juu vya chama. Hapa ndipo inapotokea kwamba wanachama wa chama wanapewa fursa ya kutoa maoni yao kuhusu wagombea wanaofaa. Katika kesi ya Samia, hata hivyo, ilionekana kama mchakato huu haukufanyika kwa uwazi.

Samia Suluhu, ambaye alikuwa makamu wa rais kabla ya kuchaguliwa kuwa mgombea, alichukua nafasi hiyo baada ya kifo cha rais John Magufuli. Hali hii ya kipekee ilimfanya kuwa chaguo la kwanza kwa CCM, lakini maswali yanayotokana na mchakato wa uteuzi yanaweza kuathiri uaminifu wa chama.

Katika mkutano mkuu wa CCM, ilipigiwa kelele kuhusu umuhimu wa uwazi na demokrasia ndani ya chama. Wanachama wengi walitaka kujua jinsi gani Samia alichaguliwa bila kujadiliwa katika vikao vya kawaida vya chama. Hali hii inaweza kuashiria kuwa kuna mabadiliko katika utamaduni wa kisiasa ndani ya CCM, ambapo maamuzi makubwa yanachukuliwa na watu wachache badala ya kuwa na mchakato wa pamoja.

Aidha, ni muhimu kuzingatia mazingira ya kisiasa ya wakati huo. Tanzania ilikuwa katika kipindi cha majonzi baada ya kifo cha Magufuli, na hali hii inaweza kuwa na athari kubwa katika maamuzi ya kisiasa. Wakati wa kipindi hicho, CCM inaweza kuwa ilihitaji muungano wa haraka na thabiti ili kudumisha umoja wa chama na kuimarisha uongozi wake. Hapa ndipo mchakato wa uteuzi wa Samia unapoonekana kuwa wa haraka, bila kujali taratibu za awali.

Pia, kuna umuhimu wa kuangalia jinsi media ilivyoshughulikia suala hili. Habari nyingi zilitolewa kuhusu uteuzi wa Samia, lakini mara nyingi zilisheheni maswali kuliko majibu. Hakukuwa na waziwazi kuhusu vigezo vilivyotumika kumchagua Samia, na hili lilizua hisia tofauti miongoni mwa wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla. Katika hali kama hii, ni rahisi kwa watu kuanza kukisia kuhusu uhalali wa uteuzi wake.

Kwanza kabisa, ni muhimu kuelewa kwamba mchakato wa kisiasa unahitaji uwazi na uwajibikaji. Wananchi wanahitaji kuona kwamba viongozi wao wanachaguliwa kwa njia ambayo inaheshimu maoni ya wengi. Hii inajenga imani katika mfumo wa kisiasa na kusaidia kuimarisha demokrasia. Katika muktadha huu, uteuzi wa Samia unaweza kuonekana kama kikwazo kwa maendeleo ya demokrasia ndani ya CCM.

Katika kuangalia mbele, ni muhimu kwa CCM kujifunza kutokana na hali hii. Kama chama kinachojivunia historia ndefu na mafanikio, kinapaswa kuzingatia umuhimu wa kuboresha mchakato wa uteuzi wa wagombea. Hii itasaidia kuimarisha uhusiano kati ya viongozi na wanachama na kuleta ufanisi zaidi katika utawala.

Kwa kumalizia, mkutano mkuu wa CCM ulionyesha wazi kwamba kuna masuala mengi yanayohitaji kushughulikiwa kuhusu mchakato wa uteuzi wa wagombea. Ingawa Samia Suluhu Hassan aliteuliwa kuwa mgombea urais, maswali kuhusu jinsi alivyofikia hapo yanaweza kuathiri uaminifu wa chama katika siku zijazo. Hivyo, ni muhimu kwa CCM kuendelea kujadili na kuboresha taratibu zake ili kuhakikisha kwamba mchakato wa kisiasa unakuwa wa uwazi na wa haki.
WanaCCM tumeshaamua mgombea wetu ni mh.Samia.....tuiteni mtakavyo....

#Nchi Kwanza!
 
Mjadala wa nafasi ya urais kwa CCM ulishafungwa, Mgombea wetu ni Mh. Samia Suluhu Hassan na Makamu ni Emanuel John Nchimbi, kwa upande wa Zanzibar Mgombea ni Hussein Mwinyi.

Full stop, tujadili wagombea wa vyama vingine ambao michakato yao bado.
 
Back
Top Bottom