ukisoma kifungu cha 56(4) cha sheria ya ulinzi wa taifa Tz, kinawataka jeshi la ulinzi, kutoa taarifa ya mazoezi yao kwa wakazi wa maeneo husika kama mazoezi hayo yataingia kwenye makazi ya watu, basi na mtu atakaye kaidi au kuingilia mafunzo yao atakamatwa na askari wa jeshi la polisi au ofisa wa jeshi la ulinzi au na askari yeyote wa jeshi la ulinzi kwa amri kutoka kwa ofisa wa jeshi la ulinzi, natena mafunzo hayo yanapaswa yawe na kibali cha maandishi kutoka kwa waziri wa ulinzi s.56(1), na pia kwa waziri wa mambo ya ndani kwa mujibu wa penal code, sasa ni mara ngapi jeshi la kudumu au jeshi la ulinzi hufanya mafunzo karibu na makazi ya watu bila kutoa taarifa kwa wakazi? na tena jeshi hili la kudumu la ulinzi huwa hawatoi hata taarifa ndani ya jeshi la polisi chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kuhakikisha watu hawaingilii mafunzo yao, kwa mujibu wa kifungu nilicho kitaja. nilazima dhana ya kudharauliana katika majeshi yetu yote iondolewe kila askari amuheshimu mwenzie kwa mujibu wa majukumu aliyo pewa na nnchi.
na hata kama ni kutafuta kwamba chombo kipi kina mamlaka juu ya chenzie bado jeshi la polisi litakuwa namba moja kimamlaka kwani ndiyo chombo pekee cha kusimamia sheria zote za nchi, ukisoma sheria ya usalama wa taifa letu utaona kwamba TISS hawana uwezo wa ku enforce sheria bali kuchunguza tuu lkn jeshi la polisi linachuguza na ku enforce, je ? nani zaidi kimamlaka ?
ukisoma kifungu cha 77(1) cha sheria ya ulinzi wa taifa, askari wa jeshi la polisi (police constable) ambaye kimsingi ni police officer anamamlaka ya kumkamata askari wa jeshi la ulinzi ambaye anasadikika kuwa ni mtoro katika jeshi hilo, au ni mtoro kabisa, kisha kumfikisha mahakamani au kumpeleka kwenye kambi yao, sasa mpaka hapo nani ni kiranja wa mwenzie kati ya jeshi la polisi na jeshi la ulinzi ? ingawa nao askari wa jeshi la ulinzi huweza kuwa na mamlaka ya askari wa jeshi la polisi pale watakapokuwa wanasaidia mamlaka za kiraia (yaani ku enforce civilian laws)kwa Kifungu cha 22 cha sheria ya ulinzi wa taifa Tz
ukisoma C.40 ya kanuni ya adhabu ndani ya jeshi la ulinzi (CODE OF SERVICE DISCIPLINE) inatamka kuwa kitendo cha askari yeyote yule wa jeshi la ulinzi kuzuia askari mwenzao au ofisa wao asikamatwe na askari polisi, wa jeshi la polisi ni kosa tena lina stahili adhabu ya miaka isiyopungua miwili, hii ni sheria ya jeshi la ulinzi lenyewe, swali ni kwamba ni mara ngapi askari wa jeshi la ulinzi hugoma kukamatwa na askari wa jeshi la polisi ? kwa kisingizio kuwa wao hawa wezi kamatwa na polisi ? na kwa mujibu wa kifungu hiki nani ni zaidi ya mwenzie ? any way TANZANIA POLICE FORCE IS THE ORIGIN OF MILITARY CIVILIZATION IN TANZANIA, DRAW ITS HISTORY FROM THE GERMANS IN COLONIAL PERIODS , FOLLOWED BY THE NATIONAL SERVICE, UKIACHANA NA KINGS AFRICAN RIFLE YA MWINGEREZA AMBAMO JESHI LA ULINZI HUPATA CHANZO CHA HISTORIA YAKE, NA TENA HATA VIONGOZI WA KWANZA WA JKT WALIKUWA NI POLICE, 'majeshi yote yanamajukumu ya ulinzi wa taifa letu na kuhakikisha usalama, ni lazima askari (wanajeshi) wote wa vyombo vyote muheshimiane na kuthaminiana.
NAHATA KAMA NI MFUMO WA VYEO VYA KIJESHI AMBAO ASKARI WA JESHI LA ULINZI HUTAMBIA SANAAAAAA, BADO WANAPASWA KUKUMBUKA KUWA MKUU WA KWANZA WA JESHI LA POLICE TANZANIA ALIKUWA NA CHEO CHA "MAJOR" ALIITWA "MAJOR DAVIS " alikuja Tanganyika akitokea South Africa (hiki kilikuwa kipindi ambacho tanganyika ilikuwa chini ya uangalizi wa muingereza), BAADA YA HAPO COMMISSIONER ELANGWA SHAHIDI AKAWA MKUU WA KWANZA WA POLICE KWA WAZAWA, NA BAADAYE TULIPO UNGANA NA ZANZIBAR ELANGWA SHAHIDI AKAWA "IGP" WA KWANZA WA POLICE TANZANIA