Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Mitandao ya kijamii ipo kwa ajili ya kuwaleta watu Pamoja kwa namna moja ama nyingine, kubadilishana mawazo na kufikisha ujumbe moja kwa moja kwa jamii na kwa haraka Zaidi, lakini mitandao ya kijamii imegeuka kuwa sehemu ya kushambulia utu na mwanamke kwa ujumla na kufanya wanawake kupata kigugumizi kuingia kwenye mitandao hii na wakati mwingine kutojifunua jinsi zao ili wasishambuliwe.
Si ajabu kukuta lugha za kukera na kuudhi juu ya mwanamke zikitumika mitandaoni, kuwakashfu na kuwaonesha kuwa wao si kitu chochote kwenye jamii ni watu ambao wapo kwa ajili ya kumfurahisha mwanaume au kutekeleza matakwa ya wanaume na hawana cha kufanya Zaidi yah apo.
Nakumbuka ni wanawake wengi maarufu ambao wamekumbwa na kadhia ya kushambuliwa na kudhalilishwa mitandaoni, mifano michache ya wanawake hao ni Wema Sepetu, Miss Tanzania 2006 aliwahi kukutana na kadhia ya kushambuliwa mpaka akaamua kuondoka kwenye mitandao ya kijamii kwa muda Fulani.
Pia Irine Uwoya wote tunajua udhalilishaji aliopitia, na wengine wengi. Selena Gomez amesema huwa anafuta App yake walau mara 2 kwa wiki kukwepa kushambulia. Unaweza kusoma zaidi kupitia kiunganishi hiki Selena Gomez: Huwa nafuta App ya Mtandao wa Instagram kwenye simu yangu walau mara moja kila wiki
Kutokana na kushambuliwa wanawake wengi wanaogopa kuwa na akaunti za mitandao ya kijamii na hizi ni hasara za wao kutokuwa na mitandao ya kijamii.
Nini kitawapata wakiogopa mitandao ya kijamii?
Ni jambo jema kuibua hoja za mabaya wafanyayo wanawake lakini ni vyema kuyaibua kwa lugha za kujenga na kutambua kuwa wao pia ni wanadamu na wana haki ya kukosea na kukosolewa kwa lugha na taratibu njema bila kuwavua utu wala thamani yao.
Kadili mitandao inavyokuwa katili kwa mwanamke kunawafanya wanawake waone mitandao sio salama kwao bali ni sehemu katili inayoweza kuwatweza kisaikolojia na kuogopa kabisa kuingia kwenye mitandao au kuingia na kutoshiriki mijadala au wengine huenda mbali na kujifanya ni wanaume ili angalau wapewe heshima ya kuthaminiwa.
Fida za wanawake kuwepo mitandaoni
Kuwashambulia wanawake mitandaoni hakuwafanyi wabadilike wawe mnavyoaka ila kunawaumiza na kuwaharibu Zaidi achene, badilikeni.

- Kusongwa na upweke
- Wanaathirika kisaikolojia
- Msongo wa mawazo
- Kukosa elimu ambayo wangeweza kuipata mitandaoni
- Kushindwa kufikisha mawazo yao kwa jamii kubwa kwa muda mchache
- Kubaki na taarifa na maarifa ya kizamani
- Kukosa fursa za kiuchumi kama ongezeko la wateja
- Kuwa nyuma kiteknolojia
- Kushindwa kuwa wavumbuzi kwa kukosa maarifa mapya
Ni jambo jema kuibua hoja za mabaya wafanyayo wanawake lakini ni vyema kuyaibua kwa lugha za kujenga na kutambua kuwa wao pia ni wanadamu na wana haki ya kukosea na kukosolewa kwa lugha na taratibu njema bila kuwavua utu wala thamani yao.
Kadili mitandao inavyokuwa katili kwa mwanamke kunawafanya wanawake waone mitandao sio salama kwao bali ni sehemu katili inayoweza kuwatweza kisaikolojia na kuogopa kabisa kuingia kwenye mitandao au kuingia na kutoshiriki mijadala au wengine huenda mbali na kujifanya ni wanaume ili angalau wapewe heshima ya kuthaminiwa.
Fida za wanawake kuwepo mitandaoni
- Kupata taarifa mbalimbali kwa wakati
- Kupata elimu na maarifa mbalimbali
- Mitandao ni fursa za kukuza uchumi kwa wanawake(Kupata wateja wa biashara na kupata njia za kupata fursa za ajira)
- Kuburudisha akili na kuondoa msongo wa mawazo
- Kutengeneza marafiki wapya
- Kuendana na teknolojia mpya na kuwawezesha kuwa wavumbuzi
- Njia rahisi ya kufikisha ujumbe na kueleza mahitaji na matakwa yao nk