Kwanini MO Dewji anataka kufunga kiwanda chake cha chai Nchini Tanzania? Bashe amgomea!

Haiwezekani serikali kumlazimisha mtu asifunge kiwanda. Wakilazimisha usifunge si unakiacha kijifie chenyewe yaani unaacha mali ghafi zilizopo ziishe na wafanyakazi unawaambia kuna hali mbaya ya kiuchumi wanaopenda kuendelea kujitolea bure kwa manufaa ya nchi waendelee wanaotaka malipo haitawrzekana.
 
Daaaah !
 
Mambo si mepesi hivyo. Kama serikali imekuambia njoo tuzungumze tatizo unaenda kuzungumza.
 
Serikali imeweka wazi nia yake ni kuokoa hizo ajira. Binafsi naona wapo sawa. Tatizo la ajira lipo hata kwenye nchi zenye uchumi mkubwa.
 
Kampuni hiyo ilishauri njia zipi mkuu
 
Acha afunge serikali yetu imezidisha sana kodi kila kona
Halafu wanasiasa wetu wakiiba hela za UMMA wanatoroshea nje ya nchi
 
Haya mambo haya... na hapo wakikaa mezani ni kwamba Serikali / Mlipa Kodi ndio atatoa Ruzuku za kufidia kama kuna hasara ili muwekezaji aendelee kuwekeza na kutoa ajira....

In reality kilichotokea baada ya Privatization na hizi Private Sectors kufanya shughuli ni vitu viwili (wakipata faida wanakula wenyewe na wakishindwa mlipa kodi anafidia) win / win for them.....

Cha maana tunahitaji na Kampuni za UMMA zipambane accordingly kwenye market na sio kuwapangia watu Binafsi wanachofanya au wanataka kufanya.... Bila hivyo hizo Kampuni Binafsi zitaendelea kuwa Binafsi mambo yakienda sawa na mambo yakienda ndivyo sivyo ni sisi ndio tutawafidia ili waendelee kuwepo / kuajiri
 
Hapa kazi ipo. Mara wawekezaji wanatakiwa mara ndio wengine wanaaga.
Mara serikali inahamasisha diplomasia ya uchumi mara wababe wanaleta mchele eti umewekwa virutubisho. Huku waziri wa kilimo anatoa maelekezo usitumike kule watu wa viwango wanasema wamecheki ubora
Pamoja na hayo hakuna aliewajibika wala kuwajibishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…