Kwanini MO Dewji anataka kufunga kiwanda chake cha chai Nchini Tanzania? Bashe amgomea!

Kwanini MO Dewji anataka kufunga kiwanda chake cha chai Nchini Tanzania? Bashe amgomea!

Zipo taarifa kwamba Serikali ya Tanzania imekataa ombi la Mohamed Dewji la kutaka kufunga kiwanda chake cha chai.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amemuomba Bwana Dewji kufanya majadiliano na Serikali kwanza kabla hajachukua uamuzi huo, ambao unatarajiwa kuathiri watu wengi wanaofanya kazi kwenye kiwanda hicho.

Lakini swali letu ni hili, kwanini MO amefikia hatua ya kufunga kiwanda chake alichojenga kwa gharama kubwa na kufunga mitambo ya kisasa? Kuna nini?

Swali jingine ni hili, kwanini jambo hili lishughulikiwe na Wizara ya kilimo badala ya Wizara ya Viwanda?

======

Serikali imegoma kuridhia ombi la kufungwa kwa Kiwanda cha chai cha Mo Enterprises na Viwanda vingine kadhaa Nchini ili kuepusha athari ikiwemo Watu kupoteza ajira.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akiwa Dodoma leo, amesema kama Wawekezaji wana changamoto yupo tayari kujadiliana nao ili kuzitatua huku viwanda vikiwa vinaendelea na uzalishaji.

“Nimepokea barua ya kampuni ya Mohamed Enterprise kutaka kufunga Viwanda nimewaambia hawawezi kufunga viwanda, tujadiliane njia nyingine lakini sio kufunga kwasababu kwetu bado sekta ya chai bado ni muhimu kwa ajira za Watu, binafsi naamini nikienda Rungwe kama Wakulima wangekuwa hawana mazao mengine umasikini ungekuwa mkubwa mno kwa hali ya chai ilivyo, Lupembe, Mafinga, Mufindi kote hali ingekuwa mbaya”

“Nimepokea maombi ya MO kuja kwetu Serikali kwamba Serikali tuyachukue mashamba (ili kuyaendeleza) tutaunda Timu itaenda kuyakagua tutaangalia thamani halisi ya wakati huu kwasababu hayakutunzwa vizuri mashamba wala vile Viwanda kwa muda mrefu sana kwahiyo tutaangalia njia zote lakini sekta ya chai itaendelea kuwa hai, nimeagiza hakuna kufunga kiwanda lazima waendeele na uzalishaji hilo ni la lazima kisha tutakaa chini kujadiliana mambo mengine”

“Nawahakikishia ninaendelea na majidiliano na Wizara ya Fedha ili tuwe na njia bora kupima viwango vya tozo, nimeongea na Waziri wa Uwekezaji ili hivi viwanda vipate nafuu ya kodi ya kuagiza nje kwasababu kama tunampa Mtu wa Export sehemu nafuu ya kodi, ukitazama sekta ya chai kwa ujumla bidhaa zake zinahusisha kusafirisha nje”

“Nimekaa na Timu ya Wataalamu imenifanyia uchambuzi wa bei ya majani mabichi ya chai, kwa namba inatakiwa bei ishuke lakini nimewaambia bei ya Mkulima haitoshuka tuta-mantain bei ya mwaka jana” —— amesema Waziri wa Kilimo
Mwulize MO mwenyewe
 
[QUOTE="Erythrocyte, post: 49772889, member:
Swali jingine ni hili, kwanini jambo hili lishughulikiwe na Wizara ya kilimo badala ya Wizara ya Viwanda?

======
“Nimepokea barua ya kampuni ya Mohamed Enterprise kutaka kufunga Viwanda nimewaambia hawawezi kufunga viwanda, tujadiliane njia nyingine lakini sio kufunga kwasababu kwetu bado sekta ya chai bado ni muhimu kwa ajira za Watu, binafsi naamini nikienda Rungwe kama Wakulima wangekuwa hawana mazao mengine umasikini ungekuwa mkubwa mno kwa hali ya chai ilivyo, Lupembe, Mafinga, Mufindi kote hali ingekuwa mbaya”

“Nimepokea maombi ya MO kuja kwetu Serikali kwamba Serikali tuyachukue mashamba (ili kuyaendeleza).......
[/QUOTE]

Huyu mbowe inabidi ashitakiwe kwa kuaageuza ndg zetu wachache kuwa manyumbu kabsaaa wasioelewa chochote milele. Hebu angalia maelezo ya waziri hayo hayo na hilo aliloliita 'swali' lake la pili.
 
Kuna mambo fulani kama muajiri ni lazima aitaarifu serikali, hawezi kufunga tu.
🤣🤣🤣🤣

Mkuu tunahitaji sana elimu humu, haki ya nani tena. 'Great thinker' anashauri Mo angefunga tu bila kuitaarifu serikali🤣🤣🤣🤣.

'Great thinker' inaonekana mpaka leo anajua hakuna utofauti wowote wa uendeshaji kati ya viwanda vikubwa na viosk vyetu vya pipi huku kwa mwananyamala na goba🤣🤣🤣🤣🤣

Nimecheka sana!!!!
 
Mkuu,

Kuna wengine wanagenzi. Wengine wanetu. Wengine wanajifunza.

Kuna kila aina ya watu hapa.
 
Sasa wafanyeje zaidi wamuue kwa High Blood Pressure? Mali kachuma humo humo CCM, leo anataka kuwakimbia, watamkata visigino.
Basi ndio maana wanalia lia utakuta walitakatisha hela humo sasa wanaona anawatapeli 😄
Money laundering ipo
 
Back
Top Bottom