Kwanini Mo Dewji anavumilia hasara Simba?

Kwanini Mo Dewji anavumilia hasara Simba?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kila Simba inapoingia robo finali mashindo ya CAF Tajiri Mohamed Dewj anajitokeza hazarani kudai anapata hasara kwelikweli kwa kuidhamini Simba, Ni kwanini hasara anazopata zinatangazwa kwenye sasa na kwanini avumilie hasara zinazomkera?

Je, unapogharamia kitu unachokipenda sana hiyo inaitwa hasara au matumizi? Yaani unatoa hela kutunza familia, kunywa pombe, kivuta sigara au kumpa mchepuko wako hayo ni matumizi yako au ni hasara?

Mo anasema yeye ni Simba lialia tangu utotoni, Simba ikifungwa analia kwelikweli na anaapa kwa jina la mama yake kuonyesha kuwa Simba ni starehe yake kama sigara na mazoezi ya mwili gym. Sasa inakuwaje starehe yake imtie hasara?

Je, anapovuta sigara anapata faida gani? Mbona hatangazi hazarani hasara anazopata kwenye matumizi yake mengine binafsi kama familia, kumtembelea Ndugu na jamaa, kivuta sigara, kwenda gym, nk.

Starehe ni gharama Kwanini haachi kama anapata hasara asizozipenda Simba?
 
Duniani hayupo anayefanya biashara ya hasara kisha akaendelea nayo tena kwa kuing'ang'ania kama gundi kwenye mbao. Huyo Mo ni muongo kama waongo wengine, kama anaona hasara awaachie wengine.

Kwenye jezi ya Simba kuna mabango ya Mo zaidi ya matatu, hebu atoke hadharani aseme mabango hayo ameilipa Simba bei gani kisha atuambie asingetumia jezi ya Simba kutangaza biashara zake huko kwenye media angelipa kiasi gani?
 
Duniani hayupo anayefanya biashara ya hasara kisha akaendelea nayo tena kwa kuing'ang'ania kama gundi kwenye mbao.
Huyo Mo ni muongo kama waongo wengine, kama anaona hasara awaachie wengine.

Kwenye jezi ya Simba kuna mabango ya Mo zaidi ya matatu, hebu atoke hadharani aseme mabango hayo ameilipa Simba bei gani kisha atuambie asingetumia jezi ya Simba kutangaza biashara zake huko kwenye media angelipa kiasi gani?
Kama Hailer kalipa 1.5b kuitangaza bidhaa zake kwenye jezi za Yanga kwa muda mfupi sana wa mashindano TU ya CAF je yeye kwa miaka 6 yote matangazo ya bidhaa zake yako kwenye jezi za Simba ingestahili kulipa ngapi?
 
Wajinga ndiyo wanakubaliana na yeye, ila werevu hilo hatulikubali abadani.
 
Kama Hailer kalipa 1.5b kuitangaza bidhaa zake kwenye jezi za Yanga kwa muda mfupi sana wa mashindano TU ya CAF je yeye kwa miaka 6 yote matangazo ya bidhaa zake yako kwenye jezi za Simba ingestahili kulipa ngapi?
sisi simba tunahitaji chama atupe furaha tu mihasara hiyo atajijua mwenyewe!

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Kifedha kwake ni hasara siwezi mbishia maana hakuna ata mmoja wetu aliyeona vitabu vya kumbukumbu za pesa zake zinavyotoka na kuingia kwenda simba.

Yuko sawa.
Tueleze kwanza thamani ya x kwenye hesabu hii hii ifuatayo: kama m-bet analipa 3b kwa mwaka kwa tangazo moja TU kwenye jezi, je, matangazo 5 ya mo kwa miaka 6 ni bei ngapi?

Lakini atuambie pia thamani ya furaha yake anayoipata wakati Simba ikishinda mechi ni sh. ngapi?
 
Kama inapata hasara mbona hawakutafuta mdhamini kwwnye haya mashindano ya CAF kwenye kutangaza bidhaa zake kwenye jezi za Simba upande wa kifuani mpaka tukaweka VISIT TANZANIA!
 
Kama inapata hasara mbona hawakutafuta mdhamini kwwnye haya mashindano ya CAF kwenye kutangaza bidhaa zake kwenye jezi za Simba upande wa kifuani mpaka tukaweka VISIT TANZANIA!
Wanalipwa na Tanapa?
 
Duniani hayupo anayefanya biashara ya hasara kisha akaendelea nayo tena kwa kuing'ang'ania kama gundi kwenye mbao.
Huyo Mo ni muongo kama waongo wengine...
Wacheza kamari wanafanya biashara ya hasara wakiamini ipo siku atabutua mbele ya safari
 
Kifedha kwake ni hasara siwezi mbishia maana hakuna ata mmoja wetu aliyeona vitabu vya kumbukumbu za pesa zake zinavyotoka na kuingia kwenda simba.

Yuko sawa.
Sasa kama hakuna aliyewahi ona vitabu utakubalije kuwa anapata hasara??
 
Back
Top Bottom