Kwanini Mo Dewji anavumilia hasara Simba?

Kwanini Mo Dewji anavumilia hasara Simba?

Simba sio timu ya baba yako Wala mama yako kwanini uvumilie hasara zinazokuumiza? Kama una mahaba na Simba na ndio furaha yako tangu utotoni kwanini unalia hasara mbele ya camera? Starehe yako unaiitaje hasara? Mbona hasara ya kununua sigara huitangazi hazarani?
 
Mwekezaji ameshanusa mnuso wa hela CAF. Hapo anataka na yeye mgao, kisa anaichangia simba. Mwisho wa siku timu inajikuta iko pale pale. Hakuna hatua yoyote ile inayopigwa kwenda mbele.

Kama kitu kinakuletea hasara, bwaga manyanga ili maisha yaendelee. Maana hakuna mtu aliyemshikia bunduki kuendelea kupata hiyo hasara. Kinyume na hapo, watu waamini Mhindi analeta porojo.
 
Mtu akimuuliza swali la Ile 20b Iko bank gani au soko gani la hisa anamuona mchimbi, nuksi asiyefaa na anaeitakia mabaya Simba.
 
Kila Simba inapoingia robo finali mashindo ya CAF Tajiri Mohamed Dewj anajitokeza hazarani kudai anapata hasara kwelikweli kwa kuidhamini Simba, Ni kwanini hasara anazopata zinatangazwa kwenye sasa na kwanini avumilie hasara zinazomkera?

Je, unapogharamia kitu unachokipenda sana hiyo inaitwa hasara au matumizi? Yaani unatoa hela kutunza familia, kunywa pombe, kivuta sigara au kumpa mchepuko wako hayo ni matumizi yako au ni hasara?

Mo anasema yeye ni Simba lialia tangu utotoni, Simba ikifungwa analia kwelikweli na anaapa kwa jina la mama yake kuonyesha kuwa Simba ni starehe yake kama sigara na mazoezi ya mwili gym. Sasa inakuwaje starehe yake imtie hasara?

Je, anapovuta sigara anapata faida gani? Mbona hatangazi hazarani hasara anazopata kwenye matumizi yake mengine binafsi kama familia, kumtembelea Ndugu na jamaa, kivuta sigara, kwenda gym, nk.

Starehe ni gharama Kwanini haachi kama anapata hasara asizozipenda Simba?
Liongo hilo.
 

Attachments

  • FB_IMG_1687611530512.jpg
    FB_IMG_1687611530512.jpg
    62 KB · Views: 3
Anasema Simba ni timu yake ya utotoni, anaipenda sana, lakini marà kwa mara anasikika akisema anapata hasara, ni nani anamlazimisha kuingia hasara hizo? Kwanini haanzishi timu yake kama wengine? Kama Haier kwa miezi 2 TU ya kutangàzwa na Yanga ametoa 1.5b mon angepaswa kulipa nagapi kwa kifusi chote kile Cha matangazo yake kila Kona ya jezi, na mitandao ya Simba?
 
Back
Top Bottom