Kwanini Mo Dewji anavumilia hasara Simba?

Simba sio timu ya baba yako Wala mama yako kwanini uvumilie hasara zinazokuumiza? Kama una mahaba na Simba na ndio furaha yako tangu utotoni kwanini unalia hasara mbele ya camera? Starehe yako unaiitaje hasara? Mbona hasara ya kununua sigara huitangazi hazarani?
 
Mwekezaji ameshanusa mnuso wa hela CAF. Hapo anataka na yeye mgao, kisa anaichangia simba. Mwisho wa siku timu inajikuta iko pale pale. Hakuna hatua yoyote ile inayopigwa kwenda mbele.

Kama kitu kinakuletea hasara, bwaga manyanga ili maisha yaendelee. Maana hakuna mtu aliyemshikia bunduki kuendelea kupata hiyo hasara. Kinyume na hapo, watu waamini Mhindi analeta porojo.
 
Mtu akimuuliza swali la Ile 20b Iko bank gani au soko gani la hisa anamuona mchimbi, nuksi asiyefaa na anaeitakia mabaya Simba.
 
Liongo hilo.
 

Attachments

  • FB_IMG_1687611530512.jpg
    62 KB · Views: 3
Anasema Simba ni timu yake ya utotoni, anaipenda sana, lakini marà kwa mara anasikika akisema anapata hasara, ni nani anamlazimisha kuingia hasara hizo? Kwanini haanzishi timu yake kama wengine? Kama Haier kwa miezi 2 TU ya kutangàzwa na Yanga ametoa 1.5b mon angepaswa kulipa nagapi kwa kifusi chote kile Cha matangazo yake kila Kona ya jezi, na mitandao ya Simba?
 
Ujanja mwingi, mbele giza. Ipo siku ataumbuka tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…