Kwanini Mo mwenye hisa 49% Simba atoe bilion 20 na wengine wenye hisa 51% hawatoi hela yeyote

Hebu nieleweshe, janja janja ya MO ni ipi'? Kama pesa anatoa..tafadhar mzee nieleweshe hio janja janja ya MO ni ipi?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] na kweli ni yKe
 
kwa hiyo wanachama wameweka bil 22 sio?
 
Kwa ufupi ni kwamba hizo 51% zilitengwa makusudi kusudi Muwekezaji asijejejichukulia Club Kirahisi. Lengo ni kwamba wanachama pindi watakapokuwa tayari kwa mda maalum wazinunue. Pia MO kwa kuanzia tayari aliahidi kuwanunulia wanachama hisa za thamani ya 500,000 kwa kila mwanachama katika kuwasaidia kufikia lengo lao la kumiliki 51%. Kama ungekuwa ni mzigo asingeingiza miguu yake. Na mbaya zaidi mpaka sasa wakati tunaposubiria mchakato umalizike yeye MO ndiye anaiyefaidi saana kupitia matangazo ya biashara na mapato yote kwa hivi sasa yote yapo chini yake (anazungushia biashara zake).Kwa mfano aliingia mkataba na Club wa kutangaza bidhaa moja tu ya Mo Extra ila sasa amechomekea MO Halisi na MO Protector
 
Mo hata kama angetoa billion 100 lazima zirudi na faida kupitia upangaji wa matokeo ili kushinda mikeka yake anayokuwa amebet
 
Mali za simba SC ndio hizo 51%
 
Mazee at times tuwe tunatumia akili kidogo, Mo alininunua asilimia 49 ya Simba kwa bil 20, mzigo huu alipaswa autoe wote ndio hoja ya pesa za management ya club ifuate.
Pia Mo hawezi kufanya maamuzi peke yake kwani bado siyo majority shareholder. Mwanzoni alitaka kununua 51% ya hisa ili aweze kufanya maamuzi ila serikali ilikataa ndio maana akapewa 49% ili wanasimba / shareholders wengine wawe na maamuzi makubwa.
 
Ada ya uanachama walikuwa wanalipiwa wakati wa uchaguzi. Hawawezi kununua hisa.
Bei ya hisa moja haijulikani. Kuna tetesi ni laki nne
 
Una kichwa kigumu sana.
Umeambiwa wanachama walikuwa wanamiliki club 100% sasa wameamua kumuuzia muwekezaji 49% ya kile wanachokimiliki na bado unataka waweke na 22bill!!!!! Yani wewe uwe na duka la nguo umuuzie mteja jeans moja kwa 10k then umuongezee na 12k juu itakuwa unafanya biashara au upuuzi. Wanachana ndiyo wamiliki wa club na ndiyo walioamua kuiza sehemu ya umiliki wao
 

Kitu kimoja cha kuelewa, hiyo 51 inasimama kwa ajili ya klabu.

Hao wenye 51 percent mchango wao ni kuifikisha hapo alipoikuta Mo. Kama unadhani ni rahisi, mwambie akaanzishe timu yake aone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…