Uchaguzi 2020 Kwanini Mpango na Tulia Ackson wasigombee wajimbo huru ya Dar es Salaam?

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Kwa kweli huwa sielewi kwa nini kila mtu afikirie kwenda kugombea kwao tena kwa watu maarufu na ambao wanajidai kua wamefanya mambo makubwa.

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania anarudi kwenda kugombea Mbeya nyumbani kwao, yeye ni mtu maarufu ni wa nini asigombee majimbo huru kama yaliyoko hapa Dar. Dar es Salaam haina mwenyewe, haina wenyeji. Wakazi wa Dar es Salaam aanahitaji kusikiliza hoja tu.

Nashangaa kusikia hata waziri Mpango ana nia ya kwenda kumuengua Obama kwenye jimbo lake kwa kigezo kua ni nyumbani kwao. Mpango ni mtu maarufu halafu ni mwanaume kwa nini asipambane majimbo huru kuliko kwenda kutafta mteremko wa unyumbani?

Leo nimemsikia Master J anasema na yeye anaenda kwao Rombo kugombea, cha ajabu Master J ni maarufu sana hapa Dar kuliko kwao Rombo, kwa nini asigombee Dar ambapo kwanza ni majimbo huru, pili ndio alikoishi sana na kufahamika sana kuliko kwao Rombo.

Kwanini watu wanapenda mteremko wa unyumbani? Mimi nitakapokuja kutaka kugombea sina sababu ya kurudi kwetu Singida kugombea kwa kutafta mteremko wa eti ni nyumbani. Nakomaa kwenye majimbo huru.
 
Sioni tatizo as long as hawatendi kosa..nadhani ni suala la maamuzi tu! Ustaarabu huanzia nyumbani.
 
Kuna maeneo watu wameshafunguka akili huko vyama vya upinzania vinaweza kufanya vizuri zaidi; ila kule kwa wajinga ccm inapeta.
 
Back
Top Bottom