M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,027
Nyumba ndogo ruksa.Hiyo ni akaunti binafsi ya Haji Manara na sio akaunti ya Simba! Kwa maana nyingine, anayetangaza hiyo bidhaa sio Msemaji wa Simba bali Haji Manara! Na kwa maana nyingine, hata Mo anaweza kutangaziwa bidhaa zake na Haji Manara lakini atatakiwa kumlipa Haji yeye binafsi, na malipo hayo hayataingia kwenye vitabu vya Simba!!! Na kwa maana nyingine tena ya msisitizo, hata GSM nao wanaweza kutangaziwa bidhaa zao na huyo huyo Haji Manara kwenye akaunti hiyo hiyo ya Haji Manara kama ambavyo Mo Dewji anavyoweza kutangaziwa bidhaa zake kwenye akaunti binafsi ya Antonio Nugaz!!
Na pia usisahau, kuna Kampuni ya Azam na Azam FC! Na pia kuna Simba SC na Mohamed Enterprises!!Nazi ni za Azam (kampuni) na sio za Azam FC!! Mshindani wa Simba SC ni Azam FC na sio Azam Kampuni! Na Mshindani wa Mohamed Enterprises sio Azam FC bali Azam Kampuni!!
On a serious note, tusisahau kuwa Mbumbumbu FC na Azam wana undugu fulani japo si wazi sana (ni kama ule wa Vyura FC na Singida).