Kwanini msemaji wa Club ya Simba anatangaza bidhaa za pinzani kibiashara? Inawezekana vipi?

Kwanini msemaji wa Club ya Simba anatangaza bidhaa za pinzani kibiashara? Inawezekana vipi?

Kuna tatizo, MO ana maji ya kunywa iweje Manara atangaze maji ya Azam?

Haji awezi tangaza maji ya Mo kama hajapewa deal yani atumie nguvu zake kumtajirisha mtu ?

Azam wanamlipa Mo na Simba makubaliano yanaisha kwenye Timu tu basi
 
Kuna kitu sijakielewa na hiki ni vigumu sana kukiona kwenye nchi zilizo endelea hass Ulaya huko.

Haji Manara ni Msemajo wa Club ya Simba na Mdhamini au mmiliki wa Club no Mo,
Mo ana boadhara zake nyingi sana, ana maji, ana aina mbalimbali za vinywaji, ana unga wa ngano kwa kifupi ana product nyingi sana na ziko hadi kwenye jesi za timu.

Ila hii ya Manara kutangaza product za Azam sielewi inawezekana vipi, how come anaye jua anisaidie kwamba inawezekana vipi? Na product anazo tangaza no the same na zonazo zalishwa na Bosi wake.

Kwa wenzetu hiki hakiwezekano Milele.View attachment 1664410
Unajuaje kama Manara amehamia Azam FC
 
Hivi haji leo atajisikiaje au ataelewa vip ikitokea mo kila siku anamsifia msemaj wa timu nyngne mfano masau au bumbuli
Kha!!! Nyinyi watu nyinyi! Kwahiyo kumbe hata Mo hatakiwi kumsifia Msemaji wa Timu nyingine?! Hivi hapa nabishana na Simba au na Vyura wa Utopoloni?!
 
Ata kama ila sio vzur anachofanya ni bora angekua baloz wa bidhaa za mo ,ni sawa bumbul au nugaz leo waanze kutangaza bidhaa nyngne mfano magodoro dodoma au unazan itakuaje
Sasa kwanini wasitangaze?! Kwani hao akina Nugaz ni waajiriwa GSM?!
 
Sasa mbona iyo unayosema akaunt yake binafs anaitumia kutangaza mambo ya simba
Ndo uzuri wa kumiliki kitu huo! Ni akaunti yake binafsi na ndo maana pia anaitumia kutangaza habari za Simba kwa mapenzi yake lakini HALAZIMIKI kuitumia kutangaza habari za Simba, na ndio maana pia 👇👇👇
Hsji.png
 
Maji ya Uhai wana compete na maji ya Masafi ya Mo, Manara anawezaje kutangaza maji ya Uhai?
Sasa Haji ana uhusiano gani na maji ya Masafi hadi ashindwe kutangaza maji ya Uhai?!! Hivi mnajisikiaje mnavyodhani mna uchungu sana na biashara za Mo Dewji kuiliko hata Mo mwenyewe?! Yaani mnaumia Haji kutangaza bidhaa za Azam kuliko hata anavyoumia Bababra?!
 
Nenda kwenye account ya Manara kuna product kama Maji ya Uhai anayanadi sana, MO ana maji pia ya Uhai
Mkuu Maji ya Mo si ni moja ya Wazamini wa Simba? Masafi? Whay Manara atangaze maji ya Uhai?
Ndo hapo jiulizeni sasa! How come mnaumia nyie badala ya Mo mwenyewe?! Au hayo maji kaanza kuyatangaza sasa?!
 
Bidhaa kama"maji ya Uhai"ni ya Bakhresa.
Bidhaa kama"maji Masafi"ni ya Mo.
Simba ni timu ya mpira.
Mo ni muwekezaji Simba.
Manara ni msemaji wa Simba.
Manara ni balozi wa bidhaa za Bakhresa kama"Vinywaji,usafiri wa majini,Ice cream,Ngano n,k.
Apo akuna shida.ila kwakuwa Uto ni
washamba na wanaroho mbaya,wataona ni tatizo.
Mfano Azam tv wakatae kuonyesha mechi za Simba kwa kuwa kwenye jezi za Simba kuna nembo ya kinywaji ambacho kwenye Azam group wanacho.
Akili kama hizi wanazo Yanga,walikataa nembo nyekundu ya Vodacom na gsm kwakuwa zinarangi nyeupe na nyekundu zinazotumiwa na timu ya Simba.
 
Nazan Haji katangaza tui hili ili kulididimiza tui la GSM
 
Wewe ni mpumbavu Sana ndio mnafanya wasomi waonekane ni wajinga.


Hujui Kama MO dewiji pia kupitia bidhaa zake anaidhamini Simba kwa hizo bidhaa? Huoni Kama msemaji kupromoti baadhi ya bidhaa ambazo Mdhamini wake pia anaidhamini Simba kunatokea mgongano wa kimaslah
Hapa ndio unazungumzia Conflict of interest halisi.Hili liko wazi.Kwa Kesi ya Haji, Azam Nazi sio mpinzani wa Simba Sports Club.Hivyo hakuna Conflicts of Interest.Haji ni Balozi wa Azam.Haji atatangaza bidhaa zote za Azam lakini hatotangaza Azam FC kwa vile Azam FC ni mpinzani wa Simba Sports Kibiashara.

Azam TV anatangaza Matangazo ya Simba, lakini Simba ni mpinzani wa Azam FC, na Mmiliki wa Azam FC na Azam TV ni Mmoja, hakuna shida sababu Azam TV sio Mshindani wa Simba Sports Club
 
Kwahiyo tumkute mwanaccm anapost Mambo ya Chadema kwenye account Yake kisa ni account binafsi.


Unajua terms and conditions za mkataba kuhusu conflict of interest ?
Punguza ujuaji ndugu...mbona hata mbele kina Rinaldo na messi unakuta wanaingia mikataba binafsi na makampuni ambayo hata hayasupport timu kama Nike,adidas etc
 
Kwahiyo tumkute mwanaccm anapost Mambo ya Chadema kwenye account Yake kisa ni account binafsi.

Unajua terms and conditions za mkataba kuhusu conflict of interest ?

Mkuu kasome logic hata ile ya civics form 5 na 6. itakusaidia sana kwenye haya mambo madogo madogo ambayo wazee wetu walikuwa nayo katika Common Sense tu.
 
kweli mkuu, ko azam tv kutangaza mechi za simba ni kosa
Hivi muheshimiwa mbowe anaweza kutangaza kofia na mashati ya ccm ?
Halafu ikajengwa hoja ya kumtenganisha mbowe na chadema?

Kwanini watanzania tunakubali kufanywa wapuuzi kwa hoja za kipuuzi?

Hivi manara popote pale utamtambulisha kama msemaji wa simba,,?
Au utamtambulisha kama nani?

Hapo mwambieni kakosea,,,angeweza kutangaza zingine na sio brand za watu ambao wapo kwenye ligi moja.

Kumbuka azam pia ni brand.
 
Hao wote wanalipwa na nani?
We jamaa yani uko mweupe halafu hujui kuwa uko mweupe.
Kampuni kadhaa kumilikiwa na mtu mmoja haina maana zinaingiliana kiutendaji na ndiyo maana ya kuwa na makampuni tofauti. Mfano assume una kesi na AZAM FC mahakama imekupa kibari ukashikilie mali zake, huwezi kwenda kushikilia mali za Uhai maana ni kampuni nyingine tofauti na AZAM FC japo zote mmiliki ni mmoja.
Tofautisha kati ya AZAM FC na AZAM wanaotengeneza nazi, ndiyo maana hawaingiliani katika utendaji, kila kampuni ina management yake na kila kitu chake. Manara katangaza bidhaa ya AZAM ambayo haina mahusiano na AZAM FC. Yani point ni kwamba haya ni makampuni mawili tofauti yanayofanya shughuli tofauti.
 
Back
Top Bottom