Kwanini mtoto anampiga mama yake (3years)

Trubarg

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2020
Posts
4,388
Reaction score
7,223
Wadau na wazoefu naomba tuelezane. Mtoto mdogo wa ana umri wa miaka mitatu lakini huwa anampiga mama yake na wakati mwingine kumng'ata.

Mama yake akimkataza kitu anamfuata na kuanza mpiga au kumrushia kitu au kumuuma meno..

Nikirudi mm nyumbani kutoka miangaiko yangu hataki mtu amguse zaidi yangu..si kumlisha wala kumuogesha...

Wadau kuna mwenye uzoefu na Hili..nini inaweza kuwa reason...
 
Huyo mtoto ni ke au me?
 
Kuanzia miaka 3-5 mtoto wa kike anakuwa na mapenzi kwa baba yake. Humuonea wivu mama yake na anakuwa na hasira naye kwasababu ya ukaribu uliopo kati mama yake na wewe.
Asee
 
Oedipus complex ni ile hali unakuta mtoto wa kiume anakuwa karibu sana na mama yake , ila kwa mtoto wa kike hiyo hali inaitwa oedipus elektra.. yaani mtoto wa kike anakuwa karibu na baba yake .. hiyo ni nature ya maswala mazima ya bayolojia ....na hiyo hali ikizidi sana(huo ukaribu) ni hatari sana tena sana ... Inaweza pelekea INCEST

MÊmENtO HoMO
 
Umri huo ni kawaida sana kuwa na tabia ya kususa. Kanalia huku kanagaagaa chini. Kanakuwa na ukorofi uliopitiliza. Lkn hiyo hali siyo ya kudumu. Akianza kupita miaka 5 anaanza kubadili tabia pole kwa pole.
Hiyo hali itaisha tu.
 
Mtoto atandikwe fimbo za maana akimfanyia ivo mama yake. Kanaonekana kamedekezwa sana na baba yake.
3yrs... Fimbo za maana? πŸ€”πŸ€”πŸ€”
Akifanya kosa alafu umchape fito, sio fimbo, kiasi tu, kesho akijaribu kurudia akikuangalia machoni tu, anaacha kufanya so inaingia kwa akili kidogo kidogo kuwa hilo jambo sio poa kufanya yeye. Lakini ukimchapa fimbo za kishua mtoto wa miaka 3, 1-umuumize bila kukusudia, 2-bahati mbaya azime(umenielewa hapo) ukiwa unamchapa, kazi kwako, 3-ni makosa kisheria. Mwisho, nikikupata nakuadhibu mimi mwenyewe, vibao vya kutosha, hivi huoni ni mtoto huyo!? 🀣 🀣 🀣 🀣 🀣 🀣 🀣
 
Mnadekeza vibaya,kachapwe kawe na adabu. Mama mtu nae anachekelea tu aiseee
Kazi kwa mama, huyo mtoto ni mdogo kwa baba kuingilia. Alafu sio kuchapa ile unajua, hako ukikachuna tu kanakuwa sambamba! 🀣
 
Hio tabia ya huyo mtoto haitabadilika kama wadau wanavyoshauri ndo kwanza atakua kiburi zaidi. Samaki mkunje angali mbichi
Kazi kwa mama, huyo mtoto ni mdogo kwa baba kuingilia. Alafu sio kuchapa ile unajua, hako ukikachuna tu kanakuwa sambamba! 🀣
Kanakula tu fimbo au kifinyo kawe na adabu. ka hivyo katakuaibisha mbele za wageni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…